Wednesday, February 26, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWAMBEGELE KATA YA KYIMO, TARAFA YA  UKUKWE BARABARA YA  TUKUYU/MBEYA WILAYA YA  RUNGWE. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI  T.873 BZA/T.501 CCZ AINA YA  HOWO TRUCK MALI   YA  CHAINER TRUCK COMPANY LTD LILILOKUWA  LIKIENDESHWA NA DEREVA JOHN MATHIAS @ MWIMBILIZYE (40), MKAZI WA DSM, LIKIWA LIMEBEBA MAKAA YA  MAWE KUTOKA NCHINI MALAWI KUELEKEA DSM KUACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU AMBAO NI DEREVA WA GARI HILO, PAMOJA NA WATU WENGINE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA ISAYA, MIAKA KATI YA  43-45, DALALI, MKAZI WA UYOLE  NA SALUM, MIAKA KATI YA  40-42, MSAIDIZI WA DEREVA. PIA MAJERUHI NI HAMISI RAMADHAN (40), DALALI, MKAZI WA UYOLE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA TUKUYU NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SPRIANO WILSON (40), MKAZI WA IFUMA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA ROBO HEKTA LIKIWA NA MICHE YENYE UREFU WA FUTI TATU [03]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:30HRS ASUBUHI
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAGERA, KIJIJI CHA IFUMA, KATA YA   LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MICHE 27 YA BHANGI KATIKA SHAMBA LAKE.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ISRAEL MWAMBENE (39), MKAZI WA SIMIKE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MICHE YA BHANGI 27, YENYE UREFU WA FUTI 2.5 ALIYOKUWA AMELIMA KWENYE SHAMBA LA MIGOMBA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:20HRS MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MALIBILA, KIJIJI CHA SIMIKE, KATA YA  LUFINGO, TARAFA YA  UKUKWE WILAYA YA  RUNGWE. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MWILI WA BALOZI KAZAURA ULIVYOWASILI KUTOKA INDIA



 Waombolezaji wakisukuma jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), marehemu Balozi Fulgence Kazaura ulipowasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)Mmiliki wa www.ujijirahaa.blogspot.com
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akiwafariji ndugu wa marehemu
 Ndugu jamaa na wafanyakazi na aliye kushoto ni Dereva wa gari la kubeba mwili huo  wakifunua jeneza kwa utambuzi  wa  mwili wa marehemu Kazaura mara ulipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India.
Wakiutoa nje tayari kwa kuondoka uwanjani hapo kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni
 Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni,kulia ni dereva wa gari litakalo beba mwili

Saturday, February 22, 2014

WAJUE MABILLIONEA WA DUNIA


HAWA NDIYO MABILIONEA WA DUNIA

Viwango vipya vimetolewa vinavyoonyesha watu matajiri zaidi duniani,kwa mujibu wa mtandao wa forbes kwa mwaka 2013 idadi imeongezeka hadi kufikia majina 1,426,na utajiri wao unafikia hadi dola za kimarekani trillioi 5.4 kutoka dola trillion 4.6.

Majina mapya yaliyoongezeka ni 210 na kwa mara nyingine matajiri wa Marekani wameendelea kuongoza kwa kuwa na mabilionea 442,wakifuatiwa na Asia 386, Europe 366, Mashariki ya kati na Africa 103.

 Carlos Slim kwa mara nyingine ameongoza kuwa billionea namba moja duniani akifuatiwa na Bill Gates. Amancio Ortega wa Hispania amekuwa wa tatu kwa mara ya kwanza.

Amekuwa mtu ambae ameingiza pesa kwa kiasi kikubwa kiasi cha dola billioni 19.5 kwa mwaka mmoja ambapo amempita Warren Buffett ingawa mwekezaji huyo wa kimarekani ameongeza dola biloni 9.5, huu ni mwaka wake wa kwanza kuwa nje ya tatu bora tangu mwaka 2000.

Mtu ambae ametia fora kwa kushindwa kuliko wote ni mbrazil Eike Batista ambae amedondoka kutoka kujiingizia kwa mwaka dola bilioni 19.4 sawa na dola millioni 50 kwa siku na amedondoka hadi nafasi ya saba kati ya matajiri 100 duniani.

MMILIKI WA WHATSAPP ALISHAWAHI KUNYIMWA AJIRA KATIKA KAMPUNI YA TWITTER NA FACEBOOK


Waanzilishi wa Whatsapp: Brian Acton na Jan Koum.
Katikati ya mwaka 2009, Brian Acton alikuwa software engineer ambaye hakuna kampuni iliyotaka kumwajiri. Pamoja na uzoefu wa miaka zaidi ya 10 kama mwajiriwa wa Yahoo na Apple Computer, alitosa kuajiriwa kwenye makampuni ya Facebook na Twitter.
Kwanza walikuwa Twitter waliomkataa mwezi May. Tarehe 23, May mwaka 2009, Brian Acton ‏alitweet: Got denied by Twitter HQ. That’s ok. Would have been a long commute.”
Kisha Facebook waliokataa kumchukua mwezi August. Tarehe 3 August, 2009 akatweet: Facebook turned me down. It was a great opportunity to connect with some fantastic people. Looking forward to life’s next adventure.”
Baada ya Acton kukosa kazi kwenye makampuni hayo, aliamua kuanzisha kitu chake mwenyewe. Aliamua kuungana na aliyekuwa mwajiriwa mwenzake wa Yahoo, Jan Koum, kuanzisha WhatsApp, ambayo leo imekuwa mfalme wa mawasialino ya ujumbe duniani. WhatsApp inatawala vichwa vya habari wiki hii sababu Facebook imekubali kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 19.


Akiwa na asilimia 20 ya hisa kwenye kampuni, Acton atakuwa tajiri wa dola bilioni 3. Historia yake imegeuka kuwa funzo la watu kutokata tamaa kwa wale wanaotafuta kazi. Story yake pia itawapa uchungu waajiri. Kuajiri watu sahihi ni jambo la bahati lakini hakuna kampuni kubwa duniani itapenda kuwa maarufu kwa kuacha Brian Acton mwingine aondoke.
Chanzo: Forbes/Kamanda wa matukio

LORI LILIVYOUA WANNE BAADA YA KUANGUKA NA KUWAKA MOTO KATIKA MILIMA YA SEKENKE



                                        Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
                                Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto
                                       Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

                               Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
                                                  Hii ni njia ya mlima sekenke
                                Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hilo
Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana
Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.
 
Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius Chacha alipoongea na mtandao  wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
 
Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwani moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
 
Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.

Tuesday, February 18, 2014

ADHA YA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM

MTU MMOJA AMBAYE AMEJITOLEA KUWAVUSHA WANAFUNZI WALIOKUWA WANASHINDWA KUVUKA MTO KIWALANI KUTOKANA NA MVUA ZILIZO NYESHA NA MTO HUO KUJAA MAJI

DADA HUYU AMBAJINA LAKE HALIKUPATIKANA MARA MOJA AKIWASAIDIA WANAFUNZI KUWAVUSHA KWENYE MTO KIWALANI WANAFUNZI HAO WANASOMA KATIKA SHULE YA MSINGI YA VETENARI LEO

WANAFUNZI WAKIVUKA MTO KIWALANI WAKIELEKEA SHULE YA MSINGI YA VETENARI LEO MTO HUO NI KIUNGO MUHIMU KATIKA YA KIWALANI MINAZI MIREFU NA TEMEKE VETENARI MAARUFU KAMA MCHICHA

WANAFUNZI PAMOJA NA WATU MBALIMBALI WAKIVUKA MTO KIWALANI ENEO LA MCHICHA

LULU ALIVYOTINGA MAHAKAMANI

LULU AKINGIA KATIKA MAHAKAMA KUU KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI YA KUUA BILA KUKUSUDIA ALIEKUWA MPENZI WAKE  KANUMBA 

KULIA DR CHENI WA PILI KULIA NI LULU NA MAMA YAKE LULU WA TATU KULIAWAKIWA  KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA KUU 

LULU

LULU AKITOKA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA KUU 

LULU AKINGIA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA TAYARI KUSIKILIZA KESI YAKE

LULU AKISINDIKIZWA NA DR CHENI KATIKA MAHAKAMA KUU

LULU AKINGIA KWENYE MAHAKAMA KUU LEO

LULU AKINGIA KWENYE CHUMBA CHA MAHAKAMA KUU

LULU AKINGIA KWENYE CHUMBA CHA MAHAKAMA KUU

LULU AKIONGEA NA MWANASHERIA WAKE WAKILI KIBATARA

LULU AKIJARIBU KUWAHI MAHAKAMANI

Monday, February 10, 2014

KIWEWE CHA KIPIGO CHAMPA MWEREKA MZEE WENGER

KOCHA WA ARSENAL MZEE ARSEN WENGER AMEKULA MUEREKA BAADA IKIWA KAMA KIWEWE BAADA YA KUPOKEA KIPIGO CHA MAGOLI 5-1,DHIDI YA LIVERPOOL,BAADAE AKAPATA MSAADA WA KUINULIWA NA WANAUSALAMA WA UWANJANI HAPO KAMA ANAVYOONEKANA KWENYE PICHA HAPO JUU.

WATANI WA TIMU HIYO WANASEMA ARSENAL WALIPIGWA 8 NA MAN UNTD,WAKAPIGWA 6 NA MAN CITY NA SASA WAMEPIGWA 5 NA LIVERPOOL...KWA VIPIGO HIVYO WAMEAMUA KUBADILI JINA,SASA WANAJIITA WABEBA MITUTU WA KIKOSI CHA 865 KJ.....................

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA MKOANI MARA AFARIKI DUNIA

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA MKOANI MARA BW CHARLES KICHUNE MARA BAADA YA KUTIWA MBARONI

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA AMBAE NAE SASA NI MAREHEM BW CHARLES KICHUNE


AKIWA CHINI YA ULINZI MKALI ILI WANANCHI WAMUONE
Mtuhumiwa ya mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilaya ya Tarime mkoani mara,aliyekuwa akihojiwa na polisi kwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili,amefariki dunia katika hospitali ya wilaya wakati akipatiwa matinbabu ya ugonjwa wa pumu.

Kamanda wa polisi Tarime na Rorya kamishna msaidizi wa polisi Justus Kamugisha,amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halisi ni Charles Kichune(38),alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa huo wa pumu.

Majina mengine aliyokuwa anayatumia  kwa mujibu wa kamanda Kamugisha ni pamoja na Josephat Chacha na Charles Msongo.

Amesema mwili wwake upo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake.

Baadhi ya raia waliouawa ni pamoja na David Yomam,Samuel Matiko,Robert Machimbe,Zakaria Marwa,Juma Nyaitare,Juma mwita,Marwa Mwita na Erick Makanya.

Kwa Mujibu wa Kamanda Kamugisha,Kichune baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi alikiri kuhusika katika mauaji ya watu mbalimbali katika kata za Binagi,Turwa na Kitare katika vijiji vya Mogabiri,Kenyamanyori,Nkende na Rebu.

 KUHUSU KUKAMATWA KWAKE

Awali kamanda Kamugisha alitangaza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na alisema kwamba,“Mtu huyu amekamatwa mkoani Tanga Februari 6 majira ya saa 1:30 jioni. Hata hivyo hakuwa na silaha yoyote ndani ya begi lake la nguo. Takribani raia 9 wameaga dunia kwa kuuawa na mtu huyu, ambaye amekiri kuhusika na matukio hayo yote.

“Baada ya kumweka chini ya ulinzi na kuanza kumhoji, ndipo tukagundua kuwa si yeye peke yake anayefanya matukio haya bali wako wengi japokuwa aliyekuwa akifahamika ni yeye tu,” alisema.

Kamanda Kamugisha alisema, alipohojiwa zaidi mtu huyo alieleza ilipo silaha anayoitumia na kuwaomba askari kuwapeleka alikokuwa ameificha. 

“Polisi mkoani Tanga waliondoka hadi mkoani Mara, ambapo aliwafikisha kwa jambazi mwenzake aliyemwachia baada ya kuona kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumtafuta.

“Aliwapeleka maofisa wa Jeshi la Polisi hadi Kijiji cha Bweri Musoma mjini, kwa mwenzake aliyemtaja kwa jina la Marwa Keryoba au Alex anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 38, ambaye ni mkazi wa Sirari akiishi Musoma.

“Wakati polisi wanaingia kwa Keryoba, aliwasikia na kutoka nje akiwa amevaa koti refu jeusi kisha kulitupa chini kwa lengo la kupoteza mwonekano wake. 

“Hata hivyo polisi walipiga risasi juu kumtaka ajisalimishe, japo alianza mashambulizi kuwashambulia maaskari hao.

“Askari walimuua Keryoba kwa kumpiga risasi baada ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, lililomtaka ajisalimishe, kwa vile alikuwa amebeba silaha ya SMG iliyokatwa kitako na mtutu huku imefutika namba,” alisema Kamugisha na kuongeza:

“Baada ya kumpekua walimkuta akiwa na vitu vifuatavyo, SMG iliyofungwa tochi kwenye mtutu, magazine moja yenye risasi kumi na kwenye nyumba aliyokuwa anaishi marehemu zilipatikana simu mbili za mkononi.

“Vitu vingine ni CD 21 za picha mbalimbali, deki moja, viatu pea mbili aina ya buti, tochi mbili na mpira wa baiskeli pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani,” alisema.

Kamugisha aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kurahisisha utendaji wa kazi wa chombo hiki chenye dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Wednesday, February 5, 2014

WATU 12 WANAODAIWA KUWA NI RAIA WA IRAN NA PAKISTAN WAMEKAMATWA NA SHEHENA YA MADAWA ZA KULEVYA KATIKA BAHARI YA HINDI WAKIWA WANAELEKEA ZANZIBAR KWA KUTUMIA JAHAZI AMBALO HALIJULIKANIK LILIKUWA LINATOKA NCHI GANI


JAHAZI LILILOKLAMATWA LIKIWA NA MADAWA YA KULEVYALIKIWA BANDARINI 

MADAWA YAKIWA  KWENYE BAHASHA WAKIYAHIFADHI


BAADHI YA MAAFISA WA JESHI LA POLISI  WAKIKAGUA MADAWA HUKU KUSHOTO IKIONEKANA JAHAZI LILILOBEBA MADAWA

KAMANDA NZOA AKIONYESHA MADAWA YALIYOKAMATWA

HAYA NDIO MADAWA YA KULEVYA YALIYOKAMATWA LEO KATIKA JAHAZI  WAKIWA KATIKA BANDARI YA DAR SALAAM
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...