Friday, June 21, 2013

MAPOKEZI YA DAVID BECKHAM CHINA YASABABISHA WATU KUKANYAGANA NA BAADHI WAUMIA VIBAYA WAKIWEMO MAAFISA USALAMAM


MAAFISA USALAMA WAKIWA KATIKA WAKATI MGUMU KUWAZUIA MASHABIKI

AFISA USALAMA ALIEJERUHIWA




ANGALIA KILA MMOJA ALIINUA SIMU YAKE JAPO APATE PICHA INGEKUWA BONGO SIJUI KAMA KUNA SIMU INGESALIMIKA HAPO

UMATI UKIHANGAIKA JAPO KUPATA PICHA

WENGINE WALIONA BORA WAGUSE HATA GARI TU




Watu watano wamejeruhiwa vibaya katika mapokezi ya David Beckham nchini China baada ya umati mkubwa kujitokeza kumlaki na kutaka japo kumgusa.Licha ya kuustaafu lakini bado mashabiki wake walifurika katika jiji la Shanghai hali iliyosababisha watu watano kujeruhiwa akiwemo polisi.
Katika ratiba yake hiyo jana Beckham alikuwa atembelee chuo kikuu cha Shanghai cha Tongji.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid alikuwa akutane na wachezaji wa timu ya chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba kuitangaza ligi kuu ya China imayptambulika kama Chinese Super League.
Hata hivyo kufuatia umati mkubwa kujitokeza kwa lengo la kumlaki kiungo huyo wa zamani wa England kumesababisha zoezi hilo kushindikana ambapo baadae aliomba radhi kwa mashabiki wake hao kupitia mtandao wa kijamii wa facebook na Sina Weibo.
Maafisa Usalama walishindwa kuzuia vurugu hizo ambapo walikuwa wakisonga mbele licha ya kuwekewa kizuizi.
Katika ujumbe wake Beckham amenukuliwa akisema"Samahani sikuweza kutokea uwanjani kuiona timu kwani ilikuwa ni vigumu kupenya kati kati ya mashabiki.Nimesikia kulikuwepo na watu waliojeruhiwa,Nina matumaini wako salama na nawatakia heri wapone haraka''
Takriban watu 1000 inaaminika walikuwa wanataka japo kumkaribia Beckham na polisi wamethibitisha kuwa maafisa wake watatu walijeruhiwa katika vurugu hizo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 38 alistaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuisaidia Paris-Saint Germain kutwaa taji la ligi ya Ufaransa maarufu kama league 1.

MBUNGE WA KASULU MJINI MH MOSES MACHALI APIGWA MKOANI DODOMA





MBUNGE WA KASULU MJINI MH MOSES MACHALI
Habari   kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana , tukio hilo limetokea jana jioni  wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.

Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo. 


Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.

.(HABARI KWA HISANI YA  LEWIS MBONDE BLOG)



Tuesday, June 18, 2013

SAFARI YA MWISHO YA LANGA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

Jeneza lenye mwili Wa Langa
AddM







 j

Picha kwa hisani ya Saleh Ali na Global Publishers

Sunday, June 16, 2013

KUFUATIA MLIPUKO WA JANA,TUME YA UCHAGUZI IMEAHIRISHA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA TANO ZA JIJI LA ARUSHA

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA
Tume ya taifa ya uchaguzi imeahirisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata tano za jiji la Arusha uliopangwa kufanyika hii leo,kufuatia tukio la mlipuko uliotokea jana huko Mkoani Arusha katika mkutano wa kuhitimisha kampeni kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,na kusababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya na mlipuko huo.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii kwa njia ya simu kutoka Zanzibar,mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema uchaguzi huo utafanyika June 30 mwaka huu na kwamba hali hiyo itawapa nafasi vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha zaidi ulinzi siku ya uchaguzi huo.

Saturday, June 15, 2013

HALI ILIVYOKUWA KWENYE SHOW YA LADY JAY DEE NA ILE YA MWANA FA

MAMBO YALIKUWA HIVI

MLIPUKO MWENGINE ARUSHA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA NA KUJERUHI

DAMU ZIKITAPAKAA ENEO LA TUKIO

MAJERUHI WAKIWA CHINI

MFUKO UNAOSEMEKANA NDIYO ULIYOKUWA NA HICHO KITU KILICHOSABABISHA MLIPUKO

MAJERUHI WAKIWA HOSPITALI

MAJERUHI WAKIPATA HUDUMA

Friday, June 14, 2013

TARATIBU ZA MAZISHI YA LANGA

marehemu Langa


akihojiwa katiaka studio za East africa Radio wakati anaitambulisha track yake mpya
Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hospitali ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.
Langa amefariki dunia jana katika hospitali ya taifa muhimbili baada ya kuugua malaria kali na alifariki dunia saa 11 jioni katika hospitali hiyo akitokea katika hospitali ya Dr Mvungi iliyopo kinondoni jijini Dar es Salaam.
Langa alianza kutambulika katika medani ya muziki wa hip hop mwaka 2004 akiibuka katika kundi la WAKILISHA lililopatikana katika mashindano ya Coca cola pop stars likiundwa na wasanii wengine Witness pamoja na Shaa.

Tuesday, June 4, 2013

ABSALOM KIBANDA AREJEA NCHINI NA KULAKIWA NA MAMIA YA WANAHABARI

WANAHABARI WAKIWA NA MABANGO




AKILIA KWA BAADA YA KUREJEA TENA NYUMBANI
AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI WENZAKE(PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)

BAADA ya kuwa Afrika Kusini  majuma kadhaa kwa ajili ya matibabu, Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya New Habari 2006 na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, hatimaye  amerejea nyumbani leo mchana na  kulakiwa na mamia ya waandishi wa habari.

HATIMAE MWILI WA ALBERT MANGWEA WAPOKELEWA DAR


MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA DAR WAKIBEBA JENEZA LENYE MWILI WA NGWEA MARA BAADA YA KUWASILI KWENYE UWANJA WA NDEGE JK NYERERE UKITOKEA AFRIKA KUSINI

PICHA YA JUU WATU WAKIJIPANGA KUUPOKEA MWILI WA NGWEA CHINI NI GARI ILIYOBEBA MWILI HUO NA KUUPELEKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AMBAPO KESHO UTAAGWA KWENYE VIWANJA VYA LEADERS













Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...