Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dhalura katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Philip Mukasa, amesema kuwa ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Sudani ya Kusini.
Rubani wa ndege hiyo aliamua kutua katikati ya barabara baada ya kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha, ambapo aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe na kuamua kutua kwa dharura kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.
Katika dharura hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa, na watu wote wametoka salama.
Haikuweza kufahamika kwa haraka sababu zilizomfanya rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
No comments:
Post a Comment