Friday, July 5, 2013

WALIMU 25 WALALAMIKIA FEDHA ZA UHAMISHO

  
 
Na  YEREMIAS  NGERANGERA----NAMTUMBO
                                                                               
 Wakati     serikali   ikiagiza   kuwa  uhamisho  wa  walimu  uendane na fedha za kugarimia uhamisho, kuepuka mzigo wa madeni kwa serikali , bado halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma iliwahamisha walimu 25 mwezi januari bila kuwalipa fedha zao mpaka sasa.. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya walimu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe kwa ajili ya kuhofia ajira zao walisema kuwa walipata barua za uhamisho mwezi januari lakini chakushangazi waliambiwa walipoti vituo v ipya vya kazi  wakati taratibu za malipo yao zinaandaliwa. 

( Mimi toka Januari mwaka huu sijafundisha naendelea kusubiri fedha za uhamisho au gari la kubebea mizigo yangu Kutoka halmashauri na huu ni mwezi wa sita toka nipate barua ya uhamisho) alisema mwalimu mmoja. Baadhi ya walimu walidiriki kwenda kwa watu binafsi kwenda kukopa fedha kwa ajili ya kugharimia uhamisho huo kwa mategemeo ya kupata fedha toka kwa mwajiri kwa ajili ya kulipia madeni hayo wapo katika hali ya wasiwasi katika  vituo vyao vya kazi kutokana na kero za watu wanaowadai walimu hao. Hata hivyo  kuna baadhi ya walimu ambao hawakutaka kuingia hasara hiyo waliendelea kukaa nyumbani bila kufundisha kwa miezi sita mpaka shule zinafungwa w akisubiri fedha za uhamisho.

 Katibu wa chama cha walimu wilayani Namtumbo bwana Werner Mhagama aliwapongeza walimu walioendelea kusubiri fedha za uhamisho mara tu baada ya kwenda kuripoti kituo kipya na kurudi kituo cha awali kusubiri fedha za uhamisho au gari la kubebea mizigo yao kwa madai kuwa walimu hao wapo sahihi kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma. Afisa elimu wa wilaya ya Namtumbo bwana Loberto Mbilinyi alikiri kuwepo kwa madai ya walimu hao na ku kusema kuwa madai hayo yanalipwa kwa awamu na baadhi ya walimu walisha lipwa. Mkurugenzi wa wilaya hiyo bwana Mohamed Maje alisema kuwa uhamisho wa walimu hao ulipita katika vikao halali kwa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na bajeti ya malipo kwa walimu hao ilishafanyika bali pametokea na uchelewaji wa fedha kutoka serikalini..

Thursday, July 4, 2013

CAPITAL RADIO NDANI YA VIWANJA VYA SABA SABA


MTANGAZAJI WA CAPITAL RADIO AMRY MASSARE AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WATU WALIOTEMBELEA SABASABA

AMRY MASSARE AKIWAKILISHA CAPITAL RADIO SABASABA

WANAUME WILAYANI TUNDURU WAWASHITAKI WAKE ZAO HAKI ZA BINADAMU

Picha siyo ya tukio halisi
Na Stevie Chindiye,Tunduru
WANAUME Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamewaomba viongozi wa Mtandao wa kutetea haki za Binadamu (Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition) ili uwasaidie kuwapatia mafunzo ya utetezi ili kuwasaidi kujikinga na vitendo vya ukandamizaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na wake zao.

Ombi hilo limetolewa na Viongozi wa mashirika yasiyo kuwa ya Kiserikali Wilayani humo wakati wakiongea na Viongozi wa Mtandao huo walipotembelea katika Ofisi za Mtandao wa Mashirika ya Kijamii Wilayani Tunduru (MATU) zilizopo Mjini hapo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Wafanyabiashara wa Mazao ya Chakula Tunduru (WAMANATU) Athuman Idd Milanzi ndiye aliyeanza kuvunja ukimya huo kwa kuwaeleza viongozi hao kuwa wanawake wa makabila ya Wayao wamekuwa wakiwanyanyasa waume zao katika utoaji wa maamuzi mbalimbali yakiwemo ya kupeleka watoto wakike katika Unyago. 

Milanzi ambaye aliungwa mkono na Daimu Mnenga aliye kiwakilisha Chama cha Wazee na wastaafu Wilayani humo walidai kuwa pamoja na wake hao kuendesha tabia za ubabe huo pia waliwatuhumu kuwa wanawake hao wamekuwa kikwazo katika maendeleo ya ndoa zao kutokana na kutojali kuachika.

Wakifafanua maelezo hayo walisema kuwa kutokana na wanawake hao kujengeka katika kiburi hicho wakati mwingine wamekuwa hawawahusishi waume zao katika maandalizi ya kuwafunda Watoto wao wa kike hasa ikionekana mwanaume husika haungi mkono taratibu hizo na wakiwa wanadai kuwa mwanamke asiyechezwa hawezi kuishi vizuri na mume atakaye muoa.

Wakiongeaa kwa nyakati tofauti mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition) Bw. Onesmo Olengurumwa na Afisa Habari wa Mtandao huo Bw. Elias Mhegera ambao pamoja na mambo mengine waliwaahidi kuwapatia mafunzo hayo ambayo walidai kuwa yatawasaidia kujilinda na kutoa utetezi katika matukio ya aina hiyo.

WANANCHI SONGEA,NJOMBE WAILALAMIKIA SUMATRA

 
Na Amon Mtega ,Songea na Njombe.
 
WANANCHI wa tarafa ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma pamoja wananchi wa kata ya Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameilalamikia kitengo  cha mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Tanzania [SUMATRA]kwa kuto kuweka wazi bei halali ya viwango vya nauli katika maeneo ya vijijini hasa kutoka Madaba Songea  hadi Mavanga Ludewa.

 Wakiongea na demashonews kwa nyakati tofauti wananchi hao ambao hawakutaka majina yao yatanjwe gazetini walisema kuwa SUMATRA imeshindwa kuangalia matatizo ya nauli katika maeneo ya vijijini na kufanya wanamchi  kulipa nauli isiyo na kiwango stahiki hata pakiwa na umbali mdogo lakini nauli ni gharama kubwa.

 Wananchi hao waliyokuwepo kituo cha mabasi cha Madaba wakisubiri usafiri wa kuelekea kata ya Mavanga Ludewa walisema kuwa wanatozwa nauli ya Tsh 5,000 hadi Tsh 6,000 licha ya umbali wake kuwa  ni wa kilometa  44 huku barabara hiyo ikiwa imetengezwa kwa kiwango cha changarawe na inapitika vizuri .
 Wakielezea kiwango hicho cha nauli walisema kuwa wanashangazwa kuona bei  hiyo inalingana na umbali wa kutoka Songea mjini hadi Madaba ambapo umbali wake ni wa kilometa zaidi ya 120 na kutoka Njombe hadi Madaba nako umbali unakaribia kulingana kwa kilometa 120 lalkini nauli zake ni Tsh 5,000 tatizo kwenye kipande kidogo cha barabra kichounganisha wilaya ya Songea na Ludewa kuwa bei juu bila maelezo ya SUMATRA.
 Walisema kuwa kama SUMATRA imeweza kuweka bayana viwango vya nauli katika maeneo mbalimbali ya njia kwa kubandika nauli hizo kwenye magari iweje kwa baadhi ya barabara kushindwa kuwekewa vuwango sahihi vya nauli.
 Baadhi yao walitaka viongozi wa SUMATRA wanao wakilisha mikoa yao ya Njombe na Ruvuma wakutane ili waweze kulijadili suala hilo kwa kina hasa kwa kiongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa kuwa eneo lake la kutoka Madaba kuelekea Ludewa ni kubwa na  linaishia daraja la mto Luhuhu ambalo linalounganisha pande zote mbili.
 Kwa mjibu wa wananchi hao wamedai kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha maeneo hayo yanapatiwa huduma zinazostahiki kama barabara zinazopitika lakini baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kama mabasi wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi  na kuwahujumu wananchi kwa kuwapandishia nauli  licha barabara kuwa nzuri.
 Kwa upande wake afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoani Ruvuma Denis Daudi akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu amekiri kuwepo kutofanyiwa kazi kiwango hicho cha nauli kulingana na umbali hivyo ameomba wananchi hilo wapeleke barua ya malalamiko huku yakiwa yamembatanishwa na risiti zinazonyesha kiwango hicho.

 Gazeti hilo lilikuwa tayari kupeleka kieleezo cha risiti kwa kuwa nalo lilibaini hilo likiwa kwenye msafara huo lakini kiongozi huo alizidi kuomba ipelekwe kwa maandishi ili ifanyiwe kazi kwa haraka zaidi.

WAKAZI WA WILAYA YA MBINGA WAIOMBA SERIKALI KUWADHIBITI WAFANYABIASHARA WANAOWARUBUNI WAKULIMA

Wadau wa kilimo cha mahindi wakiwa katika hatuwa ya mwisho katika mavuno


Na Joyce Joliga 
 
WANANCHI wa wilaya ya  Mbinga mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuhakikisha inakomesha tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa mazao wasiowaaminifu ambao wanapita  kuwarubuni wakulima kwa kubadilishana chakula na simu kitu ambacho kinawasababishia hasara. 

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kunabaadhi ya wafanyabiashara za mazao ambao si waaminifu wamekuwa wakipita katika mashamba yao na kuwadanganya kwa kuwapelekea simu za bei raisi na kubadilishana nao kwa kuwapatia mahindi.
Mmoja wa wakulima hao Aidan Komba mkazi wa Matiri amesema amejikuta akitoa mahindi dumla mia sawa na kilo 400 za mahindi baada ya kupewa  simu na kuelezwa kuwa inathamani ya kiasi cha sh 450,000 kitu ambacho kumbe kilikuwa sahihi. 

“Tunaomba serikali itusaidie kuwadhibiti wafanyabiashara ambao wanapita katika maeneo ya mashambani kwa kuwarubuni wakulima kwa kubadilishana nao vitu vya anasa na kuchukua mazao yao kwani vitendo hivi vikiachiwa ni hatari na vitatusababishia njaa,”alisema 

Kwa upande wake Mariam Mahundi  mkazi wa Myangayanga Mbinga amesema, alifatwa na mmoja wa wafanyabiashara wa mazao nyumbani kwake  ambapo alimwomba ampatie dumla 30 za mahindi ambapo angempatia simu aina ya Tekno pamoja na memori naye alifanya hivyo na kukabidhiwa simu hiyo ambapo alipewa maelekezo aichaji masaa sita na alipomaliza kuchaji aliiwasha ikagoma kuwaka lakini tangu alipochukua simu hiyo haikufanya kazi na alipoipeleka kwa fundi iligundulika kuwa tayari ilikuwa imekufa na ilinunuliwa tu kava jipya.

Wednesday, July 3, 2013

CHINA WAKABIDHI UWANJA WA TAIFA LEO KWA SERIKALI YA TANZANIA


 Balozi wa China, Lu Youqung akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga na Balozi wa China, Lu Youqung wakati wa hafla ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa.
Balozi wa China, Lu Youqung  akimkabidhi ufunguo Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara kama ishara ya makabidhiano rasmi ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA RICHARD MWAIKENDA KAMANDA WA MATUKIO

MKE WA MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWATAKA WANAWAKE KUPENDANA,WAACHE KUSENGENYANA ILI WAWEZE KUSONGA MBELE KIMAENDELEO

Mama Anabu Mwambungu Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma


 Na Joyce Joliga,
WANAWAKE mkoani Ruvuma wameshauriwa kupendana, kushirikiana na kuacha tabia ya kusengenyana ili waweze kufanikiwa kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ili viweze kuwasaidia kuinua kipato chao na familia zao na wasikubali kugombanishwa .
Ushauri huo umetolewa jana na Mke wa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati akizindua rasmi kikundi cha wanawake wajasilimali  wanaojishugulisha na ufugaji wa kuku wa nyama na mayai cha JITIHADA GROUP kilichopo kata ya Lizabon Manispaa ya Songea.
Amesema,ili wanawake waweze kufanikiwa kimaendeleo wanapaswa kujenga moyo wa kupendana kwa dhati , kuaminiana na kushirikiana  na kuacha tabia ya kupigana majungu kitu  ambacho kimekuwa kikiua vikundi vingi vya wanawake .
Anabu ameongeza kuwa ,wanawake  wengi wamekuwa wakifanikiwa kuanzisha vikundi  ila vimekuwa havifiki mbali na kuvunjika kitu ambacho si kizuri hivyo amewataka wanawake kuwa makini na miradi wanayoaanzisha ikiwa ni pamoja na kushikamana ili waweze kujiletea maendeleo.
“Nawashauri wanawake wenzangu ,kikundi hiki tukiendeleze ili kiweze kutusaidia kujikwamua na umaskini kamwe tusikubali kugambanishwa na vijimajungu vidogo vidogo ,kwani  hiyo ndiyo sumu ya vikundi vingi ,mpendane, muaminiane ,mshirikiane na kuvumiliana na mtafika mbali , name nawaunga mkono nawachangia kiasi cha sh 200,000,”alisema Anabu Mwambungu.
Awali akisoma taarifa ya kikundi hicho Katibu wa Kikundi hicho Theresia Komba amesema,bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukosa mtaji  hali inayowafanya washindwe kuzalisha kwa wingi,pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiliamali hususani wa ufugaji bora.
Aidha, wamemwomba Mke wa Mkuu wa mkoa kuwasaidia ili waweze kupata mkopo pamoja na pembejeo za kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi na kujiongezea kipato.

PAROKO MSAIDIZI WA KANISA KATOLIKI LA MATOGORO AMEWATAKA WAUMINI WA KANISA HILO KUACHA TABIA YA UCHOYO

 

Picha na maktaba



Joyce Joliga,Songea 

WAUMINI wa kanisa katoliki Matogoro Manispaa ya Songea wameshauriwa kuacha uchoyo na badala yake  kujenga tabia ya kusaidiana wao kwa wao bila  kutegemea misaada toka kwa wafadhili wan je ya nchi kwani vitendo hivyo vimepitwa na wakati.

Ushauri huo umetolewa jana na Paroko msaidizi wa kanisa katoriki  la Matogoro Nicolas Mlelwa ambaye amesema,waumini hao wanapashwa kuacha mkono wa birika na wajifunze kusaidiana na kufanya mambo yao wao wenye bila kutegemea wafadhiri.

Amesema,anasikitishwa kuona waumini wa nyanda za juu kusini si watu wa kujitoa tofauti na majimbo mengine ambapo wamekuwa wakiwasaidiana wao kwa wao ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mapadri wao
“ Nawaomba waumini muache mkono wa birika, mjenge tabia ya kushirikiana na  muanze kujitegemea kwa kusaidiana nyinyi kwa nyinyi ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mapadri wenu kwani kuendelea  kutegemea wafadhili si kitu kizuri bali tuendelee kujitolea kwa moyo wa upendo ,”alisema

Aidha,amewataka waumini hao kuhakikisha wanachangia harambee ya kongamano la vijana wakatoriki ambalo linatarajiwa kufanyika mapema mwezi huu ambapo kiasi kinachotakiwa ni sh 8,000,000 ilikuweza kufanikisha maandalizi yote ya kongamano hilo ambalo litashirikisha vijana wa vyuo vikuu.

TIMU YA MAJIMAJI MKOANI RUVUMA YAPATA UONGOZI MPYA

  Mwenyikiti  wa timu ya  Maji Maji Humphery Millanzi aliyeibuka kidedea kwa ushindi mkubwa katika uchagui wa viongozi wa timu hiyo.
 ..........................
Na Amon Mtega  ,Songea.
TIMU ya majimaji ya wanalizombe mkoani Ruvuma jana imepata uongozi mpya utakao weza kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.
 
 Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ,Joseph Mapunda uliyofanyika katika ukumbi wa saccos ya walimu uliyopo mjini hapo alisema kuwa kwa nafasi ya mwenyekiti imechukuliwa na Humphery Millanzi kwa kura 89 huku mpinzani wake Mohamed  Issa alipata kura 30.
 
 Mapunda alisema kuwa kwa nafasi ya makamu mwenyekiti mgombea alikuwa ni John Nchimbi ambaye alikuwa mgombea  peke bila upinzani na kufanya apate kura za ndiyo 101huku kura 20 zilikuwa za hapana.
 
 Akifafanua katika nafasi za wajumbe watano alisema kuwa nafasi hizo ziliwaniwa na watu tisa waliyopatikana ni watano nao ni Hilda Kapinga alipata kura 102 Mohamed Matwika kura 99 John Kabisama kura 90 Kitwana  Mzee kura 84 na Salum Masamaki kura 74 .
  
 Aidha alisema kuwa kwa wajumbe walishindwa kupata nafasi hizo ni Joseph Mswila ambaye alipata kura 62 Robarti Mgowole kura 18 Said Mangwe kura 14 na Oddo Mbunda kura 50 huku idadi ya wapiga kura walikuwa 121.
   
 Kwa upande wake mwenyekiti aliyeshinda katika nafasi hiyo Hafrei Milanzi akiongea na chombo hiki alisema kuwa amepongeza ushindi huo huku akiwa ameahidi kushirikiana na wanachama wote wa timu ya majimaji pamoja na wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kusongambele kimchezo.

MCHUNGAJI MBEYA AFUNGWA MIAKA 30 KWA KOSA LA UBAKAJI

 MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi

   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela
  Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
  Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30
 Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
Habari ,Picha na Mbeya yetu Blog 

TAZAMA VIDEO YA WATOTO WALIOLELEWA NA MBWA BAADA YA MAMA YAO KUWATELEKEZA KWA ULEVI


VIDEO INAJIELEZA KILA KITU,MBWA ALIKUWA AKIWAPELEKA HADI SHULE NA KUWARUDISHA

Tuesday, July 2, 2013

OBAMA AONYESHA UMAHIRI KATIKA KUCHEZA NA MPIRA

RAIS BARACK OBAMA AKIONYESHA UMAHIRI WA KUSAKATA SOKA


RAIS KIKWETE AKIMFUATILIA KWA MAKINI RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA WAKATI AKICHEZA NA MPIRA KATIKA MITAMBO YA UMEME UBUNGO

1.........2.........3.....4....5.........HIZI ZINAITWA DANA DANA(picha kwa hisani ya blog ya jamii)

RAIS BARACK OBAMA AONDOKA NCHINI BAADA YA ZIARA YA SIKU MBILI

RAIS OBAMA AKIPANDA NDEGE NA MKEWE TAYARI KUONDOKA KUELEKEA MAREKANI






NDEGE YA RAIS OBAMA IKIENDA KWENYE SEHEMU YA KURUKA

RAIS BARACK OBAMA APANDA MTI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

AKIANGALIA NGOMA ZA KITAMADUNI

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMUELEZA JAMBO RAIS KIKWETE WAKATI AKIJIANDAA KUPANDA MTI

akipanda mti ikulu

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI APATA MAPOKEZI YA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM

MAKACHERO WA MAREKANI NA TANZANIA WAKIWA JUU YA PAA KATIKA UWANJA WA NDEGE WAKATI WA MAPOKEZI YA RAIS BARAK OBAMA

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MGENI WAKE



RAIS BARACK OBAMA AKIKAGUA KIKOSI CHA JESHI LA TANZANIA

AKIFURAHIA NGOMA



GARI ILIYOMCHUKUA RAIS BARACK OBAMA KWENDA IKULU

WAKIPOKEA MAUA KUTOKA KWA WATOTO KAZIMINA MINJA NA JOSEPH MASASI

WAKITEREMKA KWENYE AIR FORCE ONE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...