Friday, August 30, 2013

PICHA MBALI MBALI ZIKIMUONESHA DIAMOND AKIMZAWADIA MZEE GURUMO GARI

AKIMKABIDHI GARI AINA YA TOYOTA FUNGARCO

MZEE GURUMO NDANI YA MKOKO WAKE

AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKABIDHI GARI MZEE GURUMO

GARI AINA YA FUNCARCO AMBAYO DIAMOND AMEMKABIDHI MZEE GURUMO


Mwanamuziki wa kizazi kipya anae kick kila kona Diamond Platnumz jana aliweka rekodi na kumbukumbu katika maisha yake pale alipomzawadia gari  Maalim Gurumo.

Diamond alimkabidhi mzee Gurumo gari hilo katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya number 1 katika ukumbi wa hoteli ya kimataifa Serena jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kumkabidhi gari hilo Diamond alisema alijiskia vibaya pale alipomsikia mzee Gurumo wakati akihojiwa redioni kuwa katika maisha yake ya muziki kwa miaka 53 hadi anastaafu,hajawahi kununua hata baiskeli.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...