Saturday, August 3, 2013

MBEYA BADO HAWAKOMI NA MAJANGA YA MOTO: BAADA YA LORI LA MAFUTA KUPINDUKA MBALIZI ,WANANCHI WAPIGANA VIKUMBO KUGOMBEA MAFUTA .


 Lori lenye namba za usajili  T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia

Lori  likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo


YALE YALE!!! Wananchi  wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka 
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka

Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji 
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali

Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
Tingo wa Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.


Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.



DR. SLAA AFUNGUA KONGAMANO LA UCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akifungua kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Chama cha Convervative, Rolf Aagaaro-Svenevosen na Katibu Mkuu wa chama hicho mrengo wa Vijana. 
 Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakinunua skafu, kofia za chama hicho wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama hicho mrengo wa Vijana wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam

                                                             (Picha na Francis Dande)

BALOZI SEIF ALI IDD AKUTANA NA WANA CCM MKOA WA MAGHARIBI

Wajumbe wa Halmashauri ya CCM  wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama wakimsikiliza Mlezi wa Mkoa huo Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akikaribishwa rasmi kuwa mlezi wa Mkoa huo katika Mkutano uliofanyika katika Tawi la CCM Kiembe Samaki.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya CCM wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama katika mkutano maalum wa kukaribishwa kwake kuwa Mlezi wa Mkoa Magharibi Kichama.

Balozi Seif akikabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kununulia Mabati kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi la CCM la Kilima Matange liliopo Jimbo la Muyuni kutekeleza ahadi aliyoitoa Mwezi Machi mwaka huu wakati wa ziara yake Mkoa Kusini Unguja.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ




DR SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI KWA AJILI YA UJENZI WA MADRASA HUKO UNGUJA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya kuweka jiwe la Msingi madrasatul Tarblat Islamia iliyopo Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na Wananchi na wanafunzi wa madrasatul Tarblat Islamia, ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya kuwawekea jiwe la msingi madrasa hiyo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Baadhi ya Wanafunzi wa madrasatul Tarblat Islamia,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza nao baada ya kuwawekea jiwe la msingi madrsa yao leo huko Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja,leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]




Friday, August 2, 2013

HATIMAE WANYAMA PORI HAI WAFIKISHWA KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO NANE NANE JIJINI MBEYA

 Fisi akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Simba Jike akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Simba Dume akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Waandishi wakipata ufafanuzi wa maonesho ya Nanenane  mwaka huu 2013 katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TASO Mbeya.

***********
BAADA ya kiu ya Muda mrefu kwa Wakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya kutokuwaona Wanyama hai kwa zaidi ya miaka 30, hatimaye Maonesho ya Nanenane Mwaka huu yatakayofanyika Kikanda Mkoani Mbeya Wameletwa.
Wanyama hao wanaoletwa kwa Udhamini wa Kampuni ya Pepsi na MLM International Vision (T) Ltd kutoka katika Kampuni inayohusika na Wanyama hai ya Bahari Zoo kutoka Jijini Dar Es Salaam itatoa fursa kwa Wakazi wa Kanda hii kujionea kwa ukaribu na kumaliza kiu ya Muda mrefu.
Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Leo katika Viwanja vya John Mwakangale Uyole Jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Bahari Zoo Willy Kusaga amesema kwa utafiti wake amebaini kuwa mara ya mwisho wanyama kama Simba, Chui, Chatu, Mbega, Fisi na wengine walikuja Mbeya Mwaka 1977.
Amesema yeye binafsi anajisikia fahari kuona Wakazi wa Mbeya walivyoitikia ujio wa Wanyama hao na kwamba utalii wa Ndani utatangazwa vilivyo na kuhamasisha Wananchi kuanza kupenda kutembelea vivutio vilivyojirani na makazi yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (TASO) Kanda ya Mbeya, Noel Nkoswe alisema maandalizi ya Nanenane Mwaka huu ni makubwa kutokana na watu kuham,asika na waoneshaji kuongezeka tofauti na maonesho ya nyuma.
Amesema hamasa kubwa imetokana na kiu ya kuwaona wanyama kutokana na kutokuwepo kwa muda mrefu na wengine kukosa fursa ya kutembelea mbuga za Wanyama zilizozoeleka ikiwa ni sababu za uchumi na umbali.
Ameongeza kuwa sababu nyingine itakayoleta hamasa ya maonesho ya Mwaka huu ni fursa ya kuandaa maonesho ya Kitaifa yaliyohamishiwa Dodoma kwa Mwaka wa Sita Mfululizo hivyo kuwafanya Wananchi kuamini Mwaka huu kufanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Mwenyekiti huyo amesema katika Uzinduzi wa Nanenane Kwa Kanda hii utafanywa na Waziri Wa Uchukuzi, Dr. Harisson Mwakyembe ambapo Siku zitakazofuata kila Mkuu wa Mkoa atapangiwa siku yake kwa ajili ya Mkoa husika kuonesha shughuli za Wakulima wake.

Alizitaja siku hizo kuwa ni Agosti 2, Mwaka huu kufanywa na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya huku Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Agosti 3, Mkoa wa Rukwa, Agosti 4 mkoa wa Iringa, Agosti 5 Mkoa wa Njombe, Agosti 6 Mkoa wa Ruvuma na Agosti 7 utakuwa ni Mkoa wa Katavi.
Habari/Picha  na Mbeya yetu

Thursday, August 1, 2013

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA KUONDOA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WATOTO WA KIKE


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa rasmi kwenye mkutano wa "High Level Group" na Dr. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS Regional Support Team kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Gaborone nchini Botswana tarehe 31 Julai 2013.


 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akifunga rasmi mkutano wa High Level Group uliokuwa unafanyika kwenye hoteli ya Lasmore nchini Botswana tarehe 31 Julai 2013.
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Profesa Alaphia Wright, Mwakilishi wa UNESCO kwenye nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa High Level Group ulikuwa ukifanyika jijini Gaborone nchini Botswana tarehe 31 Julai 2013.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wakisoma jarida linalochapishwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, huku wakiendelea na mkutano.

Na Anna Nkinda- Gaborone,  Botswana
1/8/2013 Jamii imetakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa  hakuna unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike pia inawalinda ili wasiingie katika mazingira hatarishi yatakayowapelekea kupata  kupata maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi (VVU) .
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kamati maalum ya viongozi wanaoshughulikia huduma na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Jumuia ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kikanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika  katika Hoteli ya Lansmore Masa Square iliyopo mjini Gabarone nchini Botswana.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema  huwa anajisikia uchungu pale anaposikia  kuwa mtoto wa kike amebakwa au amefanyiwa ukatili wa kijinsia na kuiomba jamii nzima iweze kumsaidia na kumkomboa mwanamke.
“Kama jamii yetu ya nchi za kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika itaungana kwa pamoja na kuamua  kumsaidia mtoto wa kike itawezekana  kwani hata kama watoto hawa wakipata huduma bora ya afya  bila ya kuwapatiwa elimu hakuna jambo la maana watakalolifanya  kwakuwa  watakuwa na afya bora  lakini watakosa kujiamini kwani hawana elimu”, alisema Mama Kikwete.
Akiongelea kuhusu Taasisi ya WAMA alisema kitaaluma yeye ni mwalimu na wakati anafundisha aliona changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike na pale alipoanzisha taasisi hiyo aliamua kuwasaidia watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ambao wamekosa nafasi ya kwenda shule ili nao waweze kusoma kama watoto wengine.
Mama Kikwete alisema, “ Tuna shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mfano ya WAMA-Nakayama ambayo ina jumla ya wanafunzi 325 wa kidato cha kwanza hadi cha nne pia  Taasisi ya WAMA inawagharamia masomo wanafunzi wasichana 300 ambao wanasoma shule mbalimbali za Sekondari katika mikoa yote ya Tanzania.
Alimalizia kwa kuiziomba nchi wanachama wa EAC na SADC kutunga na kufuata sera na sheria zitakazomlinda mtoto wa kike kwa kufanya hivyo ataepukana na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakwaji, udhalilishwaji, kutopewa huduma bora za afya na elimu.
Mkutano huo wa siku mbili uliandaliwa  na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupamba na Ukimwi (UNAIDS) , UNFPA, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF), Shirika la Chakula Duniani (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lengo kuu likiwa ni  kuhakikisha kuwa vijana wote wanapata elimu kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia na stadi za maisha jambo ambalo litawasaidia kufahamu zaidi  ugonjwa wa Ukimwi.SOURCE:IPSHA MEDIA

SIMALENGA NA NEEMA WAIAGA RASMI KAMBI YA MAKAPELA

MR &MRS SIMON SIMALENGA


SIMON SIMALENGA NA MKEWE BI NEEMA



Kambi ya Wasinii wa Filamu na Maigizo pamoja na Kambi ya Waanahabari Makapela Tanzania imepata pigo kubwa baada ya Mwanachama wake Nguli, Simon Simalenga kuamua kuiaga kambi hiyo na kuingia rasmi katika Kambi Tawala ya Wanandoa baada ya kufunga Ndoa na Bi. Neema Inana. Wawili hao wameamua kuiga kambi hiyo ya Upinzani katika mahusiano leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza jijini Dar es Salaam na baade katika tafrija kubwa unayofanyika usiku  wa Julai 27, 2013 katika ukumbi qa Grande Hall uliopo ndani ya Hoteli ya Picolo Beach Mbezi(PICHA NA FATHER KIDEVU)

MAAJABU YA NGORONGORO,MCHANGA UNAOTEMBEA KWA KUHAMA HAMA BILA UPEPO

KIBAO KINACHOELEKEZA MCHANGA HUO ULIPO

MCHAANGA UNAVYOONEKANA UKIHAMA

NJIA YA KUELEKEA HUKO

WATALII WAKIWA JUU YA MCHANGA

MCHANGA UNAOHAMA BAADA YA MUDA UNAENDA SEHEM NYINGINE

ENEO LINAVYOONEKANA

WATALII WAKISHIKA MCHANGA HUO

WATALII WAKIWA JUU YA MCHANGA


TANZANIA NA THAILAND ZATILIANA SAINI MKATABA WA UHIFADHI WA MALI ASILI NA UTALII

.
WAZIRI MKUU WA THAILAND BI YINGLUCK SHINAWATRA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI
 Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na utalii imetiliana saini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika uhifadhi wa mali asili na utalii na serikali ya Thailand ikiongozwa na waziri mkuu wake  Mh.  Yingluck Shinawatra.
Makubaliano hayo yamesasainiwa na waziri wa mali asili na utalii wa Tanzania kwa kumuhusisha naibu waziri  mkuu  wa Thailand Plodprasop Suraswad, mbele ya waziri  mkuu  huyo wa  Thailand kwa kuelezwa kuwa ni mwanzo mzuri katika kukuza sekta ya utalii nchini na kuchangia ukuaji wa uchumi. Akizungumza baada ya kutiliana saini katika mkataba huo,waziri wa mali asili na utalii Mh. Balozi Khamis  Kagasheki, amesema mbali na kukuza uchumi na utalii wa Tanzania, lakini pia makubaliano hayo yatasaidia kukuza kipato cha mtanzania kwani sekta ya utalii inachangia kwa asilimia 17 katika pato la taifa..
Kwa upande wake waziri wa uwekezaji na uwezeshaji nchini Mh Mary Nagu,amesema ujio wa waziri mkuu huyo wa Thailand hapa nchini kutawapa  fursa wawekezaji  wa  Thailand kuja kuwekeza nchini  katika sekta  mbalimbali.
Ziara hii ya siku moja ya waziri mkuu wa Thailand katika hifadhi ya taifa ya Serengeti ambao ni miongoni  mwa maajabu saba ya Afrika,imepokelewa kwa furaha kubwa na viongozi wa mkoa wa Mara na wadau  wa sekta ya utalii mkoani Mara.

RAIA 9 NA ASKARI WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA PEMBE ZA NDOVU

 Watu tisa wakiwemo wawili waliokuwa askari polisi wa kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Pwani wakituhumiwa kwa makosa mawili ya kukutwa na nyara za serikali na kushiriki katika kosa la kuhujumu uchumi kinyume cha sheria.
 
Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2013 inaunguruma mbele ya hakimu mkazi nwandamizi mfawidhi wa mahakama hiyo Mh, Bahati Ndeserua,ambapo wakili wa serikali Bi Cecilia Shelly akisoma hati ya mashtaka mbele ya mahakama hiyo amewataja washtakiwa hao kuwa ni Koplo Senga Idd Nyembo,Pc issa Mtama,wengine ni Prosper Mareto,Seif Kadro,Said Kadro,wakazi wa panga la mwingireza vikumburu Kisarawe,Ramadhan Athmani,Musa Ali dereva mkazi wa Kinondoni studio ambaye kazi yake ni mgambo. Mahakama ikaambiwa kuwa,washtakiwa wote kwa pamoja wametenda makosa hayo Julai 28 mwaka huu katika kituo cha ukaguzi cha kauzeni na kijiji cha vikumburu Kisarawe mkoani Pwani,ambapo imedaiwa katika shtaka la kwanza washtakiwa hao walikutwa na nyara za serikali ambazo ni viapnde 70 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 306 vyenye thaamni ya shilingi milioni 850 na miatano mali ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyama pori nchini. Katika shtaka la pili wakili wa serikali akaiambia mahakama kuwa,washtakiwa hao kwa pamoja walishiriki katika kosa la kuhujumu uchumi kinyume na sheria na kwamba wakiwa katika kijiji cha Vikumburu Kisarawe mkoani  Pwani kwa nia ya kutenda uovu walikutwa na nyara za serikali ambavyo ni vipande vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 306.5 vyenye thamani ya shilingi milioni 850 mali ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyama pori nchini. Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa  wote kwa pamoja hawakutakiwa kujibu lolote kisheria kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria ya kusikiliza kesi za aina hiyo na wamerudishwa rumande hadi Agosti 14, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena na upelelezi wa kesi mahakama imesema bado haujakamilika.

UCHAGUZI ZIMBABWE NANI KUIBUKA KIDEDEA

Raia wa Zimbabwe wamepiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe akiwa na miaka 89 amesema atang'atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa katika uchaguzi huo.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.

Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw.Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.

Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika{AU}, Kanda ya Kusini mwa Afrika{SADC} na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.

Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo.Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura leo ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.

Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.
 
Hivi ndivyo Watu wengi walivyojitokeza kupiga kura kiasi cha kuilazimisha Tume ya uchaguzi kuongeza muda hadi pale waliokuwa kwenye vituo wamalizike.
Mgombea wa MDC Bw Morgan Tsvangirai
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...