Saturday, March 30, 2013

IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA KUANGUKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 SASA IMEFIKA 20

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 katika makutano ya mitaa ya Indira Gandhi na Zanaki jijini D ar es Salaam imefikia 20.
MADAKTARI WAKIMPA HUDUMA YA KWANZA MAJERUHI WA AJALI HIYO
HARAKATI ZA UOKOAJI NA UTAFUTAJI WA MIILI YA WAKLIYOPOTEZA MAISHA ZILIVYOKUWA ZINAENDELEA

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam bwana Suleiman Kova,amesema shughuli za utafutaji wa waathiriwa zinaendelea katika eneo la tukio na utambuzi wa maiti unaendelea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kwamba hadi saa tano asubuhi ya leo maiti wanane walikuwa wametambuliwa na ndugu zao.

Amesema Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na uzembe   wa ujenzi uliosababisha ghorofa hilo kuporomoka jana asubuhi.

Amewataja wanaoshikiliwa ni pamoja na mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya ujenzi ya Lucky Constructions inayomilikiwa na diwani wa kinondoni bwana IBRAHIMU MOHAMED KISOKI.

Amesema baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuhusu jengo la pili linalojengwa na kampuni hiyo lililopo mkabala na jengo lililoporomoka huenda jengo hilo likaamriwa kubomolewa.
JENGO LILILOKUWA MKABALA NA LILILOANGUKA LINALOJENGWA NA KAMPUNI ILIYOKUWA INAJENGA JENGO LILILOANGUKA HUENDA LIKABOMOLEWA IWAPO ITABAINIKA NALO LIPO CHINI YA VIWANGO

Watu zaidi ya 60 wanahofiwa kufunikwa kwenye kifusi baada ya jengo hilo lililokuwa linaendelea kujengwa kuporomoka jana saa 2 asubuhi,wakiwemo wajenzi,wapita njia na ombaomba ambao wana mazoea ya kukaa chini ya jengo hilo

MAHAKAMA YA JUU YA KENYA IMERIDHIA USHINDI WA BWANA UHURU KENYATTA KAMA RAIS MTEULE WA NCHI HIYO

Mahakama ya juu ya Kenya kwa kauli moja imeridhia ushindi wa bwana UHURU KENYATTA kama rais mteule wa nchi hiyo kutokana na uchaguzi uliofanyika tarehe nne ya mwezi huu. 
RAIS MTEULE WA KENYA BWANA UHURU KENYATTA NA MGOMBEA MWENZA BW RUTTO

Likitangaza uamuzi wake,jopo la majaji sita likiongozwa na jaji mkuu bwana WILLY MTUNGA,lilitupilia mbali pingamizi tatu zilizodai kuwa matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa na dosari.

Majaji hao wanasema hoja zilizotolewa na walalamikaji akiwemo waziri mkuu bwana RAILA ODINGA,hazikuwa na uzito wa kutosheleza kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo ambao Jaji mkuu MTUNGA amesema uliendeshwa kwa uhuru na haki.

Katika uchaguzi huo bwana KENYATTA alipata asilimia 50.07 ya kura wakati mpinzani wake mkuu bwana RAILA ODINGA alipata asilimia 43.25 ya kura

Friday, March 29, 2013

JENGO LA GHOROFA 16 LAANGUKA MTAA WA ZANAKI NA INDIRA GHANDI DAR LEO ASUBUHI

JENGO LA GHOROFA14 LIKIWA LIMEANGUKA LOTE
WAOKOAJI WAKITAFAKARI NAMNA YA KUFANYA KUOKOA WATU WALIOFUNIKWA NA KIFUSI

HARAKATI ZA UOKOAJI ZIKIENDELEA

PILIKAPILIKA ZA UOKOAJI ZIKIENDELEA
WAKAZI HAWA WA ENEO KARIBU NA JENGO LILILOANGUKA WAKIJITAHIDI KUITA WAOKOAJI WANAHISI ENEO HILOKUNA MTU
WAKAZI WA ENEO HILO WAKIJITAHIDI KUFUKUA KIFUSI ILI KUTAFUTA WATU WANAOHOFIWA KUFUNIKWA NA KIFUSI HICHO
JENGO HILI LIPO KARIBU KABISA NA JENGO LILILOANGUKA NALO LINA GHOROFA 14 NA INASEMEKANA LINAMILIKIWA NA MTU MMOJA NA JENGO LILILOANGUKA
UMATI WA WATU UKISHUHUDIA HALI HALISI ENEO LA TUKIO

GARI LILILOKUWA KARIBU NA JENGO LILILOANGUKA LIKIWA LIMEHARIBIWA VIBAYA NA KIFUSI .(PICHA ZOTE KWA HISANI YA SUFIANIMAFOTO.COM)

RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI MZEE NELSON MANDELA AMELAZWA TENA HOSPITALI BAADA YA KUSUMBULIWA TENA NA UGONJWA WA MAPAFU

MZEE NELSON MANDELA

MBUNGE WA CHAMBANI-CUF MH SALUM HEMED KHAMIS AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Chambani kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF,Mh Salum Hemed Khamis amefariki dunia katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa na kuanguka ghafla akiwa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es Salaam
Marehemu Salum Hemed Khamis

Tuesday, March 26, 2013

ZIARA YA RAIS XI JINPING WA CHINA NCHINI TANZANIA

Rais wa China Xi Jinping akihutubia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Kikwete na Xi Jinping wakiwapungia wananchi
Rais wa China Xi Jinping na rais Kikwete
Rais Xi Jinping na Rais Kikwete wakiwa na wake zao
Wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya rais Xi Jinping wa China

Saturday, March 16, 2013

HAFLA FUPI YA KUWAAGA SEVERINE KIWANGO NA JOHN LUGENDO AMBAO WAMESTAAFU ITV/RADIO ONE

MKURUGENZI MTENDAJI WA ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE AKISEMA JAMBO KABLA YA KUMPATIA ZAWADI YA KUMBUKUMBU ALIYEKUWA MTAYARISHAJI NA MUONGOZAJI WA VIPINDI SEVERINE KIWANGO AMBAYE AMESTAAFU.

SEVERINE KIWANGO AKIPONGEZWA NA MKURUGENZI MTENDAJI ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE

AKIPOKEA ZAWADI YAKE

HAPA AKIIFUNGUA WATU WAIONE,ALIYEKAA NI JOHN LUGENDO AMBAYE PIA AMESTAAFU NA MACHARIA KOIGI PEMBENI YAKE AMBAYE NI MKURUGENZI WA ITV

IKAFIKA ZAMU YA JOHN STEPHEN LUGENDO AMBAE ALIKUWA MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI ITV/RADIO/RADIO ONE

JOHN LUGENDO AKIPOKEA ZAWADI YAKE PIA KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE

MZEE KIWANGO AKIONYESHA ZAWADI YAKE YA KUMBUKUMBU

JOHN LUGENDO NAE AKIWA BUZY KUIFUNGUA YAKE HUKU KIWANGO AKIMSHANGAA

HATIMAE NAE AKAINYOOSHA JUU WATU WAIONE

AFISA UTAWALA WA ITV/RADIO ONE HELLEN ELIPOKEA ALIHAKIKISHA KILA KITU KINAENDA SAWA HAPA MAULID KAMBAYA ILIBIDI AKAE KARIBU NAE ILI HUO MZIGO UKIISHA AFANYE TAKE TWO

BAADA YA YOOTE UKAFIKA WAKATI HUU MUHIMU KWENYE SHEREHE YEYOTE ILE.

WAFANYAKAZI WA ITV/RADIO ONE WAKIFANYA YAO

BLANDINA SEMBU AKISUBIRI ZAMU YAKE YA KUPATA ANACHOPATA DJ DWHITE MWENYE TSHIRT NYEKUNDU AKIFANYA YAKE

ASILIMIA 28 YA WANAFUNZI WA KIKE AFRICA KUSINI WANA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI


Takribani asilimia 28 ya wanafunzi wa kike nchini Afrika Kusini wanaishi na virusi vya UKIMWI idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na asilimia 4 ya wanafunzi wa kiume wanaoishi na virusi hivyo. Waziri wa afya wa nchi hiyo Aaron Motsoaledi amesema wasichana wengi wamekuwa wakiambukizwa kutokana na kushiriki ngono na wanaume wenye umri mkubwa.
Waziri wa afya wa Afrika kusini Aaron Motsoaledi

Akitoa takwimu hizo Motsoaledi amesema wanafunzi wa kike wapatao 94,000 nchini humo wamepata ujauzito katika kipindi cha mwaka 2011, baadhi yao wakiwa katika umri wa miaka kumi.

Motsoaledi ametoa wito kwa watoto wote wa kike kutojihusisha kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa na kujiepusha na ngono ili kupunguza na kasi ya maambukizi ya UKIMWI miongoni mwao.

Taifa hilo lina jumla ya watu milioni 50, na takwimu za wizara ya afya zinaonyesha watu milioni 6 nchini humo wanaishi na virusi vya UKIMWI.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye maambukizi makubwa ya UKIMWI duniani, hata hivyo idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo imekuwa ikipungua siku hadi siku.

Hivi karibuni idara ya afya nchini humo imeanzisha jitihada za kukabiliana na maambukizi ya VVU kwa watoto wa shule. Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na upimaji wa afya kwa hiari na ugawaji wa mipira ya kufanyia mapenzi condom

TOP FLAVOUR KUANZA ZIARA YA KUSAKA VIPAJI MIKOANI



Kundi la muziki wa kizazi kipya lenye maskani yake kigamboni jijini Dar es Salaam limeanza mchakato kwa kusaka vipaji nje ya jiji la maraha Dar es salaam, akizungumza na  Mwaipaya blog mkurugenzi 
wa kundi hilo ambaye pia ndiye mlezi shaaban Ramadhani maarufu kama Sheby alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwakuwa wasanii wengi wa bongo wanafursa kubwa ya kufanya kazi ukilinganisha na wasanii wa mikoani.
Akifunguka zaidi mkurugenzi wa kundi hilo amesema kuwa wasanii watakaopatikana watakuja jijini na kurekodi ngoma moja ambayo itafanyiwa video na kufanyiwa promo na baada ya hapo ngoma hiyo itakuwa ni ya msanii mwenyewe na atakuwa na uhuru nayo.Ziara ya kundi hilo ilianza jana huko mikindani Tanga,leo wapo Lindi na Kesho Mtwara kabla ya kugeuza jijini.

Akizungumzia juu ya kuondoka kwa msanii aliekuwa katika kundi hilo pamoja  produza aliekuwa anakuja kwa kasi sheby alishangaza kidogo baada ya kusema kuwa yeye hamfahamu MAN NGINJA  ambaye alikuwepo ndani ya kundi hilo kwa kudai kuwa aliletwa pale na msanii mwenzake ambaye ni Tony Touch…..’’ huyu jamaa mimi simfahamu ila alikuja hapa na akashiriki katika wimbo wa kundi ambao tuilikopi kwa P square wa beautiful onyinye na alifanya chorus lakini simjui’
Alipoulizwa zaidi vipi kwa upande wa producer wa shebiz records ambaye nae ameondoka muda mfupi tu baada ya kuondoka kwa Man nginja Shebiy alisema kuwa producer huyo alikuwa na mkataba wa kufanya ngoma mbili yaani ngoma moja ya kundi na ngoma moja ya msaniii Tony Touch ya your the one and only aliyomshirikisha mwanadada MEG

Blog hii ililazimika kumtafuta producer Chid Bay ilikuzungumzia hili lakini simu yake ilikuwa haipatikani muda wote ila taarifa ambazo tumezipata ni kwamba kwa sasa mtayarishaji huyo wa mapigo ya muziki anafanya mazoezi ya kuimba na kundi la dansi nchini kundi la Akudo Impact.

Kwa upande wa Man Nginja alipotafutwa yeye  alisema kuwa  anamuachia Mungu na kwamba hata kama kusoma hujui  bac picha unaweza ukaielewa kama ni ya kike au ya kiume na alipotakiwa kuelezea zaidi alisema ipo siku atafunguka ila kwa sasa yupo buzy akiandaa ngoma zake ambapo ameshaachia ngoma moja inayokwenda kwa jina kla kizai Zai alioifanya nje ya kundi la Top fleva.
Mkurugenzi wa kundi la TOP FLAVOUR la kigamboni Shaaban Ramadhan aka SHEBBY

SHEBBY AKICHART

Wasanii wa Top flavour TISTA mwenye rasta Mrs Shebby kati kati na Momba producer wa asahebby's Recordz

Maulid Kambaya akiwa na wasanii wa Top Flavour Tista  na Momba

Maulid Kambaya akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Shebby's Recordz Shaaban Ramadhan kati kati ni Mrs Shebby

Kambaya akiwa na kundi la TOP FLAVOUR mara baada ya Interview

Maulid Kambaya akiwa katika pozi kijiji beach kigamboni mara baada ya kufanya mahojiano na TOP FLAVOUR

Kundi la Top Fleva linaundwa na wasanii wa tatu ambao ni Tony Touch msemaji wa kundi first lady Tista na Momba amabye kwasasa ameshikilia mikoba ya uandaaji wa muziki wa kundi hilo chini ya studio inayomilikiwa na kundi hilo ya Shebiz recods

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...