Monday, March 10, 2014

WATAALAMU WA USALAMA WA ANGA WATOA SABABU ZINAZOHISIWA ZIMESABABISHA NDEGE YA SHIRILA LA NDEGE LA MALAYSIA KUANGUKA



NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA BOING 777 ILIYOPOTEA NA MPAKA SASA HAIJULIKANI ILIPO IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200


WATAALAM WA VIETNAM WAKIWA KATIKA NDEGE KUFUATILIA ENEO AMBALO WANAHISI NDEGE HIYO ILIANGUKA

SEHEMU HII INAONYESHA MAFUTA YAKIWA YANAELEA WATAALAM WA VIETNAM WANAHISI IMEANGUKIA HAPA
SEHEMU INAPOHISIWA KUWA NDEGE YA MALAYSIA IMEANGUKA

WAPENZI HAWA WALIKUWEMO KATIKA NDEGE HIYO NA INAHOFIWA WAMEPOTEZA MAISHA

MOJA YA FAMILIA YA WATU WALIOSAFIRI NA NDEGE HIYO

NDUGU WA ABIRIA AKILIA KWA UCHUNGU MARA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA KUPOTEA KWA NDEGE HIYO

WAZAZI HAWA MAMA MWENYE SURUALI NYEUSI NA BABA MWENYE JAKETI JEUSI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIJANA WAO NA MPENZI WAKE KABLA YA KUONDOKA KUALA LUMPUR NA NDEGE ILIYOPOTEA

 Wataalam wa masuala ya anga wanasema wakati mgumu na tete kwa ndege yeyote ni wakati inataka kuruka au kutua,mara chache sana matukio yasiyokuwa ya kawaida huwa yanatokea pale ndege inapokuwa angani umbali wa takribani mile saba sawa na kilometa 11 kutoka usawa wa ardhi.
  

Kwa  hiyo kwa kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysi awakati ikiwa angani siku ya Jumamosi asubuhi ikiwa na abiria zaidi ya 200 katika bahari ya kaskazini mwa China,imefanya wataalamu wa masuala ya anga kubaini kwamba chochote ambacho kitakuwa kimetokea basi kitakuwa kimetokea ghafla na kwa haraka mno kiasi cha kumfanya hata rubani wa ndege hiyo kushindwa kupiga simu ya dharula. 


Inaweza ikachukua miezi au hata mwaka kwa wachunguzi wa ajali za ndege kubaini kile kilichotokea kwa ndege hiyo ya shirika la ndege la Malaysia boing 777 iliyoruka kutoka mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur kuelekea China.


Mmoja kati ya wachunguzi hao wa ajali za ndege bw Todd Curtis ambae ni mhandisi wa masuala ya ndege mstaafu,amesema katika hatua ya awali kabisa ya uchunguzi wao wanajitahidi kutafuta ukweli wa mambo ambayo mpaka sasa hawayajui.Todd ameshafanya kazi kwenye ndege hiyo boing 777 na sasa ni mkurugenzi wa taasisi moja ya usalama wa ndege huko Malaysia Airsafe.com foundation.


Radar ya jeshi imebashiri kwamba ndege hiyo iliyopotea Boing 777 inaweza kuwa iligeuza safari iliyokuwa imeianza kabla ya kupotea,Mkuu wa shirika la ndege la Malaysia amesema siku ya Jumapili kwamba mamlaka inachunguza abiria wanne ambao utambulisho wao unamashaka.Hii itaonyesha mazingira yalivyokuwa katika dakika za mwisho kabla ndege haijapata ajali.Mkuu wa shirika la ndege hakubainisha muelekeo wa ndege hiyo kabla ya ndege hiyo kupoteza uelekeo au ilikwenda umbali gani kabla ya kupotea ila baadhi ya taarifa zinatafutwa kwa kushirikiana na radar ya mtu binafsi.


Kama zikipatikana taarifa sahihi kuwa ndege hiyo iligeuza na kurudi ilikotoka kabla ya kupotea,basi kuna uwezekano mkubwa kuwa ndege hiyo ilikubwa na tatizo kubwa wakati ikiwa angani lakini maswali mengi yanaibuka kwa nini rubani hakutoa ishara yeyote katika chumba cha kuongozea ndege ili apate msaada.Kama kulikuwa na matatizo kidogo ya kiufundi au engine zote mbili za ndege zilizima,rubani lazima angekuwa na muda wa kupiga radio ya upepo,Kutokupiga kwake radio ya upepo kunatoa picha kwamba kuna kitu cha ghafla mno kilitokea hadi akashindwa kufanya chochote, alisema William Waldock ambae anafundisha masuala ya uchunguzi wa ajali za ndege katika chuo cha Embry-Riddle Aeronautical Arizona.


Inawezekana kuwa aidha lilitokea tatizo la ghafla au kitu cha haraka kilichosababisha ikaanguka.Baadhi ya wataalam wanadhani inawezekana pia likawa ni tukio la ugaidi au rubani akawa ameiangusha kwa makusudi.





Haijalishi tukio hili limetokea kwa namna gani,lakini ni mapema mno kusema kitu halisi kilichotokea,Kitu cha msingi ni kusubiri mabaki ya ndege hiyo yatakapopatikana na kupatikana kwa kisanduku kinachohifadhi sauti na uchunguzi wa tatizo.Wachunguzi wa kimarekani kutoka FBI,Bodi ya usafiri Salama ya taifa na shirikisho la uongozi wa anga, na wataalam wa ndege aina ya Boeing wote wameelekea Asia kusaidia uchunguzi huo.

Utafutaji wa hali ya juu umeshafanyika baharini lakini mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa kupatikana kwa ndege hiyo,ingawa Serikali huko Vietnam imesema kuwa Jumapili jioni ndege yao ilikuwa inapita chini chini katika bahari iliona kitu kama cha pembe tatu kilomita karibu 90 sawa na mile 56 kusini mwa kisiwa cha Tho Chu,sehemu hiyo hiyo ambayo mafuta yameonekana yakielea siku ya Jumapili,lakini gazeti la serikali limesema mkuu wa jeshi msaidizi wa Vietnam amekaririwa akisema kitu hicho kilichoonekana baharini ni mlango wa ndege.




Baadhi ya mambo yanayohisiwa kuwa yamesababisha ndege hiyo kupotea ni  muundo wa umbo la ndege ambao ni Alluminium,hali mbaya ya hewa,Rubani kutotambua tatizo mapema,kuzima au kushindwa kufanya kazi kwa ingini zote mbili za ndege,kupigwa bomu au kutekwa hizi ni baadhi ya sababu zinazohisiwa na wataalamu wa ajali za ndege na usalama wa anga kuwa zimesanbabisha ndege hiyo kupotea.

Sunday, March 2, 2014

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.


MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.


Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.


Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo

Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo



MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.
Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.
Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.
Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.
Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.

Na Mbeya yetu

MALORI YAFUNGA BARABARA BAADA YA MMOJA WA DEREVA WA MALORI HAYO KUVAMIWA NA KUJERUHIWA NA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI


BAADHI ya Magari yaliyokwama kupita (yaliyofunga barabara kuu ya Dodoma-Singida hadi Nzega), baada ya majambazi kuteka malori mawili katika kijiji cha  Kisaki, mkoani  Singida.

Watu zaidi ya ishirini wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliovamia  na kuyateka  malori mawili makubwa ya mizigo katika kijiji cha Kisaki nje kidogo ya Mji wa Singida, barabara kuu ya Dodoma-Singida hadi Nzega na kusababisha mabasi na malori zaidi ya 320 kushindwa kupita na kusababisha  kufunga njia kwa muda wa saa kaadhaa .baada ya kumteka dereva wa lori na kujeruhi na pamoja na abiria kuwanyanganya vitu katika eneola kisaki nje kidogo mwa  mji wa singida

ANGALIA PICHA JINSI YANGA WALIVYOKATA NGEBE ZA WAARABU

YANGA YAITANDIKA AL AHLY BAO 1 - 0 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

 Kikosi cha Yanga 
 Kikosi cha Al Ahly
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri akitafuta namna ya kumzuia katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Al Ahly ya Misri katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akizuiwa na Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri,Ramy Abdel Aziz katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
Kipa wa timu ya Al Ahly ya Misri,Sherif Ekramy Ahmed akida moja ya hatari iliyokuwa ikielekeshwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza.
 Heka heka ya kuwania mpira wa Kichwa.
 Mshambuliaji Machachari wa timu ya Yanga,Emmanuel Okwi akiwachachafya mabeki wa timu ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wao uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wa kuwania tiketi ya kusheza 16 bora ya Klabu Bingwa Barani Afrika.katika mchezo huo,Yanga imeifunga timu ya Al Ahly bao 1 - 0. 
 Emmanuel Okwi wa Yanga akichezewa faulo na mabeki wa timu ya Al Ahly ya Misri.
 Heka heka langoni mwa timu ya Al Ahly.
Mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Yanga leo ndio alikuwa mwiba kwa timu ya Al Ahly,maana alikuwa akikabwa na Mabeki wawili wawili........
 Kipa wa timu ya Al Ahly ya Misri,Sherif Ekramy Ahmed akiruka mithili ya nyani wakati akiokoa moja ya hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni kwake.
 Okwi anatafuta namna ya kuchia shuti.
 Mshambuliaji wa Yanga,Didier Kavumbagu akiwania mpira na Mabeki wa timu ya Al Ahly ya Misri.
 Ulinzi maridhawa kabisa ulitawala Uwanjani hapa.
 Ilikuwa ni nyomi la hatari.
Wachezajiwa timu ya Yanga wakishangilia ushindi wao sambamba na Mashabiki wao lukuki waliofurika uwanjani hapa.

Mfungaji wa bao pekee la Yanga,Nadir Haroub akirejea uwanjani baada ya kutoka kushangilia pamoja na washabiki wao.
 Benchi la ufundi la Al Ahly ya Misri.
 Benchi la Yanga.
 Mashabiki wa Al Ahly wakishangiliwa mwanzo mwisho,wakisaidiwa na Mashabiki wa timu ya Simba. 
 Okwiiiiiiii.......
Kocha wa Al Ahly akihaha kutoa maelekezo kwa Wachezaji wake. 
 Mabeki wa timu ya Yanga,Nadir Haroub pamoja na Kelvin Yondani wakiwa wamejipanga vyema kuuzuia mpira wa Mshambuliaji wa timu ya Al Ahly,Moussa Yedan.
 "Poa tu mwana,hii ni fea pleii tuuuuu......" 
 Ni shangwe tupu kwa Mashabiki wa timu ya Yanga uwanjani hapa hii leo. 
Mashabiki wa timu ya Al Ahly wakifungasha virago vyao baada ya kulala kwa bao 1 - 0.
 Kocha wa Yanga akisema na wachezaji wake mara baada ya kipenga cha mwisho kulia.
 Kufungwa kubaya jamaniiiiii....
 Mara baada ya Yanga kupata Goli la kwanza na la pekee,Mashabiki wa Simba walianza tena kunyoa viti na kuwarushia mashabiki wa timu ya Yanga waliokuwa wakishangilia ushindi wao huo. 
 Wazee wa feva wakiwatuliza washabiki hapo wa Simba.
Cheki mapengo ya kung'olewa kwa viti uwanjani hapa.Hali hii ni nani anatakiwa kuidhibiti???


 Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo wa leo dhidi yao na Al-Ahly ya Misri uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Canavaro amefunga bao hilo kufuatia mpira wa Kona iliyopigwa na Simon Msuva katika dakika ya 82. 
 Hongera Nahodha wetu.......
 Hili ndilo bao la Canavaro, Kipa wa Al-Ahly akiwa hoi chini baada ya kuchambuliwa......
 Kipa wa Al-Ahly akitafakari baada ya kufungwa bao hilo.....
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao hilo...
 Uwanja ulijaa kama hivi......
 Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia timu ya Al-Ahly wakiendelea na zoezi la kung'oa viti kama kawaida yao.....
 Mtanange ukiendelea uwanja wa Taifa, huku timu zote zikikosa kosa, hapa ni katika harakati za Yanga kukosa bao na Al Ahly kuokoa, mpaka sasa hakuna time yeyote iliyokwisha liona lango la mwenzake bado ni 0-0, sasa mpira ni kipindi cha pili.
 Hamis Kiiza, akijikunja kupiga shuti lililomtesa vilivyo kipa wa Al Ahly.
 Simon Msuva kijilaumu kukosa bao baada ya heka heka na jitihada alizoonyesha uwanjani katika kipindi cha kwanza.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MICHUZI BLOG NA SUFIANI MAPHOTO)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...