Friday, October 24, 2014

WANANCHI WA MKOA WA KILIMANJARO WAONDOLEWA HOFU YA KUWEPO MGONJWA WA EBOLA MKOANI HUMO

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
Uongozi wa mkoa wa kilimanjaro umewaondoa hofu wananchi wake juu ya ugonjwa hatari wa Ebola kutokana na kuwepo mgonjwa anayehudumiwa katika zahanati ya Shirimatunda katika manispaa ya Moshi aliyedhaniwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mkuu wa mkoa huo bwana Leonidas Gama amewataka wananchi hao kuondoa hofu hiyo kwa kuwa mgonjwa huyo mwanaume amethibitika kuwa ana Maleria kali ambayo imekuwa ikimsumbua.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Halmashauri ya manispaa ya Moshi imeifunga zahanati ya kata ya Shirimatunda na kuwahamisha wagonjwa wanaouhudumiwa na zahanati hiyo katika Hospitali za manispaa hiyo ikiwemo ya Mtakatifu Joseph kwa hofu ya kuwepo kwa mgonjwa anayehudumiwa kwenye zahanati hiyo anadhaniwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...