Sunday, May 26, 2013

VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI BUNDA MKOANI MARA



MATUKIO KAMA  HAYA YAMEZIDI KUFUMMBIWA MACHO NA YANAZIDI KUTOKEA KAMA WALIVYOUAWA KIKATILI  VIKONGWE WATATU HUKO BUNDA MKOANI MARA
WANAWAKE watatu wameuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na wananchi wanaojiita wenye hasira na kisha miili yao kuteketezwa kwa moto, wilayani Bunda mkoani Mara.
Kamanda wa Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi, Absalom Mwakyoma alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika vijiji vya Nyamitwebi na Kasahunga, wilayani hapa.
Aliwataja watu waliouawa kuwa ni Tibezuka Biseko au Bibi Rai (51), mkazi wa Kijiji cha Nyamitwebili, Chausiku Rubisha (73) na Mugara Manyama (75) wakazi wa Kijiji cha Kasahunga.
Alisema wanawake hao waliuawa na wananchi waliopiga yowe wakiwatuhumu kuwa ni wachawi, huku wakidai kuwa walimchukua kichawi ndugu yao mmoja aliyefariki dunia hivi karibuni katika ajali ya gari baada ya kugongwa akiwa anaendesha pikipiki.
Aidha, alisema kuwa pia wananchi hao waliziteketeza kwa moto nyumba tano za wanawake hao pamoja na nyumba nyingine za wanawake wengine ambao walinusurika kuuawa baada ya kupata taarifa na kutoroka.
“Wanawake watatu wameuawa katika tukio hilo na nyumba zao zimeteketezwa kwa moto… na hili tukio linahusishwa na imani za ushirikina, baada ya kuambiwa na waganga wa jadi.
“Hawa waganga feki wanawatia hasira wananchi kwa mambo ya kijinga kiasi hiki, hatuwezi watu kuwa tunauawa kinyama, maana hawa wazee walitakiwa waishi kama watu wengine,” alisema.
Akifafanua juu ya tukio hilo, Kamanda Mwakyoma alisema kuwa hivi karibuni mwanaume mmoja aitwaye Phales Wegero, aligongwa na gari wakati akiendesha pikipiki hali iliyosababisha wananchi wenye hasira kuiteketeza kwa moto gari hiyo.
Alisema baada ya mwanaume huyo kugongwa, ndugu zao walipiga ramli kwa waganga wa jadi na kuambiwa kuwa amechukuliwa kichawi, na kwamba wachawi hao wamekuwa wakimtembeza usiku kijijini hapo.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa hali hiyo iliwafanya wananchi hao kujikusanya baada ya kupiga yowe na kuwavamia wanawake hao kwa nyakati na maeneo tofauti na kuwashambulia hadi kuwaua.
Aliongeza kuwa pia wauaji hao wameviteketeza kwa moto vitu vyote vya watu hao, zikiwemo thamani za ndani.
Alisema kuwa kuhusiana na tukio hilo la jana, wanawashikilia watu kadhaa kwa mahojiano zaidi na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwasaka wengine wanaodaiwa kutoroka.
Kutokana na tukio hilo, baadhi ya wananchi wameyakimbia makazi yao na kukimbilia milimani wakiogopa kukamatwa na polisi.

Friday, May 24, 2013

RAMADHAN SULEIMAN(RAMA MLA WATU) NA MAMA YAKE WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

MAMA YAKE RAMA

RAMA AKIWA MAHAKAMANI
PICHA YA RAMA NA MAMA YAKE 2008


PICHA ZOTE KWA HISANI YA GPL
KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto SaloMahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. 

Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. 

Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani

BAADA YA NGASSA NIYONZIMA ASAINI TENA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI YANGA

HARUNA NIYONZIMA aka FABRIGAS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI BAADA YA KUSAINI TENA MKATABA WA MIAKA MIWILI WA KUITUMIKIA TENA CLAB YA YANGA(Picha kwa hisani ya GPL)
Hatimae kiungo wa kimataifa kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima amefikia makubaliano mapya na timu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa  kuitumikia tena timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa twiga pale Jangwani.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa clab ya simba ilikuwa inamuwania kiungo huyo mwenye chenga na pasi zenye uhakika na zisizomithirika na ilikuwa imemtengea kiasi cha shillingi miliono 70.
Pia tetezi zingine zilivuma kuwa Azam FC nao walimtengea donge nono ili asaini kuichezea timu hiyo.
Kabla ya kusaini mkataba huo leo saa tano asubuhi Niyonzima alishaamua kuondoka kurejea kwao nchini Rwanda kama wangekuwa hawajakubaliana na clabu yake aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa msimu uliopita.
Hata hivyo Yanga imemtimizia kila alichokitaka mchezaji huyo hatimae amesaini mkataba huo wa miaka  miwili.
Niyonzima amekuwa mchezaji wa pili kusaini katika club hiyo ikiqwa ni siku chache tu zimepita tangu Mrisho Ngassa nae kusaini mkataba mpya na timu hiyo akitokea Simba.

Thursday, May 23, 2013

HII NI HALI YA KAWAIDA KATIKA JIJI LA DAR,KILA KUKICHA MAGARI HAYAISHI KUGONGANA,ANGALIA MAGARI HAYA YALIYOGONGANA KARIBU NA KITUO CHA BASI CHA ITV

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARA BARANI AKIWASIKILIZA MADEREVA WA MAGARI YALIYOGONGANA KARIBU KABISA NA KITUO CHA MABASI CHA ITV
GARI DOGO LENYE NAMBARI ZA USAJILI T375 BUR LIKIWA LIMEHARIBIKASEHEMU YA TAA YA KULIA BAADA YA KULIGONGA GARI LA CHUO CHA ARDHI


GARI LA CHUO CHA ARDHI LENYE NAMBARI SU 39382 LIKIWA MBELE YA GARI DOGO AMBALO LILIIGONGA GARI HIYO KWA NYUMA

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA AKICHUKUA MAELEZO KUTOKA KWA MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI

Wednesday, May 22, 2013

MTOTO WA CHINI YA MIAKA MITANO AFUNGIWA NDANI NA BABA MZAZI NA MAMA WA KAMBO KWA KARIBU MIAKA MIWILI IYUNGA MKOANI MBEYA

Mtoto Joshua akiwa anashangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana
Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

Mtoto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha
Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu
Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni
Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo

Akimbeba kuelekea kituo cha afya
Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua
Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema  yeye huwa analala na joshua chumbani kwake
Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo
Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo
Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo
Mama wa mlezi wa Joshua akiingia numbani kwake na kutushangaa tumekuja fuatanini kwake
Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza (HABARI/PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU)




Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika  mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
 Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora  pamoja na huduma nyingine.
.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye  Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
 Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
  
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa  wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya  Inyala Kata ya Iyunga  jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo  wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo

Tuesday, May 21, 2013

WATANZANIA WALAMBA NONDO CLARK UNIVERSITY USA

Bi Dainess Mgidange baada ya kulamba nondo yake ya shahada ya juu ya Enviromental Scince and policy kutoka Clark University,MA USA

bibi maendeleo ya Jamii Namtumbo Rahiya nasser baada ya kulamba nondo yake ya Shahada ya juu Intenational developement and Social change kutoka  Clark Unversity ,MA  USA .

NZERA KITANO NDIYE REDDS MISS KIBAHA 2013

 
Katikati  Redds Miss Kibaha Nzera Kitano , kushoto mshindi wa pili Ester Albert na kulia ni Rachel Joh ambaye ni mshindi wa tatu.




MISS KIBAHA 2013 NZERA KITANO

Na Mwandishi wetu

ALIYEKUWA mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera  Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer  Kibaha Maili Moja mkoani Pwani.

Nzera ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.

Aidha kwa ushindi huo  Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.

Mshindi wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.

Mshindi wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.

Kwa ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania  tiketi ya shindano la taifa.
Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia kinywaji cha Dododma Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Media Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr Studio, ASET ,Santorine Holiday Resort na Amazon Night Club.

Bendi ya Muziki wa dansi ya Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.Washiriki wengine waliobaki walipata kifutajasho cha .sh.100,000 kila mmoja


Monday, May 20, 2013

MBUNGE WA IRINGA MJINI PETER MSIGWA NA WATUHUMIWA 75 WAFIKISHWA MAHAKAMANI MCHANA HUU

MH PETER MSIGWA AKISHUSHWA KWENYE GARI LA POLISI

MH PETER MSIGWA AKIWA KWENYE ULINZI MKALI
Mbunge wa Iringa mjini mh Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine 75 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya mkoani IRINGA na kusomewa mashtaka matatu yanayowakabili

Saturday, May 18, 2013

PILAU LA UBINGWA BILA NYAMA HALINOGI,HIVI NDIVYO MNYAMA ALIVYOCHINJWA UWANJA WA TAIFA

YANGA WAKIFURAHIA KIKOMBE CHA UBINGWA NA KUMCHINJA MNYAMA




JUMA KASSIM NATURE AKIFANYA VITU VYAKE





GOLI LA YANGA

MRISHO NGASSA AKIBEBWA JUU JUU NDANI YA JEZI YA YANGA



REFA WA MTANANGE HUO AKIWA AMEUMIA

REFA AKIPATA HUDUMA YA KWANZA

MAKOCHA WA YANGA WAKICHORA RAMANI YA KOMBORA MBILI

WACHEZAJI WAKITINGA UWANJANI KWA AJILI YA KUANZA MTANANGE


KOCHA WA SIMBA(picha zote na Shafii Dauda)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...