Tuesday, February 17, 2015

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 13 ASIMIKWA RASMI KUWA CHIFU WA WAHEHE

Mwanafunzi wa darasa la saba Adam Abdul Sapi Mkwawa(13) ametawazwa rasmi kuwa chifu wa kabila la wahehe kufuatia kifo cha baba yake mzazi Abdul Sapi Mkwawa(66).

Rais Jakaya Kikwete alikuwa ni mmoja kati ya watu waliohudhuria maziko ya Chifu Abdul Sapi Mkwawa katika kijiji cha Kalenga mkoani Iringa na baadae kushuhudia kusimikwa kwa chifu huyo mpya wa kabila la wahehe Adam.

 Kusimikwa kwa mtoto huyo anayesoma katika shule ya msingi Highland iliyopo mkoani Iringa kutasubiri hadi atakapotimiza miaka 20 ndiyo ataanza kutumikia wadhifa huo wa uchifu ambapo kwa sasa wadhifa huo utashikiliwa kwa muda na mdogo wa marehemu Salehe hadi hapo Adam atakapotimiza umri huo(20).
Chifu mpya wa kabila la wahehe Adam Abdul Sapi Mkwawa

Rais Jakaya Kikwete akimfariji Chief Adam Abdul Sapi Mkwawa
Wazee wz kimila wakimsimika Adam Abdul Sapi Mkwawa kuwa chifu mpya wa kabila la wahehe siku mbili baada ya kifo cha baba yake Abdul Adam Sapi Mkwawa aliyekuwa chifu wa kabila hilo


RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA CHIFU ABDU MFWIMI ADAM MKWAWA KATIKA KIJIJI CHA KARENGA IRINGA FEBRUARI 16, 20155
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini katika kitabu cha maomborezo baada ya kuwasili kushiriki mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa katika  Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.
7
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.
3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji  Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili (14), wakati wa mazishi ya baba yake aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa  katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga  Februari 16, 2015
9dhdh
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa   katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.

Wednesday, February 11, 2015

JENGO LA GHOROFA 2 LIMETEKETEA NA MOTO JIJINI DAR

KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIWA KAZINIKUJITAHIDI KUZIMA MOTO ULIOTOKEA KATIKA MAKUTANO YA BARABARA YA LIIBYA NA MSIKITI KATIKA YA JIJIKIKOISI CHA KUZIMA MOTO WAKIWA KAZINI KUZIMA MOTO ULIOTOKEALEO


JENGO LILILOUMGUA MOTO

WAFANYAKAZI WA KIKOSI CHA ZIMAMOTO

KAMANDA SULEIMAN KOVAAKIWA KATIKAA ENEO LA TUKIO LA MOTO


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...