Saturday, July 19, 2014

BARAZA LA USALAMA LAKUTANA KUHUSU UKRAINE KUFUATIA AJALI YA NDEGE


BARAZA LA USALAMA WAKATI WA DAKIKA MOJA YA UKIMYA KUWAKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA YAO KWENYE AJALI YA NDEGE

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali nchini Ukraine, kufuatia ajali ya ndege ya Malaysia hapo jana mashariki mwa Ukraine, kwenye eneo linalodhibitiwa na waasi. Taarifa kamili na Amina Hassan
(Taarifa ya Amina)
Mwanzoni mwa mkutano wa leo, Rais wa Baraza la Usalama, Richard Gasana, amewasilisha ujumbe wa rambirambi za wanachama wake kwa familia za wahanga wa ajali hiyo, na serikali za nchi zilizopoteza raia wao
GASANA
"Naomba nyote msimame na kubaki kimya kwa dakika moja, kuwakumbuka waliopoteza maisha yao"
Akizungumza kwenye mkutano huo, Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman wakati hali inaendelea kuzorota kwa kasi nchini Ukraine, inasikitisha kuwa mwanga wa matumaini ulioonekana baada ya kutangazwa mpango wa Rais Poroshenko wa amani, ukiwemo usitishaji mapigano, sasa umedidimia haraka. Kuhusu baa la ndege ya Malaysia, ambalo chanzo chake bado hakijathibitishwa, Bwana Feltman amesema
"Katibu Mkuu amesikitishwa na ripoti zinazoonekana kuwa za kuaminika kuwa kombora la kurushwa angani lilitumiwa. Katibu Mkuu analaani vikali hiki kinachoshukiwa kuwa utunguaji wa kukusudia wa ndege ya kiraia. Tukio hili la kutia hofu ni ukumbusho wa jinsi hali mashariki mwa Ukraine ilivyo mbaya mno, na jinsi inavyoathiri nchi na familia nje ya mipaka ya Ukraine."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...