Wednesday, October 29, 2014

RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIA



Rais wa Zambia Michael Sata amefariki dunia nchini uingereza alikokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa ambao mpaka kifo chake haijawekwa wazi kuwa alikuwa anaumwa nini.

Rais Sata ambae alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mfalme Edward VII amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 77.

Taarifa zinasema rais huyo wa Zambia aliaga dunia baada ya mapigo ya moyo kupanda ghafla.

Hakuna taarifa ya mara moja juu ya mtu atayemrithi Rais Sata,suala hilo litaamuliwa na baraza la mawaziri la nchi hiyo linalotarajia kukutana leo Jumatano asubuhi.

akitangaza kifo cha rais huyo,katibu wa baraza la mawaziri Roland Msiska kwenye televisheni ya taifa ya nchi hiyo,alisema kwa masikitiko na mshtuko mkubwa,natangaza kifo cha rais wetu mpendwa Michael Sata.

Aliongeza kwa kusema kuwa mke wake na mtoto wake wa kiume walikuwa pembeni yake wakati rais huyo anakata roho.

Akawataka wazambia wote kuwa watulivu,wamoja kwa kipindi hiki kigumu cha msiba uliolikumba taifa hilo.

kifo cha Rais Sata kimekuja siku chache baada ya Zambia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waingereza.

Rais Sata anakuwa Rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani mwingine alikuwa ni Levy Mwanawasa alifariki dunia mwaka 2008.





Friday, October 24, 2014

MOTO WATEKETEZA MAGHALA 5 NA KUUNGUZA TANI ELFU TATU ZA MASHUDU MKOANI SINGIDA




Maghala matano ya kiwanda cha maunt meru Oil Miller cha mjini singida kimeteketea kwa moto na kuunguza zaidi ya tani elfutatu za mashudu ikiwemo mashine ya kukamulia mafuta na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Akieleza mkuu wa mkoa wa singida Dk.Parseko Kone amesema   kiwanda hicho ambacho kimeanza kuungua majira ya saa tano usiku wa tarehe ishini natatu hadi sasa,imebidi mkoa kuomba gari lingine kutoka mkoa wa jirani wa manyara ili kuweza kusaidia kuzima moto ambao bado unaendelea kuwaka.
 
Kwaupande wake kamanda wa polisi mkoa wa singida  kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Bwana Thobias Sedoyeka amethibitisha kuungua kwa kiwanda hicho na  jeshi la polisi limejitahidi kuweka ulinzi  na  amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi matukio kama hayo yanapo tokea.
 
Meneja wa kiwanda hicho Bwana Sajay Sumarzya  amesema wao walipata taarifa kutoka kwa walinzi usiku majira ya saa tano  na walipo fika walikuta maghala matano ya mashudu  yenye tani zaidi ya elfutatu  yakiwaka moto.

MUONEKANO WA KITUO KIPYA CHA DALA DALA KILICHOHAMISHWA KUTOKA UBUNGO


GAR LA DALADALA LIKITOKA KATIKA KITUO KIPYA CHA DALADALA CHA MAWASILIANO

BAADHI YA MAGARI YA DALADALA
 KATIKA KITUO KIPYA KINACHOJULIKANA KAMA SINZA TEMINAL ENEO LA MAWASILIANO

ABIRIA WAKIWA KATIKA KITUO KIPYA CHA DALADALA


MAGARI YAKICHEKIWA

HATA UDA YUPO KATIKA KITUO HICHO

BAADHI YA ABIRIA WAKIHANGAIKA KUTAFUTA KIBAO KINACHOANDIKWA SEHEMU ANAYOKWENDA(PICHA NA  MZUKA WA FUNGO)

WANANCHI WA MKOA WA KILIMANJARO WAONDOLEWA HOFU YA KUWEPO MGONJWA WA EBOLA MKOANI HUMO

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
Uongozi wa mkoa wa kilimanjaro umewaondoa hofu wananchi wake juu ya ugonjwa hatari wa Ebola kutokana na kuwepo mgonjwa anayehudumiwa katika zahanati ya Shirimatunda katika manispaa ya Moshi aliyedhaniwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mkuu wa mkoa huo bwana Leonidas Gama amewataka wananchi hao kuondoa hofu hiyo kwa kuwa mgonjwa huyo mwanaume amethibitika kuwa ana Maleria kali ambayo imekuwa ikimsumbua.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Halmashauri ya manispaa ya Moshi imeifunga zahanati ya kata ya Shirimatunda na kuwahamisha wagonjwa wanaouhudumiwa na zahanati hiyo katika Hospitali za manispaa hiyo ikiwemo ya Mtakatifu Joseph kwa hofu ya kuwepo kwa mgonjwa anayehudumiwa kwenye zahanati hiyo anadhaniwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

Wednesday, October 22, 2014

MIAKA 10 TANGU KIFO CHA FREDY NDALA KASHEBA

ndala-kasheba_2255445 
LEO tunatimiza miaka kumi toka kifo cha mwanamuziki mahiri Freddy Supreme au maarufu kama Ndala Kasheba. Freddy alianza kufundishwa gitaa na baba yake wakati akiwa na umri wa miaka 12. Baba yake alijua kupiga gitaa japo hakufanya kazi ya uanamuziki, alikuwa akipiga gitaa nyumbani baada ya saa za kazi. Moja ya bendi maarufu ambazo zilimtambulisha sana Fredd ilikuwa Orchestra Fauvette, Freddy alieleza kuwa bendi ya Orchestra Fauvette ilianza tarehe 7 mwezi wa sita mwaka 1964 katika jiji la Lubumbashi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Jina hilo Fauvette kwa kiswahili ni Chiriku, bendi ilikuwa na muimbaji ambaye waliamini alikuwa anaimba kama chiriku na hivyo kuipa bendi hiyo jina hilo. Vyombo vyao vya muziki walinunua Ujerumani kupitia duka la muziki la Dar es salaam Music House (duka lipo mpaka leo). Vyombo vilikuwa  vya aina ya Hofner, jina lililoheshimika sana kwa wanamuziki wakati huo.
IMG_2110
HILI NDILO KABURI LA FREDY NDALA KASHEBA LILIPO KINONDONI JIJINI DAR

Kati ya nyimbo ambazo zilipigwa katika kipindi hicho ni Camarade ya nzela, ambayo Freddy alieleza ni wimbo uliokuwa ukizungumzia rafiki wa kukutana nae barabarani au njiani, ambaye roho yake huwa kama sanduku la nguo, ambalo ndani yake huwezi kujua kuna nini. Pia ulipigwa wimbo Jacqueline ambao ulitungwa na mwenyewe Freddy ambao alieleza alikuwa alimtungia mpenzi wake aliyempenda Jacqueline. Wimbo mwingine uliopigwa katika kipindi hicho ni Nono na Kalemie, wimbo huu ulitunguiwa binti aliyeitwa Nono mkazi wa Kalemie ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa bendi ya Fauvette.
  Fauvette ilifika Dar na kuwa inapiga katika ukumbi wa White House Ubungo, lakini kwa miaka hiyo Ubungo ilikuwa mbali sana na mji, na kulikuwa na ajali nyingi zikiwapata wapenzi wa bendi katika usafiri wa kutoka kwenye muziki, hivyo bendi ikaamua kuhamia ukumbi wa Mikumi Tours ambapo walikuwa wakipiga Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Fauvette walikuwa na ndoto ya kuwa bendi bora Afrika. Hawakufikia huko lakini waliweza kuweka alama kubwa katika historia ya muziki wa Afrika mashariki na Kati
Kasheba aliweza kuimarisha jina lake zaidi alipolifanya maarufu gitaa la nyuzi kumi na mbili, mwenyewe akiliita nyuzi dazani, hasa alipoanza kulipiga kwa mtindo wa Dukuduku akiwa Safari Sound Orchestra. Pamoja na bendi hizo Kasheba pia alipitia Safari Nkoy, Zaita Muzika, Kasheba group, pia alipita Maquis, na kwa wiki chache alipitia Tancut Almasi.

Kasheba alifariki 22 Oktoba 2004 akiwa na miaka 58.

Tuesday, October 21, 2014

OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA


Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kwa kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi wa pili mwaka jana.Pia amehukumiwa miaka mitatu kwa kosa la kutumia vibaya silaha aliyokuwa anaimiliki kisheria lakini hukumu hiyo imesimamisha na badala yake atatumikia miaka mitano yote kwa pamoja.
oscar 2 oct 21 
Hukumu hiyo imetolewa na jaji mwanamama Thokozile Masipa baada ya kusikiliza kwa makini na kupima hoja za kila upande dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mwanariadha huyo wa Afrika kusini.


Pia hukumu ya miaka mitatu imetolewa baada ya kuitumia bastola kinyume na sheria pale alivyoifyatua chini ya meza kwenye mgahawa wa Tasha uliopo Johannesburg mwezi January mwaka 2013,mwezi mmoja kabla hajamuua mpenzi wake siku ya wapendanao february 14,2013.

HUKUMU ILIVYOSOMWA

Katika hukumu yake,jaji Masipa alianza kusoma mwenendo mzima wa kesi jinsi ilivyokuwa inaendeshwa na hoja mbali mbali kutoka upande wa mashtaka na upande wa utetezi katika mahakama kuu mjini pretoria Afrika kusini.

Pistorius amepatikana na hatia ya kuua bila ya kukusudia mwezi uliopita baada ya kusababisha kifo cha Reeva Steenkamp pia kutumia sdilaha kinyume cha sheria tukio ambalo alilifanya kwa nyakati tofauti na lile la mauaji.

Jaji Masipa alisema wakati wa kuendesha mwenendo mzima wa kesi hiyo alikuwa na washauri wawili waliokuwa wanamsaidia katika kupima kila hoja zilizokuwa zinatolewa na pande mbili,lakini uamuzi wa hukumu ni wakwake yeye binafsi.

Alisema wakati mwingine kupata hukumu stahiki ni vigumu sana tatizo ambalo linazikabili mahakama nyingi zinazoendesha makosa ya jinai.


Masipa amesema kabla ya hukumu,upande wa utetezi ulipeleka mashahidi wanne wakatoi upande wa mashtaka uliita wawili tu katika kuthibitisha mashtaka waliyoyawasilisha mbele ya mahakama.

Akielezea ushuhuda wa daktari wa saikolojia Dr Löre Hartzenberg alisema kuwa alikuwa akimtibu Pistorius tangu alipofanya mauaji hayo mwezi february mwaka jana.
.

Hartzenberg alisema mahakama haina budi kuzingatia maisha ambayo amekuwa nayo mara baada ya tukio,kwani alipoteza marafiki,hakuweza kuendelea na kazi yake,na alikuwa ameathirika kisaikolojia.

Masipa alisema shahidi wa pili  Joel Maringa, ambae ni afisa ustawi wa jamii alipendekeza Pistorius angekuwa kwenye kifungo cha ndani lakini nyumbani kwake kwa miaka mitatu na kufanya kazi za kijamii kwa masaa yasiyopungua 16 kwa mwezi.

Meneja wa Pistorius Peet van Zyl, alikuwa ni shahidi wa tatu aligusua kuhusu matembezi ya hisani aliyopanga kuyafanya kuhusu kazi aliyokuwa anaifanya.

Ushahidi wa Van Zyl ulisema kwamba kabla hajamuua mpenzi wake kwa risasi,Pistorius alikuwa anaheshimika kama mwanamichezo mahiri ulimwenguni,amabae alitumia muda na pesa zake katika mambo mengi ya msingi.

Kwa mujibu wa  Van Zyl, amesema fursa ya pistorius kushiriki kwenye mambo yote hayo imesimamishwa tangu kifo Steenkamp

Shahidi wa nne ambae pia ni afisa ustawi wa jamii Annette Vergeer, ambae alitumia muda mwingi kuelezea hali mbaya na tete ya magereza ilivyo nchini humo.

Ameiambia mahakama kuwa jela za nchini humu hazikidhi mahitaji maalum ya Pistorius kulingana na hali yake.

Kwa upande wa mashahidi wa mashtaka dhidi ya Pistorius wa kwanza alikuwa ni binamu yake marehemu Steenkamp Kim Martin,ambae alielezea kwa undani kazi za mwanamitindo huyo marehemu pamoja na maisha yake binafsi yalivyokuwa.


Martin aliiambia mahakama jinsi Steenkamp alivyokuwa karibu saana na wazazi wake,Barry na June na aliwasaidia sana kifedha na walikuwa wakimtegemea kwa kila kitu.Jaji Masipa alibaini jinsi gani Martin alivyokutana na Pistorius kwa mara ya kwanza mwezi mmoja kabla ya kifo cha Steenkamp.Martin alikumbusha mahakama kuhusu taharuki iliyoikumba familia yao baada ya kupata taarifa ya kifo cha ndugu yao.

Alisema hali ya afya ya baba mzazi wa Steenkamp, Barry ilikuwa mbaya kwani alikuwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha mwanae.

Shahidi wa mwisho kwa upande wa mashtaka alikuwa ni kaimu mkurudenzi wa taifa idara huduma urekebishaji tabia Zac Modise alisema mfumo wa jela za nchi hiyo ni mzuri na unaweza kumhifadhi Pistorius.


Jaji Masipa aligusia namna upande wa utetezi ulivyotoa hoja kuwa Pistorius asiende jela kwa kuwa anahitaji msaada wa matibabau ya kisaikolojia na akakubaliana na hoja ya shahidi wa mashitaka bwana Modes kuwa huduma za aina hiyo zinapatikana na mwanariadha huyo anaruhusiwa kumpeleka daktari wake huko jela akamtibie.

alisema hata wanawake wajawazito ni kundi ambalo lina mazingira magumu sana kwenye jamii,na walikuwa wanakwenda jela na idara za amgereza ziliweza kuwahudumia vyema,hivyo haitakuwa vyema kwa sheria iwatazame kwa umuhimu wa kipekee watu wenye pesa na maarufu huku upande mwingine wa watu masikini waachwe.

Masipa anaamini kwamba upande wa utetezi umeegemea sana katika hoja zake kuhusu hali ya ulemavu aliyokuwa nayo Pistorius,lakini akasema ukiyaangalia maisha ya Pistorius hasa ya kazi yake alikuwa anashindana pia na watu wazima na alikuwa anashinda.

alisema hukumu yake imepangwa kuonyesha hali halisi ya Pistorius,kuwa aliweza kubadili mtazamo hasi wa watu dhidi ya ulemavu ana aliwavutia wengi hasa vijana,amesema jambo hili halitapuuzwa kamwe litaheshimiwa na kubaki kuwa hivyo japo meneja wake alisema akifungwa haya mambo yote aliyokuwa anafanya kwenye jamaii yatasimama.

Masipa anaamini  Pistorius anajutia kwa kile alichokifanya kutokana na ushahidi kwamba  alijaribu kuwatafuta wanafamilia wa Steenkamp kwa siri na kuwaomba radhi.


Baadae alimuamrisha Pistorius kusimama kisha akamhukumu miaka mitano jela kwa kuua bila kukusudia na miaka mitatu kwa kosa la pili ila ataitumikia yote kwa pamoja na miaka miwili inaanza sasa akiwa jela.

Pistorius baada ya hukumu aliweza kuwapa mikono baadhi ya wanafamilia wake kabla ya kupanda karandinga kwenda jela.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...