Friday, June 28, 2013

AJALI YA LORI LA MAFUTA KIBAHA2093648 orig 8c4d3
WATU NA VIDUMU VYAO KAMA KAWAIDA YAO BADO MATUKIO KAMA HAYA YALIYOTOKEA AWALI NA KUSABABISHA VIFO VYA MAMIA YA WATU HAYAJAWAFUNDISHA

7076096 orig aa465
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA BLOG

UTARATIBU HUU UTAENDELEA BAADA YA OBAMA KUONDOKA?CHEZEA OBAMA WEWE?HARAKATI ZA USAFI ZIKIENDELEA KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA JIJI LA DAR.(picha kwa hisani ya demashonews)

Thursday, June 27, 2013

SIMBA YAMPA KISOGO KIPA WAO NAMBA MOJA JUMA KASEJA

JUMA KASEJA

WAKATI ALIPOKUWA TIMU YA YANGA

AKIBEBWA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA KUFANYA VIZURI UWANJANI

AKIWA KAZINI

Kipa namba moja wa timu ya Simba  na Taifa Stars Juma Kaseja,amepewa kisogo na klabu yake yenye maskani yake mtaa wenye pilika nyingi za kila siku Kariakoo.
Akiongea katika kipindi cha michezo cha Radio One stereo mwenyekiti wa kamati ya usajili Hans Pope amesema hawatamsajili tena kipa huyo hivyo atafute sehemu ya kwenda.
Juzi iliripotiwa kwenye gazeti la Nipashe kuwa kocha mkuu wa timu hiyo alisema anamshauri Juma Kaseja kama mwanae kuwa atafute kitu kingine cha kufanya kwani mashabiki wengi ambao wamekuwa wakifika kwenye mazoezi ya timu hiyo wamekuwa wakimpigia kelele kocha hhuyo kuwa hawataki kumuona tena kipa huyo katika timu hiyo kwani amekuwa akiwababaisha sana.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba kipa huyo amegoma kusaini mkataba mpya na klabui yake hiyo kwa kutokubali kiasi timu ilichopanga kumpatia na yeye alikuwaa anataka kiwango cha juu zaidi.Lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Juma Kaseja ilikuwa apewe milioni 20 ili asaini mkataba mpya na yeye hakukubaliana na kiwango hicho akitaka apewe  milioni 40 kiasi ambacho kamati ya usajili ya timu hiyo imesema hakina pesa hizo za kumlipa kipa huyo hivyo atafute pa kwenda na hawatampa mkataba tena.

Friday, June 21, 2013

MAPOKEZI YA DAVID BECKHAM CHINA YASABABISHA WATU KUKANYAGANA NA BAADHI WAUMIA VIBAYA WAKIWEMO MAAFISA USALAMAM


MAAFISA USALAMA WAKIWA KATIKA WAKATI MGUMU KUWAZUIA MASHABIKI

AFISA USALAMA ALIEJERUHIWA
ANGALIA KILA MMOJA ALIINUA SIMU YAKE JAPO APATE PICHA INGEKUWA BONGO SIJUI KAMA KUNA SIMU INGESALIMIKA HAPO

UMATI UKIHANGAIKA JAPO KUPATA PICHA

WENGINE WALIONA BORA WAGUSE HATA GARI TU
Watu watano wamejeruhiwa vibaya katika mapokezi ya David Beckham nchini China baada ya umati mkubwa kujitokeza kumlaki na kutaka japo kumgusa.Licha ya kuustaafu lakini bado mashabiki wake walifurika katika jiji la Shanghai hali iliyosababisha watu watano kujeruhiwa akiwemo polisi.
Katika ratiba yake hiyo jana Beckham alikuwa atembelee chuo kikuu cha Shanghai cha Tongji.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid alikuwa akutane na wachezaji wa timu ya chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba kuitangaza ligi kuu ya China imayptambulika kama Chinese Super League.
Hata hivyo kufuatia umati mkubwa kujitokeza kwa lengo la kumlaki kiungo huyo wa zamani wa England kumesababisha zoezi hilo kushindikana ambapo baadae aliomba radhi kwa mashabiki wake hao kupitia mtandao wa kijamii wa facebook na Sina Weibo.
Maafisa Usalama walishindwa kuzuia vurugu hizo ambapo walikuwa wakisonga mbele licha ya kuwekewa kizuizi.
Katika ujumbe wake Beckham amenukuliwa akisema"Samahani sikuweza kutokea uwanjani kuiona timu kwani ilikuwa ni vigumu kupenya kati kati ya mashabiki.Nimesikia kulikuwepo na watu waliojeruhiwa,Nina matumaini wako salama na nawatakia heri wapone haraka''
Takriban watu 1000 inaaminika walikuwa wanataka japo kumkaribia Beckham na polisi wamethibitisha kuwa maafisa wake watatu walijeruhiwa katika vurugu hizo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 38 alistaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuisaidia Paris-Saint Germain kutwaa taji la ligi ya Ufaransa maarufu kama league 1.

MBUNGE WA KASULU MJINI MH MOSES MACHALI APIGWA MKOANI DODOMA

MBUNGE WA KASULU MJINI MH MOSES MACHALI
Habari   kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana , tukio hilo limetokea jana jioni  wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.

Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo. 


Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.

.(HABARI KWA HISANI YA  LEWIS MBONDE BLOG)Tuesday, June 18, 2013

Sunday, June 16, 2013

KUFUATIA MLIPUKO WA JANA,TUME YA UCHAGUZI IMEAHIRISHA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA TANO ZA JIJI LA ARUSHA

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA
Tume ya taifa ya uchaguzi imeahirisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata tano za jiji la Arusha uliopangwa kufanyika hii leo,kufuatia tukio la mlipuko uliotokea jana huko Mkoani Arusha katika mkutano wa kuhitimisha kampeni kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,na kusababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya na mlipuko huo.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii kwa njia ya simu kutoka Zanzibar,mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema uchaguzi huo utafanyika June 30 mwaka huu na kwamba hali hiyo itawapa nafasi vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha zaidi ulinzi siku ya uchaguzi huo.

Saturday, June 15, 2013

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...