Saturday, September 21, 2013

SHUHUDIA BAADHI YA PICHA ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA NAIROBI LEO


eneo la maduka lilipotokea shambulio hilo

mmoja kati ya watu waliouawa ndani ya gari

hali inaonekana kuwa tete

baada ya tukio

baadhi ya watu waliouawa wanaonekana wamelala


tafrani nje ya jengo


madaktari wakitoa huduma ya kwanza
Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
 
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.Inaarifiwa watu watano wamekufa.
 
Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
 
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.
 
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.
 
Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika.

ANGALIA PICHA YA HAKIMU AKIWA AMELOA DAMU BAADA YA KUCHOMWA KISU MAHAKAMI--SHINYANGA

Hakimu wa mahakama ya mwanzo mkoani Shinyanga achomwa kisu na mlalamikaji baadaya ya kutoa hukumu kwa mtuhumiwa,hakimu huyo alitoa hukumu kwa mtuhumiwa wa wizi wa baiskeli yenye thamani ya 150000 aina ya neria.CHANZO : MATUKIO NA MICHAPO BLOG

Wednesday, September 18, 2013

MAALIM SEIF AREJEA KUTOKA INDIA KUCHUNGUZA AFYA YAKE

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis pamoja na viongozi wengine, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Masoud (kulia), alionesha uso wa bashasha baada ya kuwasili nchini akitokea India. (picha na Salmin Said, OMKR  
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amewasili nchini akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
 
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Maalim Seif alipokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis.
 
Aidha mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama Cha Wananchi CUF, yaliambatana na shamra shamra mbali mbali za burudani.
 
Maalim Seif aliondoka nchini tarehe 24 mwezi uliopita kuelekea India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake, utaratibu ambao umekuwa ukifanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.

JELA MIAKA 2 KWA MAUAJI YA BILA KUKUSUDIA

 Steven Augustino wa Demashonews, Tunduru
 
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma kupitia Vikao vinavyo
endelea Wilayani Tunduru Imemuhukumu Kifungo cha Miaka Miwili Jela
Manywele Abdalah Ausi (35) baada ya kutia hatianai katika kosa dogo la
kuua bila kukusudia kinyume cha sheria kifungu namba 195 sura ya 16
cha kanuni ya adhabu kama ilivyo fanyiwa makebisho mwaka 2002.

Manyele aliye kuwa anakabiliwa na Shauri la mauaji  ya kukusudia Namba
Rm 16/2012 alidaiwa kuwa alimuua marehemu bakari Mohamed Komando
katika tukio la ugomvi wa kugombea deni la shilingi 2000 lilitokea
Januari 8 /2012 katika kijiji cha Chikomo mashambani  Wilayani humo.

Alisema baaya ya kusomewa Shitaka hilo ambao mtuhumiwa Manywele
akikanusha ,Wakili wa utetezi Dickson Pius Ndunguru aliiomba mahakama
mteja wake kuwa yuko tayari kukili kosa dogo la kuuwa bila kukusudia
ombi ambalo halikupigwa na upande wa mashtaka na ndipo mahakama baada
ya kusomiwa kosa hilo ilipo mtia hatihani kwa kosa dogo la kuuwa bila
kukusudia.

Akifafanua hukumo hiyo Jaji anayesikiliza Kesi hizo Njingafibili
Mwaikugile alisema kuwa adhabu hiyo Pamoja na mambo mengine mahakama
hiyo imezingatia hoja za wakili wa utetezi Dickson Ndunguru aliyeiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu ndogo kwa mteja wake kwavile ni mkosaji wa
mara ya kwanza hivyo alijikuta akipingana na sheria kwa bahati mbaya,
amekaa mahabusu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi tisa hali ambayo
inaonesha kuwa tayali amekwisha jutia na kujifunza kuwa vitendo vya
kufanya makosa havilipi.

Sababu nyingine iliyotolewa na Jaji Mwikugine katika utoaji wa adhabu
hiyo ni pamoja na kuzingatia hoja za utetezi kuwa kitendo cha
mtuhumiwa huyo kukubali kufanya kosa hilo la kuua bila kukusudia pia
kimeonesha uungwana wake hali ambayo inaonesha kuwa amejutia kosa
alilo lifanya na ameipunguzia mahakama muda na gharama za uendeshaji
wa kesi hiyo.

Jaji Mwaikugile aliendelea kuleza kuwa kutokana na hali hiyo pia
pamoja na kuzingatia adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia usalama ya
Mtuhumiwa na jamii Kijiji kwake Mahakama hiyo imechukua mamuzi hayo
Awali akitoa hoja Mahakamani hapo kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo
Mwanasheria wa a Serikali Hamimu Nkoleye pamoja na mtuhumiwa huyo
kukiri kufanya kosa hilo dogo la kuua bila kukusudia aliiomba Mahakama
hiyo kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa
wakichukua sheria mkononi na kusababisha matukio ya mauaji kuongezeka
Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na taifa kwa ujumla.

Upande wa mjibu hoja uliowakilishwa na Wakili wa kujitegemea Dickson
Ndunguru aliiomba Mahakama hiyo kumpatia mteja wake adhabu yenye
unafuu na ikiwezekana afungwe kifungo cha nje.

Awali akimsomea Shitaka hilo ambalo mtuhumiwa huyo alikiri kulifanya
kwa maelekezo kuwa hakuwa anajitambua, Mwanasheria wa Serikali Hamimu
Nkoleye alidai mbele ya Jaji huyo kuwa Manyele ambaye alikuwa
akishuhudiwa na Mkewe Asha Mohamed Selemani alipiga na kumkalia chini
marehemu hadi walipofika wasamalia wema kuamulia ugomvi huo zikiwa ni
juhudi za shuhuda huyo kupiga kelele za kuomba msaada huo.

Nkoleye aliendela kufafanua kuwa Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mkazi
wa Kijiji cha Chikomo Wilayani humo alifanya kosa hilo wakati marehemu
akiwa katika mashamba yaliyopo Kijijini hapo ambapo alienda
kumtembelea kwa nia ya kudai deni hilo ambalo tayari akuwa amekwisha
jibiwa kuwa hatalipwa.

RAIS KIKWETE AMTEUA BI JACQUELINE MALEKO MKURUGENZI MKUU TANTRADE

Bi.Jacqueline Maleko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi.Jacqueline Mneney Maleko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue,uteuzi huo ulianzia September 10,mwaka huu,2013.

Kabla ya uteuzi huu,Bi.Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Masoko, Wizara ya viwandana Biashara,kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa (TANTRADE).


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
DAR ES SALAAM.

18 SEPTEMBA, 2013

Tuesday, September 17, 2013

SIMBA AUA MFANYAKAZI WA HIFADHI

SIMBA ANAEJULIKANA KWA JINA LA KENENISA BAADA YA KUMUUA ABERA MFANYAKAZI WA HIFADHI
Simba amemuua Abera Silsay (51),katika sehemu ya kutunzia wanyama pori ambao wanafugwa katika sehemu hiyo kwa ajili ya utalii huko Addis Ababa,Ethiopia.

Taarifa zinasema simba huyo alimvamia Abera baada ya kusahau kuufunga mlango wa sehemu simba huyo anapolala.

Abera aliuawa na simba huyo anaejulikana kwa jina la Kenenisa wakati akisafisha banda namba 10 analolala simba huyo kutokana na kusahau kuufunga mlango ndipo simba huyo alipotoka kumvamia na akamuangusha chini huku akimng'ata sehemu yake ya shingoni.

Mkurugenzi mkuu wa hifadhi hiyo bw Musie Kiflom amesema walinzi wa hifadhi hiyo walijaribu kupiga risasi hewani ili kumtisha simba huyo lakini jitihada zao ziligonga mwamba.

Taarifa zinasema hii ni mara ya pili kwa simba kuua muhudumu wa hifadhi kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 17 iliyopita katika hifadhi hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema wameamua kuchuklua hatua ya kuzidi kuwapa elimu wafanyakazi hao wa hifadhi namna ya kuwalinda wanyama,kuishi nao, kuwahudumia kwa kuwapa chakula na kuwasafisha.

Monday, September 16, 2013

POLISI YAUA JAMBAZI DAR BAADA YA KUPORA FEDHA KATIKA DUKA VINGUNGUTI,TAHADHARI NA TUNAOMBA RADHI BAADHI YA PICHA ZINATISHA

MTU ANAEDHANIWA NI JAMBAZI BAADA YA KUUAWA NA POLISI LEO ENEO LA SUKITA JIJINI DAR

KIKOSI CHA DEFENDER CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKOSI CHA POLISI MAGOMENI

WAZEE WA KAZI MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA

MOJA KATI YA WATU WANAODAIWA KUPORA FEDHA VINGUNGUTI BAADA YA KUUAWA NA POLISI
Jeshi la polisi kikosi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumuua mmoja kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mara baada ya kurushiana risasi na polisi eneo la SUKITA jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo saa tano asubuhi maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la tukio.

Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao, alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea kusikojulikana

Saturday, September 14, 2013

RONALDO AMPOKEA BALE KWA KUMUUMIZA MAZOEZINI,JE NI MAKUSUDI KUTOKANA NA BALE KUMPIKU UTHAMANI AU BAHATI MBAYA TUU

1
Wachezaji wawili wenye historia ya kuweka rekodi ya kuwa wachezaji ghali kuliko wote hii leo wamekutana kwa mara ya kwanza kabla ya mazoezi ya timu yao .
Gareth Bale na Cristiano Ronaldo walikutana kwa mara ya kwanza tangu wakati Bale aliposajiliwa na Real Madrid toka klabu ya Tottenham Hotspurs .
Bale amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo baada ya usajili wake kwenda Real Madrid kuigharimu klabu hiyo ya Hispania paundi milioni 86 akiwa ameuzidi usajili wa Ronaldo kwa paundi mdilioni 6
.
2
Ronaldo na Bale dakika chache baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.
Bale na Ronaldo walikutana hii leo mapema dakika chache kabla ya kuanza kwa mazoezi ya Real Madrid wakiwa wamejiunga na klabu hiyo baada ya kuziacha kambi za timu zao za taifa .
Bale alicheza kwenye mechi mbili za Wales ikiwemo mechi dhidi ya Macedonia iliyochezwa jana huku Ronaldo akicheza na kuifungia Ureno kwenye mchezo dhidi ya Ireland Ya Kaskazini na aliukosa mchezo wa jana kati ya Ureno na Brazil.  


SIKU YA TATU MAZOEZINI MAMBO YAKAWA HIVI..
Katika siku ya tatu tu ya mazoezi yake kamili klabu hiyo mpya, Bale tangu ajiunge nayo kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 86, alijikuta akipitiwa kwanja na nyota huyo wa zamani wa Manchester United ambaye bila shaka alitaka kumuonyesha 'mchawi huyo wa Wales' kwamba si kazi rahisi kuwa mkali Real.
Pia Pepe alionekana kuchekelea wakati akiangalia Mreno mwenzake, Ronaldo akimtenda kitu Bale kwa kumrukia kwenye kifundo cha mguu.

That's just for starters: Cristiano Ronaldo looks up at Gareth Bale after making a sliding challenge
Cheki kitu hicho: Cristiano Ronaldo akimpitia miguuni Gareth Bale
Incoming: Ronaldo decides to launch into a slide tackle on Bale
Anamfuata: Ronaldo akimrukia Bale
Locked on: Ronaldo's boot is studs up but grounded as he homes in on Bale
Mguu umefika: Ronaldo akipeleka mguu wake kupitia mpira miguuni mwa Bale
Direct hit: Bale feels the full force as Ronaldo slides through his ankle
Maumivu: Bale akipewa kitu na Ronaldo 
Bale alionekana kuwa sawa tu baada ya kitendo hicho, lakini hakuonekana kuwa mwenye furaha baada ya hapo.
Ronaldo alikuwa anashikilia rekodi ya mchezaji ghali wa dunia wa awali kwa Pauni 80 alizonunuliwa kutoka Manchester United mwaka 2009 na kwa picha hizi inaweza kuchukuliwa kama ni wivu wake kwa mchezaji mwenzake mpya Bernabeu.

RAISI WA ZANZIBAR ALLY MOHAMMED SHEIN AFIKA HOSPITALI KWENDA KUMUONA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padre wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Mwang'amba, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, Mjini Unguja, baada ya kumwagiwa tindikali Mjini Magharibi - Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Padre Joseph  Mwang'amba alipokuwa akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kumwagiwa tindikali jana.
Mmoja wa Ndugu wa Padre aliyemwagiwa tindikali akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, hisia zake kwa uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa tindikali Padre na kuomba hatua zilichukuliwe ili kukomesha vitendo kama hivi ambavyo vimeanza kuzoeleka

HIVI NDIVYO FATHER KIDEVU MROKI MROKI ALIVYOANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

Moja ya vitu muhimu sana nilivyo vifanya leo katika sehemu ya likizo yangu ni kumtembelea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nyumbani kwake Dodoma na kisha kwenda hadi shambani kwake kijiji cha Zuzu ambako alinifahamisha vitu kadhaa juu ya kilimo hasa Ufugaji nyuki na kilimo cha migomba. Hakika nimejifunza mengi ambayo nitayatumia vyema Kijijini kwangu Kinyenze pale Mvomero Morogoro. PM amesema wazi kuwa kujitoa ni jambo muhimu sana hasa kwa sisi vijana hasa kama tunania ya kilimo.

MECHI YA YANGA NA MBEYA CITY YAGUBIKWA NA VITUKO KIBAO,GARI LA YANGA LAVUNJWA KIOO NA MAYAI MATATU YAKUTWA KATI KATI YA UWANJA


KIOO CHA BASI LA YANGA KILICHOVUNJWA NA MASHABIKI HUKO MBEYA LEO

BASI LA YANGA LIKIWASILI KATIKA UWANJA WA SOKOINE MJINI MBEYA

MSEMAJI WA TIMU YA YANGA BARAKA KIZUGUTO AKIZUNGUMZA NA WAHABARI UWANJANI HAPO


KOCHA WA TIMU YA YANGA ERNIE BRANDTS KWA MBAALI ANAONEKANA AKISHUKA KWENYE BASI TAYARI KWA MPAMBANO

MAYAI MATATU YALIYOFUKULIWA UWANJANI YAKIWA YAMEANDIKWA QURAAN,KATIKA MTANANGE WA YANGA NA MBEYA CITY,KAMISHNA WA MECHI HIYO ALIYAKUTA KATI KATI YA UWANJA NA HAIKUFAHAMIKA MARA MOJA NI NANI HASA ALIYAWEKA MAYAI HAYO

MAYAI YALIYOKUTWA KATI KATI YA UWANJA (PICHA NA MAULID KAMBAYA)


Friday, September 13, 2013

TAZAMA PICHA ZAIDI ZA BINTI ALIYEKUFA KWA KUKOSA HEWA WAKATI AKIPIKA CHAPATATI MWANANYAMALA KISIWANI JIJINI DAR ES SALAAM

MAJIRANI WAKIELEZEA

MASHUHUDA






PICHA INAMUONYESHA ASHA AKIWA AMEFARIKI DUNIA NA PEMBENI NI CHAPATI ALIZOKUWA ANAPIKA


SEHEMU YA BIASHARA ALIOKUWA ANAFANYIA ASHA


MWILI WA ASHA


MAMA MWENYE NYUMBA AKIONGEA NA WANAHABARI





MWILI WA ASHA BAADA YA KUFUNIKWA





MWILI WA ASHA UKIPAKIWA KWENYE GARI

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...