Wednesday, January 29, 2014

HAPPY BIRHDAY DA SOO MAMAA WA KASH KASH CAPITAL RADIO,UZEE NDO HUOOOOOO TARTIIIIBU

SOPHIA RAJAB A.K.A DA SOO WA KASH KASH CAPITAL RADIO LEO ANATIMIZA MIAKA........NKITAJA UTASHANGAAA

MTANGAZAJI WA RADIO ONE ALAMBA TUZO YA UANDISHI BORA WA HABARI ZA MASUMBWI

OMAR KATANGA AKIWA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA BFT MUTA RWAKATARE MARA BAADA YA KUKABIDHIWA TUZO YA UANDISHI BORA WA HABARI ZA MASUMBWI YA RIDHAA NCHINI

TUZO BAADA YA KUWASILI NYUMBANI HAIKUCHELEWESHWA MOJA KWA MOJA UKUTANI KAMA INAVYOONEKANA IKIPAMBWA NA PICHA

OMAR KATANGA MTANGAZAJI MAHIRI WA KIPINDI CHA MICHEZO RADIO ONE AKIWA NA TUZO YAKE

Tuesday, January 28, 2014

WAUZA DHAHABU FEKI WANASWA DAR

H
MMOJA KATI YA MATAPELI HAO AMBAE NDIYE MMILIKI WA GARI LILILOTUMIKA KUTAPELIA AKIWA KWENYE OFISI YA MPELELEZI KITUO CHA POLISI CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM


GARI BAADA YA KUKAMATWA NA WANANCHI KWENYE FOLENI WALILIHARIBU KAMA LINAVYOONEKANA

WATUHUMIWA WENGINE

GARI BAADA YA KUHARIBIWA NA WANANCHI WENYE HASIRA

GARI YENYE NAMBARI T859 AVV ILIYOTUMIKA KWENYE UTAPELI HUO

WATYUHUMIWA WAKIWA CHINI YA ULINZI POLISI CHANG'OMBE









WATU WATANO WANAODHANIWA KUWA NI MATAPELI WALINUSURIKA KIFO BAADA KUPEWA KIBANO NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMUUZIA DADA MMOJA DHAHABU BANDIA.

BAADA YA JKUWAKABIDHI KIASI CHA SHILINGI MILIONI MBILI WATU HAO WAKAONDOKA HARAKA ENEO LA TUKIO WAKIJUA MPANGO WAO UMEKAMILIKA.
MUDA SI MREFU DADA HUYO AKAGUNDUA KUWA DHAHABU ZILE NI BANDIA NDIPO ALIPOKODISHA PIKIPIKI NA KUANZA KUWAFUKUZIA NA KWA BAHATI NZURI KWAKE ALIWAKUTA KWENYE FOLENI ENEO LA CHUMA ROAD KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WALIWADHIBITI,NA KWA KUANZA KULIPIGA GARI LAO MAWE,NDIPO POLISI WAKAPATA TAARIFA NA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUWANUSURU WATU HAO KISHA KUWAFIKISHA KATIKA KITUO CHA POLISI CHANG'OMBE.

BAADHI YA PICHA ZA MALORI YALIYOFUNGA BARABARA NA KUSABABISHA MAELFU YA ABIRIA KUKWAMA NZEGA BAADA MWENZAO KUTEKWA,KUUAWA NA KUTOBOLEWA MACHO






TANESCO MKIKUSANYA BILI MKUMBUKE NA KUKARABATI MAGARI YENU MABOVU YALIYOPO BARAGBARANI

GARI HILI LA TANESCO BONETI LINAONEKANA KUWA BOVU NA BADO LIPO BARABARANJI,TRAFFIC HAMLIONI HILI??

GARI BOVU LA TANESCO 


BONETI LIKIWA BOVU HALIFUNGI

Monday, January 13, 2014

BIBI MMOJA ABAKWA NA VIJANA ENEO LA CHANIKA



chumba cha bibi huyo



sehemu ambapo bibi huyo alibakwa

nyumba anayoishi bibi huyo




akipakiwa kwenye piki piki kukimbizwa hospitali

Bibi mmoja jina tunalihifadhi amevamiwa na kubakwa nyumbani kwake maeneo ya Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati amelala.

Mashuhuda wa tukio hili wanasema bibi huyo alivamiwa na kundi la vijana nyumbani kwake usiku wakati nyumba ya pili tu anakokaa bibi huyo kulikuwa na kigodoro ambapo wakazi wa maeneo mbali mbali hapa jijini hukesha kwa kucheza ngoma na muziki usiku kucha.

Vijana hao walipovunja mlango wa bibi huyo wakamtoa hadi kwenye korido yake na mmoja wapo akambaka na kumlawiti wengine wakakimbia kwa kuhofia kukutwa.

Baadae wakamuacha bibi huyo akiwa akiugulia maumivu,na badala ya kumpeleka hospitali kuna jirani akawa anamkanda tu nyumbani hadi majirani walipogundua hali hiyo ndiyo wakampakia kwenye piki piki na kumkimbiza hospital.

TAARIFA YA IKULU KUHUSU MAPUMZIKO YA LEO

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz            
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
     THE STATE HOUSE,
      P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
                                       

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muunganol wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa leo,Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako jana ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.​

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa leo itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako jana ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.​

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michez wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.


Mwisho
Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es Salaam.
12 January, 2014

Friday, January 10, 2014

UNAKIKUMBUKA KIKOSI CHA PAMBA FC YA MWANZA WANA TP LINDANDA MIAKA YA '80 ?


Waliosimama toka kushoto - Madatta Lubigisa, Rajabu Musoma, Beya Simba, Nteze John “Lungu”, Kitwana Selemani “Popat”, Fumo Felician (Mzee wa mishuti), Pascal Mayala, Paul Rwechungura.

Waliokaa toka kushoto- George Gole, Khalfan Ngassa (mzee wa makanzu), Ally Bushiri, Alphonse Modest (beki mtulivu), Mao Mkamy (Ball Dancer), Saleh Muhammad (aliziba pengo la masatu), Hamisi Nyembo, Nico Bambaga

MESSI AREJEA KWA KISHINDO ATUPIA MBILI DHIDI YA GETAFE

Back in action: Lionel Messi celebrates scoring on his return from injury in the Copa del Rey clash with Getafe
Messi akishangilia goli baada ya kurejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi.

On strike: Messi strikes the ball to score after returning from a spell on the sidelines with a thigh injury
 Messi akifunga goli mara tu aliporejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kupata majeraha ya paja,messi alitupia mbili kati nne dhidi ya getafe.

 Lionel Messi amefunga mabao mawili akiwa amerejea baada ya kukaa nje kwa miezi miwili akisumbuliwa na tatizo la misuli na kuisaidia Barcelona kuichapa Getafe 4-0 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya tano ya Kombe la Mfalme.

Tangu alipoumia Novemba 10 mwaka jana, Messi aliingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuchukua nafasi ya Andres Iniesta alifunga bao lake la kwanza dakika ya 61 na ya 87 akimalizia kazi ya Martin Montoya. Hilo lilikuwa ni bao lake la 16 na 17 msimu huu.

‘’Nilijisikia vizuri wakati wa mazoezi pamoja na kuwa walinifanyia vipimo lakini unapoingia uwanjani kila kitu kinakuwa tofauti,’’ alisema Messi na kuongeza. ‘’Mwili wangu upo safi kabisa, sijahisi maumivu yoyote ya misuli.’’

‘’Nilicheza nikiwa ni majeruhi,’’ alisema Messi ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa siku 59.

‘’Lakini nashukuru nimefanikiwa nimepona na sasa nimeanza vizuri mwaka huu.’’

Mwanasoka huyo bora mara nne wa Fifa alikosa mechi 12 za msimu huu kwa sababu ya kuumia.

Cesc Fabregas aliifungia Barcelona bao la kuongoza dakika ya saba na kupachika la pili kwa mkwaju wa penalti  61, likiwa ni bao lake la 11.

Mechi ya marudiano dhidi ya Getafe itafanyika Januari 16.

Real Betis inayoshika nafasi ya mwisho katika Ligi ya Hispania, iliichapa Athletic Bilbao, nayo timu ya daraja la pili ya Alcorcon ilishinda 1-0 dhidi ya Espanyol huku Racing Santander wakitoka sare na Almeria.

Manchester City iliisambaratisha West Ham 6-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi, huku Alvaro Negredo akifunga mabao matatu.

Hicho ni kipigo cha pili kikubwa kwa West Ham ndani ya siku nne.

Edin Dzeko alifunga mabao mawili na Yaya Toure moja kwa City, inayosaka kucheza fainali ya Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1976.

OPA IPO SOKONI WASILIANA NA ABOUBAKARY SADIQ 0713 561556







GARI AINA YA OPA T937 BBU INAUZWA NA IKO KWENYE HALI NZURI SANA, IMETUMIKA LAKINI HAIJAWAHI KUGUSWA ENGINE.KILA KITU KIPO INTACT.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA ABOUBAKARY SADIQ KWA SIMU NAMBARI 0713 561556

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA NA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA , KATIKA MLIMA NYOKA


 Miili ya Marehemu ikiwa imetelekezwa katika mlima nyoka
 Miili ya Marehemu baada ya kupigwa vibaya
 Kiatu vya mmoja wa marehemu aliye uawa
Hapa ni eneo marehemu walipo jaribu kukimbia

Baadhi ya mashuhuda akiwemo mwenyekiti wa Bajaji wa pili kushoto na watatu mwenye begi mgongoni mwenyekiti wa Bodaboda wakiwa eneo la tukio Mlima Nyoka
Picha na Ezekiel Kamanga 


Mbeya yetu Blog

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO MKOANI TABORA


Watu wawili wamekanyagwa na tembo na kupoteza maisha katika kitongoji cha Nyampindi wilayani Uyui mkoani Tabora ,  huku familia tisa zikikabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na akiba yao kuliwa na wanyama hao, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wananchi wanalima na kuishi katika njia za tembo hao.

Hayo yamebainishwa na mtendaji wa kijiji cha Songambele kata ya miyenze wilayani Uyui mkoani Tabora Bi Malieta Makenga wakati akitoa taarifa kwa mwenyekiti wa umoja wa wabunge wanaojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyamapoli, tembo na faru pamoja na vyanzo vya maji waliokwekuwa katika kukagua hali ya uhalibifu wa mazingira, katika mikoa ya Lindi, Rukwa Katavi na Tabora.

Akizungumza na wananchi waliokumbwa na adha hiyo katika kijiji cha Songambele, mwenyekiti wa umoja huo Mhe. Riziki Saidi Ruliga, mbunge viti maalum CCM mkoa wa Lindi, amesema kuwa pamoja na kuwepo uharibifu mkubwa wa mazingira, ameitaka serikali kuanzisha rasmi tume ya haki za wanyama, kwa lengo la kuhifadhi wanyama hao.

Aidha akizungumzia fursa za wananchi katika kupambana na mauaji ya wanyama ambao ni rasilimali za taifa, makamu mwenyekiti wa umoja huo mbunge wa jimbo la Igarula Mhe. Mhandisi Dk Athumani Mfutakamba amewataka wananchi kwa pamoja kuwa na mshikamano wa kuchukia vitendo vya ujangili, vinavyofanywa na baadhi ya watu na kutoa taarifa za siri ili watiwe mbaloni.

BASI LA MTEI EXPRESS LATEKETEZWA KWA MOTO NA WANANCHI BAADA YA KUWAGONGA NA KUUA WATOTO WATATU WA FAMILIA MOJA HUKO SINGIDA


DSC05595

DSC05594

DSC05596

DSC05599
DSC05601
Watoto watatu wa familia moja  ambao walikuwa wamepanda pikipiki wamekufa  baada ya kugongwa na basi  la Mtei express katika njia kuu itokayo Singida hadi Arusha ambapo baada  ya tukio hilo wananchi wenye hasira waliamua kulichoma moto basi hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Singida  SACP Gefrey Kamwela  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Mtei  Express lenye usajili wa namba T 742 ACU lilikuwa likitokea Singida na kuelekea  jijini Arushana pikipiki aina ya Slag yenye usajili wa namba  T368 BXZ ambayo ilikuwa imepakia watoto watatu na baba yayo akiendesha.

Katika hatua nyingine kamanda Kamwella amewataja waliokufa papo hapo ni  Tabiri Shabani,Kasimu Shabani na Hamza Shabani kafa wakati akipatiwa matibabu na dereva wa pikipiki ambaye ni baba wa watoto hao  amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo ambaye naye alikuwa abiria bwana Nakomolwa Thomas amesema dereva wa pikipiki aliamua kukata kona upande wa kulia bila ya kuangalia kama nyuma kuna basi lina kuja na kusababisha kugongwa na basi na kuburuzwa hadi pembeni mwa barabara.

Naye Nganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktali Banuba Deogratius amesema wamepokea maiti mbili , mtoto moja amefariki wakati  wanampatia huduma na mwingine ambaye ni baba watoto hao bado anaendelea na matibabu.

Wednesday, January 8, 2014

SAMAKI AINGIA TUMBONI KWA MSICHANA KUPITIA SEHEMU ZA SIRI HUKO BUNDA MKOANI MARA

 

MAISHA ya mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini baada ya kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na kukimbilia tumbani.

Tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu iliyopo kandokando
ya ziwa hilo.

Akizungumza na Majira, kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka 31, alisema tukio hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji vyake.

Alisema mdogo wake alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.

"Mdogo wangu alifanya jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni na kuanza kupata maumivu makali,kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa na miba ya
mgongo wa samaki huyo.

"Baada ya tukio hilo, alirudi nyumbani kwa shida akijivuta na kuugulia maumivu...alimweleza mama na ndugu zake juu ya mkasa huu, walimchunguza na kujaribu kuingiza mkono sehemu za siri wakidhani watampata lakini hawakufanikiwa," alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kumpeleka zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya akilalamika maumivu makali tumboni ambapo familia inaamini tukio hili limetokana na imani za kishirikina hivyo waliamua kumtoa katika zahanati hiyo.

"Tulimpeleka kwa mganga wa kienyeji kijiji cha Amuyebe,wilayani Ukerewe...katika hali ya kawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama tumboni.

"Pamoja na kuchukua uamuzi wa kumpeleka kwa mtaalamu,hali yake bado inazidi kuwa mbaya, hata baba yetu alifariki katika mazingira yenye utata mwaka 2003," alisema.

Aliongeza kuwa, hata kaka zake watatu na mtoto huyo nao walifariki kwa mfululizo mwaka 2004, 2005, 2006 ambao vifo vyao viligubikwa na utata mkubwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limewashangaza watu na kuahidi uongozi wa kitongoji hicho utaendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Diwani wa Kata ya Napindi, Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Bunda Mjini,alikiri kupokea taarifa za tukio hilo kwa mshangao mkubwa.

"Nitalifuatilia kwa karibu baada ya kurudi kijijini kwa kufanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea kwani sijawahi kusikia tukio kama hili katika umri nilionao," alisema.

Taarifa zilizopatikana kutoka Ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema kwa sasa hawezi kuzungumza akizidi kulalamika maumivu makali ya tumbo na samaki huyo bado hajatolewa. MAJIRA.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...