Wednesday, April 17, 2013

BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki mkongwe wa taarab nchini tanzania FATUMA BINTI BARAKA maarufu kwa jina la kisanii Bi KIDUDE,amefariki dunia leo saa sita mchana visiwani Zanzibar eneo la bububu.




AKIONYESHA UMAHIRI WA KUPIGA NGOMA

DJ MACKAY WA EAST AFRICA RADIO AKISALIMIANA NA BI KIDUDE ENZI ZA UHAI WAKE

picha hapo juu kwa hisani ya matokeo blog,inamuonyesha bi kidude enzi za ujana wake na ingine akiwa uzeeni

Tuesday, April 16, 2013

MUNGU ANAJUA KUUMBA NA AKAWAPA UPENDO,TUKIWAIGA TUTAFIKA MBALI KATIKA MAHUSIANO

NIPENDE NIKUPENDE HAHAHAAA

MOTO WATEKETEZA MALI KATIKA JENGO LA SHIRIKA LA NYUMBA JIJINI DAR LEO

MOSHI UNAOKEKANA KATIKA MOJA YA SEHEMU YA MKAZI MMOJA AMBAE AMEPANGA KATIKA NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA JIJINI DAR

Moto umeteketeza vitu mbali mbali vilivyokuwemo katika ghorofa alilokuwa anaishi mpangaji mmoja wa shirika la nyumba la Taifa NHC.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema walishangaa kuona moshi mkubwa ukitoka katika madirisha ya nyumba hiyo ndipo wakaanza harakati za kuuzima.
Watoto wa mpangaji huyo wanasema walikuwa wawili tu nyumbani wakati huo ambapo mtoto wa kiume anasema allikuwa anafua na dada yake alikuwa anafanya usafi wa nyumba ndipo wakashtuka kuona moshi mkubwa katika chumba cha dada zake.
Hata hivyo kikosi cha zimamoto kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo licha ya kuwa uliteketeza sehemu kubwa ya sehemu iliyokuwa inaungua

SPIKA ATOA AGIZO KWA WABUNGE WANAOTUMIA LUGHA YA MATUSI NDANI YA BUNGE KUTOLEWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE NA ASKARI

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU MASUALA MBALI MBALI YANAYOJIRI BUNGENI.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Anne Makinda amesema kutokana na tabia ya baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi wakati wa vikao vya Bunge basi ataawaamuru askari wa Bunge kumtoa nje mbunge yeyote atakaetenda kosa hilo.
Mh Makinda amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo kufuatia jana baadhi ya wabunge kutumia lugha ambazo zimetafsiriwa kuwa ni za matusi na hazifai kutumika ndani ya Bunge hilo tukufu.
Jana Mbunge wa kondoa Mh Juma Nkamia alimwambia Mbunge wa mbeya mjini kuwa awe na adabu na kwamba hazungumzi na mbwa bali na mwenye mbwa hali iliyofanya baadhi ya wabunge kuomba muongozo wa kiti kwani walitafsiri kama wao ni mbwa,pia mbunge waIringa mjini Mh Peter Msigwa aliponukuu moja kati ya vipengele vya vitabu vitakatifu kuwa na kutumia neno la MPUMBAVU.

Monday, April 15, 2013

MAKAMU WA RAIS DR MOHAMMED GHARIB BILAL NA VIONGOZI WENGINE WASHIRIKI KUMUAGA MEJA GENERALI MAKAME RASHID

MAKAMU WA RAIS DR BILAL AKIANDIKA KWENYE KITABU CHA RAMBI RAMBI
MAKAMU WA RAIS AKITOA HESHIMA MBELE YA JENEZA LA MEJA GENERALI MAKAME RASHID
MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA GENERALI  DAVIS MWAMUNYANGE,MKUU WA JESHI LA POLISI SAID MWEMA NA MKUU WA JESHI LA MAGEREZA
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA,MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA DAVIS MWAMUNYANGE ,MAKAMU WA RAIS DR BILAL NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI ALHAJ ALI HASSAN MWINYI(PICHA ZOTE KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO.COM)

PICHA ZA AJALI YA NDEGE ILIYOMUUA BOB SAMBEKE MFANYABISHARA MAARUFU MKOANI KILIMANJARO

HILI NI ENEO AMBALO NDEGE ILIANGUKIA NA NI KM 1 KUTOKA KATIKA NJIA YA KURUKA NA KUTUA NDEGE

MABAKI YA NDEGE ALIYOPOTEZA MAISHA YA BOB SAMBEKE

HALI HALISI YA ENEO LA AJALI

PANYA ANAEGUNDUA MABOMU AFRIKA



                           'Panya mwokozi wa maisha'
Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.

Friday, April 12, 2013

MWIGULU NCHEMBA ADAI KUWA NA USHAHIDI WA KUTOSHA KUHUSU SHUTUMA ZA UGAIDI DHIDI CHADEMA

MH MWIGULU NCHEMBA (MB) IRAMBA  MAGHARIBI
Mbunge wa Iramba magharibi mh MWIGULU NCHEMBA amesema bungeni kuwa yuko tayari kutoa ushahidi mahala popote kuthibitisha mipango ya chama cha demokrasia na maendeleo ya kuteka na kuua na kutaka chama hicho kisiisingizie Idara ya Usalama wa Taifa wala jeshi la polisi.

Akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu,amesema ana ushahidi wa kutosha juu ya mipango na utekelezaji wa mipango hiyo inayofanywa na baadhi ya wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.

Mara baada ya mbunge huyo wa Iramba magharibi kuzungumza,akasimama mbunge wa Mbulu mh MUSTAPHA AKUNAY akitumia kanuni  ya bunge ya 68 kifungu cha pili ambacho kinamkataza mbunge kuzungumzia suala lililoko mahakamani na kuomba muongozo wa spika.

Mbunge wa Singida mh TUNDU LISU kwa upande wake amelishutumu jeshi la polisi kwa kupanga ugaidi kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa na kisha kuwabambikizia kesi baadhi ya watu.
Kutokana na malumbano hayo,spika wa Bunge  Mh ANNA MAKINDA alilazimika kuwataka wabunge kuacha kuyazungumzia au kuyajadili mambo ambayo yako mahakamani,jambo lililopingwa vikali na baadhi ya wabunge,hivyo akaliacha suala hilo lijadiliwe

WANAHABARI WAWILI NA AFISA UHAMIAJI WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI HANDENI

MAREHEM HUSSEIN SEMDOE MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI ALIYEFARIKI KWENYE AJALI
WAANDISHI wa habari wawili pamoja na Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo majira ya saa nne asubuhi nje kidogo ya Mji wa Handeni. Waliofariki dunia ni Hussein Semdoe  mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Hamis Bwanga wa Radio Uhuru na Abood pamoja na Mariam Hassan ambaye ni Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifo vya marehemu hao. Mkuu  huyo wa Wilaya hiyo amesema ajali hiyo imetokea wakiwa kwenye msafara kuelekea Ndolwa kupanda miti.

Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo, Muhingo alisema gari lililopata ajali ni la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, STJ 4673 ambalo ndilo lililokuwa likitumiwa na Ofisa Uhamiaji, Hassan pamoja na wanahabari hao.
Akizungumzia mazingira ya ajali alisema ajali imetokea baada ya gari hilo kupasuka tairi la nyuma likiwa kwenye mwendo kisha kupoteza uelekeo na kuanguka. “Baada ya kupoteza uelekeo lili binuka kando ya barabara na marehemu wote walitupwa nje ya gari na kuangukia mawe hivyo kupoteza maisha, wawili walifia papo hapo na mmoja baadaye,” alisema Muhingo.

Alisema dereva pekee ndiye aliyenusurika katika ajali hiyo na amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya Handeni. “…Dereva naye alirushwa nje wakati wa ajali pamoja na marehemu wote, lakini yeye aliangukia juu ya kichaka hivyo kutoumia sana,” alisem kama wenzake.

Alisema msiba huo ni mkubwa kwa Wilaya ya Handeni kwani wamepoteza wachapakazi na watu muhimu katika mchakato wa maendeleo ya wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Wilaya ya Handeni imepoteza wanahabari kwa asilimia 100, kwani waandishi hao ndiyo waliokuwa wanahabari pekee wilayani hapo. “…Msiba huu ni mkubwa si kwa tasnia ya wanahabari pekee bali hata kwa juhudi za maendeleo ya Wilaya ya Handeni, tulikuwa tukizunguka nao katika shughuli mbalimbali hapa Wilayani hivyo ni pigo kubwa,” alisema muhingo.
Aliongeza kwa upande wa Ofisa Uhamiaji, marehemu Hassan alikuwa ni mpambanaji mkubwa wa wahamiaji
haramu katika wilaya Hiyo, na hivi karibuni alifanikiwa kuwakamata takribani wahamiaji 70 eneo hilo, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwa nguvu kazi ya wilaya. Alisema tayari miili ya marehemu wawili (Mdoe na Hassan) imechukuliwa kwa shughuli za mazishi na mmoja bado (Bwanga) unasubiri wanandugu kutoka Handeni.(HABARI NA PICHA KWA HISANI YA THE HABARI.COM)

Tuesday, April 9, 2013

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA RAIS MPYA WA KENYA UHURU KENYATTA


RAIS MSTAAFU WA KENYA MZEE MWAI KIBAKI AKIAGWA KWA HESHIMA
UHURU KENYATTA AKILA KIAPO CHA KUWA RAIS WA NNE WA KENYA

RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AKIWAPUNGIA WANANCHI MARA BAADA YA KUAPISHWA
RAIS MSTAAFU MZEE MWAI KIBAKI AKIZUNGUKA UWANJA KUWAAGA WAKENYA MARA BAADA YA KUWATUMIKIA KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI

RAIS UHURU KENYATTA AKIKABIDHIWA FIMBO IKIWA NI ISHARA KUWA SASA AMEKABIDHIWA RASMI JUKUMU LA KUIONGOZA KENYA

AKIINYANYUA JUU FIMBO HIYO KUTOKA KWA RAIS MSTAAFU MWAI KIBAKI
UMATI WA WANANCHI WALIOHUDHURIA UWANJANI HAPO KUSHUHUDIA RAIS WAO MPYA AKIAPISHWA

RAIS WA KENYA UHURU KENNYATTA AKILA KIAPO
KIAPO CHA KUWA RAIS

AKIWAPUNGIA WAKENYA KW FURAHA NA BASHASHA NYINGI

Sunday, April 7, 2013

VIJANA WA IPP WALIVYOUNGANA NA WANAHABARI MBALIMBALI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KATIKA KUADHIMISHA MEDIA DAY LEADERS CLUB

AMINA CHENGO NA REHEMA NYAMAKA
MAULID KAMBAYA NA KIDUKU
TIMOTHY CHELULA TC NA MAULID KAMBAYA WAKIYARUDI MANGOMA MEDIA DAY
WACHA WEE........TC
HAPO SASA HAPOOOOOO.....TC
VIJANA WA IPP
,AULID KAMBAYA NA AMINA CHENGO KATIKA POZZZ
HAWA WAZEE NAO WALIKUWEPO,PIUS PAUL KATIKATI,KULIA NI DAMDELI NDUNGURU NA AMINA CHENGO PEMBENI YA PIUS
MZEE WA DAKIKA 45,SULEIMAN SEMUNYU AKIWA HOOOI BAADA YA MCHEZO ALOKUWA ANACHEZA HA HAAA....

Saturday, April 6, 2013

JAMBAZI LAKAMATWA NA RISASI 1,200 MKOANI KIGOMA

KAMANDA WA POLISI MKOANI KIGOMA FRAISER KASHAI AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI RISASI 1200 ALIZOKAMATWA NAZO MTU MMOJA ANAETUHUMIWA KUWA JAMBAZI

KAMANDA WA POLISI MKOANI KIGOMA FRAISER KASHAI AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI BUNDUKI AINA YA GOBORE AMBALO  NI MOJA KATI YA SILAHA ALIZOKAMATWA NAZO MTUHUMIWA HUYO WA UJAMBAZI

KAMANDA KASHAI AKIONYESHA BUNDUKI ALOKUTWA NAYO MTUHUMIWA HUYO WA UJAMBAZI

KAMANDA KASHAI AKIONYESHA NOTI BANDIA ZENYE THAMANI YA TSH 200,000 ALIZOKUTWA NAZO MTUHUMIWA HUYO(PICHA KWA HISANI YA MCHOMEBLOG.COM)

Monday, April 1, 2013

WATU 18 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORAM HUKO MOSHONO JIJINI ARUSHA

Watu zaidi ya 18 wanahofiwa wamepoteza maisha baada ya kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Moram huko Moshono jijini Arusha.

 Waliokubwa na mkasa huo ni pamoja na wale waliokuwa wanapakia Moram hizo katika malori mawili aina fuso na lingine lenye uzito wa zaidi ya tani 18 ambayo yalifunikwa kabisa na kifusi hicho

Kazi ya uokoaji na utafutaji ya waliopoteza maisha ilikuwa  ikifanywa na askari wa JWTZ wakishirikiana na wadau mbalimbali.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku tatu tu tangu jengo la ghorofa 16 kuporomoka katika makutano ya mitaa ya Indira Gandhi na Z anaki jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine 17 kujeruhiwa.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH GODBLESS LEMA AKIWASILI ENEO LA TUKIO

WANANCHI WAKIWA ENEO LA TUKIO KUSHUDIA HALI HALISI YA TUKIO HILO LA KUSIKITISHA

ASKARI WA JWTZ WAKISHIRIKIANA NA WANANCHI KUUBEBA MWILI WA DEREVA WA MOJA YA MALORI YALIYOFUKIWA KABISA NA KIFUSI ENEO LA TUKIO

HALI HALISI ENEO LA TUKIO

WASAMALIA WEMA WAKIMBEBA MMOJA WA WANANCHI AMBAO WALIPOTEZA FAHAMU BAADA YA KUONA MWILI WA RAFIKI YAKE UKITOLEWA KWENYE KIFUSI

WENGINE WALISHINDWA KABISA KUZUIA HISIA ZAO NA KUANGUA VILIO  BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUJIONEA HALI HALISI

SHUGHULI YA UOKOAJI IKIENDELEA

KULIA KABISA NI MOJA YA MALORI YALIYOFUNIKWA NA KIFUSI HICHO NA LINGINE HALIONEKANI KABISA NA KAZI YA KUYAFUKUA HAPO INAENDELEA.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA LUKEMUSICFACTORY.BLOGSPOT.COM)

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...