Tuesday, October 15, 2013

ANGALIA PICHA ZA MH VINCENT NYERERE AKIWA HOSPITALINI INDIA KWA MATIBABU


MBUNGE WA MUSOMA MJINI MH VICENT NYERERE
MBUNGE WA MUSOMA MJINI KUOPITIA CHADEMA VINCENT NYERERE AKIWA KATIKA HOSPITALI YA APOLLO HYEDERABAD INDIA KWA MATIBABU YA MGUU

AKIWA AMEJIPUMZISHA
Mbunge wa Musoma mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh Vincent Nyerere amelazwa katika hospitali ya Apollo Hyederabad India kwa matibabu ya mguu ambao ulivunjika mara tatu mara baada ya kupata ajali maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam mwaka 2007.

Akizungumza na blog hii moja kwa moja kutoka India,Mh Vincent amaesema mara baada ya kupata ajali hiyo aliwekewa chuma ambacho baada ya muda kilianza kumletea shida kwani kilianza kusaga mifupa ya goti na nyonga.

Amesema amefanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia hasa sehemu ya paja kwa lugha ya kitaalam FEMUR

Madaktari bingwa wa hospitali hiyo wamejitahidi kuufanyia marekebisho mguu huo ambapo sasa anaendelea vizuri kwani bado anatumia dawa na hajaanza kutembea.

Mh Vincent Nyerere ni mmoja kati ya wabunge vijana machachari, wenye misimamo wanaposimamia hoja zao na mmoja kati ya wabunge vijana walioshinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliomfanya aingie bungeni kwa mara ya kwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Tumuombee kila la kheri ili arudi kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto mbali mbali za maendeleo katika nchi yetu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...