Wednesday, October 23, 2013

ANGALIA JINSI UNCLE J JULIUS NYAISANGAH ALIVYOAGWA VIWANJA VYA LEADERSDR REGINALD MENGI AKIWASILI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS AKIPOKEWA NA ABUBAKAR LIONGO,TEDDY MAPUNDA NA FRED OGOT

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS
FAMILIA YA MAREHEMU JULIUS NYAISANGAH


MAKAMU WA RAIS DR BILAL AKIZUNGUMZA

MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP DR REGINALD MENGI AKIONGEA WAKATI WA KUMUAGA UNCLE J


MAKAMU WA RAIS DR BILAL,MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP DR REGINALD MENGI,MKUU WA WILAYA YA BAHI BETTY MKWASSA NA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE


MAKAMU WA RAIS AKIANDIKA KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO

MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP DR REGINALD MENGI ASINDIKIZWA KWENDA KUKAA MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS KUSHOTO KWAKE NI TEDDY MAPUNDA NA KULIA NI ABUBAKAR LIONGOMWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AKITOA SALAM ZA POLE KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI VIWANJANI HAPO

MTOTO WA MAREHEM AKIMUAGA BABA YAKE

BAADHI YA WAOMBOLEZAJI

CEO WA BLOG HII ALIKUWEPO PIAMKE WA MAREHEM AKIMBUSU MAREHEM MUMEWE HUKU MISANYA BINGI AKIMFARIJIDADA WA MAREHEM AKILIA KWA UCHUNGU

Sunday, October 20, 2013

TANZIA;MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGAH AMEFARIKI DUNIA MKOANI MOROGORO ASUBUHI HII

Mtangazaji mahiri mwenye sauti tamu ya kuvutia Julius Omang'era Nyaisangah amefariki dunia mkoani Morogoro leo asubuhi.Nyaisanga amefariki katika hospitali ya mazimbu inayomilikiwa na chuo kikuu cha Kilimo SUA,na mwili wake umehamishiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhifadhiwa.Taarifa za awali zinasema Julius Nyaisanga alizidiwa jana akiwa nyumbani kwake Kihonda Mkoani humo na kukimbizwa katika hospitali hiyo ya mazimbu kabla mauti hayajamkuta leo asubuhi.

Nyaisangah anakumbukwa kwa umahiri wake katika kufanya vipindi mbalimbali hasa sauti yake ambayo ilikuwa na mvuto wa kipekee na alianza kuvuma wakati yupo Radio Tanzania Dar es Salaam hasa kwenye vipindi vya club raha leo show,misakato na disco show na taarifa za habari kabla hajahamia ITV/Radio One akiwa ni mmoja kati ya waanzilishi wa vituo hivi ambapo aliwika katika vipindi vya sunday special,hizi nazo,habari nyepesi,nyepesi,mambo mseto na taarifa za habari kabla ya kuondoka na kuhamia Abood media group.Julius Nyaisanga alijulikana pia kwa jina la uncle J,super tall na babu wa kimanzichana ameacha mjane na watoto watatu.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Ameen,angalia baadhi ya picha akiwa katika matukio mbali mbali.
MDAU AKIMUONESHEA KIDOLE JULIUS NYAISANGA
AKIPATA CHAKULA WAKTI ALIPOKWENDA JAPAN
AKIWA KATIKA SHOPPING MALL JAPAN
JULIUS NYAISANGAH
AKIWA NA ABUBAKAR LIONGO NA MDAU MKOANI MOROGORO

Tuesday, October 15, 2013

ANGALIA PICHA ZA MH VINCENT NYERERE AKIWA HOSPITALINI INDIA KWA MATIBABU


MBUNGE WA MUSOMA MJINI MH VICENT NYERERE
MBUNGE WA MUSOMA MJINI KUOPITIA CHADEMA VINCENT NYERERE AKIWA KATIKA HOSPITALI YA APOLLO HYEDERABAD INDIA KWA MATIBABU YA MGUU

AKIWA AMEJIPUMZISHA
Mbunge wa Musoma mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh Vincent Nyerere amelazwa katika hospitali ya Apollo Hyederabad India kwa matibabu ya mguu ambao ulivunjika mara tatu mara baada ya kupata ajali maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam mwaka 2007.

Akizungumza na blog hii moja kwa moja kutoka India,Mh Vincent amaesema mara baada ya kupata ajali hiyo aliwekewa chuma ambacho baada ya muda kilianza kumletea shida kwani kilianza kusaga mifupa ya goti na nyonga.

Amesema amefanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia hasa sehemu ya paja kwa lugha ya kitaalam FEMUR

Madaktari bingwa wa hospitali hiyo wamejitahidi kuufanyia marekebisho mguu huo ambapo sasa anaendelea vizuri kwani bado anatumia dawa na hajaanza kutembea.

Mh Vincent Nyerere ni mmoja kati ya wabunge vijana machachari, wenye misimamo wanaposimamia hoja zao na mmoja kati ya wabunge vijana walioshinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliomfanya aingie bungeni kwa mara ya kwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Tumuombee kila la kheri ili arudi kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto mbali mbali za maendeleo katika nchi yetu.

MAJESHI YA SERIKALI YA DRC YAWATIMUA WAASI WA M23 KILIMANYOKA KASKAZINI MWA GOMA

  ROGER LUMBALA MMOJA WA WAJUMBE WA KUNDI LA WAASI KATIKA MAZUNGUMUZO YA KAMPALA

ASKARI WA DRC WAKIWATIMUA WAASI WA M23 KATIKA KILIMANYOKA KASKAZINI MWA GOMAVIJANA WALIYO SHIKWA KWENYE UWANJA WA MAPIGANO KUTOKA KUNDI LA WAASI WA M23 WANADAIWA KUWA NI  RAIA WA RWANDA

Monday, October 14, 2013

ANGALIA PICHA MBILI ZIKIMUONESHA UFOO SARRO AKIWA MUHIMBILI BAADA YA KUJERUHIWA KWA RISASI JANA

SAM MAHELA JOYCE KIRIA WAUGUZI NA BAADHI YA WATU WAKIMSINDIKIZA WODINI UFOO SARO

HAPA ANAONEKANA AKIUGULIA MAUMIVU,POLE SANA COMRADE

HOTUBA YA MWALIMU NYERERE KATIKA MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA

THE LEGACY OF JULIUS KAMBARAGE NYERERE

HABARI YA KUSIKITISHA: WATOTO WENYE UMRI WA MIAKA 7 NA 8 WATELEKEZWA NA WAZAZI WAO KA MIEZI MIWILI SASA BILA KUPATA MAHITAJI YA MSINGI

 Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake

 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha 


 Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

 Agustino Steven (8) akipika mchicha

 Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula 


 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe


 Unga pamoja na maharage
 Hili ndilo sanduku lao Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za msingi.

Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza  shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.

Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa  Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.

Aidha watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500  ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.

Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao  wa Mbeya yetu umebaini kuwa Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.

Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake nayeye kukimbilia kwa rafiki yake.

Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).

Na mbeya yetu
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...