Friday, September 6, 2013

PICHA ZA VURUGU BUNGENI DODOMA JANA

 
 Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini 
 Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
 Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni 
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo 
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo. hata hivyo   Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
  Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
 Mbunge  wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa  na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya  hivyo na Naibu Spika wa  Bunge, Job Ndugai 
 Mbunge wa Mbeya Mjini  akizuiwa na wabunge  wa CHADEMA ili asiambane na polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
PICHA ZOTE NA BLOG YA JAMII

Wednesday, September 4, 2013

JWTZ YAKAMATA WANAJESHI WANNE WA RWANDA WALIOKUWA KONGO WAKIWASAIDIA WAASI WA M23

SKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Kongo (Monusco), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamedai kuwakamata maofisa wanne wa jeshi la Rwanda, katika mapigano ya wiki iliyopita nchini Kongo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa askari aliyepo ndani ya kikosi cha JWTZ huko nchini Kongo, alisema maofisa hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizi za sasa zinakuja wakati ambapo kumekuwa na madai ya muda mrefu, ambayo yamekuwa yakitolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani kwamba, Rwanda imekuwa ikiwasaidia waasi wa kundi la M-23.

Pamoja na kwamba Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo, kitendo chake cha wiki iliyopita cha kuamua kupeleka bataliani mbili zenye wanajeshi 1,700 ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa ni kishindo cha vikosi vya Umoja wa Mataifa vyenye jukumu la kulinda amani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa kirasilimali, kinatokana na waasi wa M23 kupata kipigo kikali.

Chanzo chetu hicho kutoka uwanja wa mapambano nchini Kongo, kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao wa Jeshi la Rwanda waliwakamata katika mapigano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja, ambayo tayari yamewakimbiza waasi wa M23.

“Askari wa Rwanda tuliowakamata, ni maofisa wa ngazi za juu kabisa jeshini, tena walikuwa na sare za jeshi hilo… walikuwa wakiwasaidia hao M23, lakini kwa kuwa sisi tulikuwa makini tulifanikiwa kuwatandika hadi tukawakamata,” kilisema chanzo chetu hicho.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika zinaeleza kwamba, hatua hiyo ya kuwakamata maofisa hao pamoja na kuondoka kwa waasi wa kikundi cha M23, imefanikisha kushinda vita hiyo kwa zaidi ya asilimia 95.

Mtoa taarifa wetu huyo kutoka Kongo, ameliambia gazeti hili kuwa, tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baada ya kufanikisha hatua hiyo.

MAPIGANO YALIVYOKUWA
Akielezea namna walivyofanikiwa kutoa kibano kwa M23, askari huyo kwanza alikiri kuwa mapigano yalikuwa makali, kutokana na kikundi hicho cha waasi kusheheni vifaa vya kisasa na msaada wanaoupata kutoka Serikali ya Rwanda.

“Kwa kweli mapigano yalikuwa makali sana, lakini kwa upande wetu sisi tulikuwa tunajiamini kutokana na vifaa ambavyo pia ni vya kisasa hususani ikizingatiwa jeshi letu ni la Umoja wa Mataifa.

“Tulifanikiwa kuteka ngome yao kwa kutumia mbinu mbalimbali za kijeshi na kuwafanya watawanyike kabisa katika eneo hilo.

“Ngome yao ilikuwa ni kubwa sana, ina ukubwa wa zaidi ya viwanja vitatu vya mpira… na katika eneo hilo kulikuwa kumesheheni vifaa vyao vya kivita, kama makombora, mafuta, mizinga pamoja na vifaa vingine kama magari na baadhi ya silaha nyingine kubwa kubwa za kivita,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, sasa hali ni shwari ndani ya nchi hiyo ya Kongo.

“Baada ya kuwasambaratisha sasa wamekimbilia eneo moja lililopo karibu na mpaka wa Uganda. Kama unavyofahamu hawa jamaa walikuwa wakitumia mbinu za kujihami kwa kurusha mabomu katika eneo la Rwanda, ili ionekane kuwa sisi tumerusha,” alisema askari huyo.

“Lakini tunamshukuru Mungu, tupo salama ingawa tumempoteza askari mmoja na askari wengine wenzetu wa Tanzania ambao ni wanne, wamepata majeraha kidogo lakini wanaendelea vizuri.

“Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu waendelee kutuombea turudi salama, kwa sababu kazi sasa imeshakamilika,” alisema askari huyo.

Juhudi za gazeti hili kumpata msemaji wa Monusco, Luteni Kanali Prosper Basse kuzungumzia juu ya taarifa hizo, zilishindikana.

Taarifa ambazo tumezinasa kwa siku kadhaa sasa kutoka uwanja wa mapambano na ambazo zimegusa vichwa kadhaa vya habari zinaeleza kuwa, brigedia maalumu ya vikosi vya UN yenye dhamana ya kujibu mashambulizi (FIB), katikati ya wiki iliyopita iliendesha operesheni kubwa iliyoharibu kabisa ngome muhimu ya waasi wa M23, hali inayotajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ndiyo iliyoishtua Serikali ya Rwanda ambayo inatuhumiwa kuwasaidia waasi hao.

Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa, FIB ambayo inaundwa na wanajeshi wapatao 3,000 kutoka Tanzania na Afrika Kusini chini ya Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limejizatiti kwa zana za kisasa za kivita zikiwamo mizinga na helikopta za kivita.

Taarifa kutoka mashariki ya Kongo zinaeleza kwamba, mashambulizi dhidi ya waasi wa M23 ambao hivi karibuni waliripotiwa kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Tanzania aliye katika jeshi la UN, yamesababisha waasi hao kukimbilia katika eneo la milima lililopo umbali wa kilomita tano kutoka mji mdogo wa Kanyaruchinya Mashariki mwa Goma.

M23 WAZUNGUMZA
MTANZANIA Jumatano jana lilifanikiwa kuzungumza na Rais wa M23, Bertrand Bisiimwa, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza sababu za vikosi vyao kuondoka katika ngome yao ya kivita sambamba na taarifa za kuibuka kwa mapigano mapya ya hivi karibuni.

Katika hilo, Bisiimwa alikiri kikosi chake kurudi nyuma siku nne zilizopita, huku akiitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ilitokana na wao kutotaka vita baada ya majeshi ya Kongo kuanza kuwarushia mabomu kwenye kambi yao.

“Sisi tuliamua kurudi nyuma tusiendeshe vita, tunajua aliyetupa hayo mabomu ambayo yalifika mpaka Rwanda, tunaitaka Umoja ya Mataifa ikuje ifanye uchunguzi wake…wakuje waangalie vifaa yetu waone kama inaweza kurusha mabomu hadi Rwanda,” alisema.

Hata hivyo, Bisiimwa alisema kuwa sio kweli kama majeshi ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na JWTZ yaliwasambaratisha katika ngome yao.

“Sio kweli walikuja Kanyaruchina tukiwa tumeondoka na tuliondoka si kwa sababu ya kuwakimbia, hapana tulitaka UN wafanye uchunguzi yake juu ya kurushwa mabomu, kwa sababu wanataka kutuvalisha mambo ya uongo mchafu,” alisema Bisiimwa.

Bisiimwa alijigamba kuwa majeshi ya Kongo hayawawezi na kwamba walikwishawashindwa, lakini akakiri kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaweza kuwaondoa.

“Ninakiri hiyo kwa sababu Umoja wa Mataifa inaweza kututoa, unajua inakuwa na nguvu ya hatari,” alisema Bisiimwa kwa Kiswahili cha tabu.

CHANZO-Mtanzania

TAZAMA PICHA SITA ZA LORI LILILOANGUKA KARIBU KABISA NA KITUO CHA MABASI CHA MOROGORO

Add caption





MWANAFUZI ALIESHINDA NA KUONGOZA TOKA DARASA LA KWANZA HADI LA SABA


Mwanafunzi Zainab Aboubakary Mlawa wa shule ya msingi St Magreth iliyopo kimara jijini Dar essalaam akiwa na vyeti vyake  alivyotunukiwa katika mahafali ya darasa la saba  baada ya kufauru katika masomo yote toka alipoanza darasa la kwanza katika shule hiyo mpaka alipofika darasa  la saba na kutunukiwa vyeti vya  nafasi za kwanza kwa kila darasa anapoingia anafanya vizuri na kuongoza masomo yote toka alipoanza darasa la kwanza mpaka anamaliza la saba.
 

Baba mzazi wa mwanafunzi Zainab,  Aboubakary Mlawa  akilimsha keki mtoto wake mpendwa  mara baada ya kunukiwa vyeti katika mahafali ya kumalizika darasa la saba mtoto zainab  ambayo alipata zawadi zote za kitaaluma na nidhamu kwa wanafunzi wote wa darasa la saba toka alipoanza shule miaka saba iliyopita

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALLY IDDI AZINDUA KITUO KIPYA CHA AFYA UNGUJA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikifungua rasmi kituo cha Afya cha Sheia ya Chuini kilichopo Wilaya ya Magharibi.

Balozi Seif akifurahia kitendo cha Mtoto Ikram Silima akipimwa uzito na Watendaji wa Kituo cha Afya cha Chuini mara baada ya kukizindua rasmi ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia nusu karne.

Bibi Lny Paul na Mumewe ambaye hayupo Pichani akisisitiza umuhimu wa wananchi kujenga tabia ya kutunza mazingira katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Chuini uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Bwana Paul Jonson mmoja wa wahisani wakubwa waliochangia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chuini akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima iliyotolewa na wananchi wa Chuini kama ishara ya kumbu kumbu kutokana na mchango wake huo.
Uongozi wa Shehia zinazobahatika kupata wawekezaji katika maeneo yao hapa nchini umetakiwa kujenga uhusiano mwema na wawekezaji hao kwa lengo la kupata maendeleo ya haraka yatakayosaidia kustawisha hali za wananachi wao.


Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hafla fupi ya kuzindua Kituo kipya cha Afya katika Kijiji cha Chuini Wilaya ya Magharibi ikiwa ni mwanzoni mwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 sawa na nusu Karne.


Balozi Seif alisema Uzoefu unaonyesha kuwa wawekezaji wengi hapa nchini hupendelea kuchangia maendeleo ya wananchi lakini mara nyingi hukatishwa tamaa kwa matumizi mabaya ya misaada wanayoitoa kunaofanywa na baadhi ya Viongozi wa shehia  kwa kushirikiana na watendaji wabadhirifu wa Taasisi za Serikali na zile zisizokuwa za Kiserikali. 


Alionya kwamba tabia hiyo mbaya inarejesha nyuma maendeleo ya Taifa na wananchi kwa jumla, hivyo hakuna budi kwa wenye hulka hiyo kuachana nayo mara moja.


“ Mara nyingi na baadhi ya maeneo wawekezaji wetu hukatishwa tamaa na udokozi wa baadhi ya wenzetu ambao hujisahau bila ya  kuzingatiwa kuwa wawekezaji hao ni wageni wetu tuliyokwenda kuwatafuta ili waje kuwekeza nchini mwetu “. Alifafanua Balozi Seif.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wananchi na viongozi wa Shehia ya Chuini kwa kuwepuka matumizi mabaya ya misaada ya wahisani jambo ambalo limesaidia kuwaletea maendeleo ya haraka.


    Balozi Seif alifahamisha kwamba wananchi wa Chuini wamefanikia

    kuwa na uadilifu mkubwa uliopelekea kulinda na kuheshimu michango

    inayotolewa na wahisani, wadau na washirika wa maendeleo ndani na

    nje ya Nchi.


Akizungumzia huduma za afya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameiasa jamii kujenga utamaduni wa kuvitumia vituo vya afya katika kujipatia huduma bora za afya pamoja na kupata taaluma ya kinga ya maradhi tofauti.



Alisema tabia ya baadhi ya watu wakiumwa kufikiria wamerogwa na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji haina tija kwao na  kwa kiasi kikubwa inaweza  kuhatarisha maisha yao.


“ Tunapougua ni vyema tukakimbilia vituoni ili kutibiwa. Tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kila mara, bila ya sababu za msingi tuziache mara moja “. Alisisitiza Balozi Seif.


Aliwahakikishia Wananchi wa Shehia ya Chuini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake, itajitahidi kuona dawa muhimu kwa ajili ya wananchi hao zinapatikana kituoni hapo pamoja na wafanyakazi wa kutosha.


Kuhusu hali ya ukimwi hapa Nchini Balozi Seif alisema maambukizi ya maradhi hayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi badala ya kupungua kama inavyoonekana sehemu nyengine duniani.


Alieleza kwamba Jitihada za Serikali za kupambana na ukimwi hazitaweza kuleta mafanikio bila ya wananchi kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya maambukizi na maradhi hayo ya Ukimwi. 


Alitahadharisha kuwa ukimwi hauna tiba, hivyo wananchi wajitahidi kujiepusha na vitendo vyote vinavyochangia kusambaa kwa ukimwi hapa nchini, kama vile uzinifu, ngono zembe pamoja na  utumiaji wa dawa za kulevya.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika kuunga mkono juhudi za wananchi hao wa Chuini ameahidi kuchangia matofali elfu moja kwa ajili ya kuongeza nguvu za ujenzi wa jengo jipya la Madaktyari wa Kituo hicho cha afya cha Shehia hiyo.


Katika risala yao wananchi hao wa shehia ya Chuini iliyosomwa na katibu wa Kamati ya maendeleo wa shehia hiyo Bibi Narie Mbaraka Kaite alisema Kituo hicho kilichogharimu jumla ya shilingi Milioni 28,000,000/- kitakuwa na huduma zote za msingi.


Bibi Narie alisema uongozi na wananachi wa shehia hiyo hivi sasa wamejikita katika ujenzi wa nyumba ya familia mbili ya daktari ikiwa katika hatua ya msingi ili jamii ya kijiji hicho ifikie hatua ya kupata huduma za afya wakati wote.


Katibu huyo wa kamati ya maendeleo ya shehia ya Chuini kwa niaba ya wananachi na viongozi wa shehia hiyo amewashukuru wafadhili, wahisani na washirika wa maendeleo waliosaidia michango iliyokamilisha ujenzi wa Kituo hicho cha afya.


Naye Mwakilishi wa wahisani na wafadhili wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya Bwana Paul Jonson na Mkewe Bibi LNY wakitoa salamu zao walisema Kituo hicho kitasaidia ukombozi wa kiafya kwa wananchi walio wengi katika shehia hiyo.


Bwana Paul aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara inayohusika na masuala ya Afya kukipatria vifaa vya kazi kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora na za kisasa.


Bibi Lny Paul akaisisitiza jamii ya wazanzibari kujenga tabia ya kupenda kulinda na kutunza mazingira ili visiwa vya Zanzibar viendelee kuwa na haiba nzuri.


Kituo cha Afya cha Chuini kitakuwa kikitoa huduma zote za msingi ikiwemo mama wajawazito, watoto, maradhi ya kawaida, ushauri nasaha pamoja namaabara.
 

WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU WATIWA MBARONI MKOANI TANGA

WAHABESHI WALIOKAMATWA  NA UHAMIAJI MKOANI TANGA


MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO

WATANZANIA WALIOKAMATWA WAKIWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU KUSHOTO NI ALHAJ MIRAJ SHIMBO NA KULIA NI HALFAN MWAVESO


OFISI YA UHAMIAJI MKOA WA TANGA

ALHAJ MIRAJI SHIMBO MMOJA WA WATUHUMIWA


HALFAN MWAVESO MTUHUMIWA WA USAFIRISHAJI WAHAMIAJI HARAMU AKIANGUA KILIO WAKTI AKITOA MAELEZO

AFISA UHAMIAJI WA MKOA WA TANGA BW SIXTUS NYAKI

KILIO KIKIENDELEA

KIKISHIKA KASI KILIO

Idara ya uhamiaji mkoani Tanga imewatia mbaroni watanzania wawili wanaodaiwa kufanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na Somalia kwenda nje ya nchi.

afisa uhamiaji mkoa wa Tanga  bwana Sixtus Nyaki amewataja watanzania hao kuwa ni Alhaj Miraj Shimbo na Halfan Mwaveso ambao walikuwa na wahamiaji wawili raia wa Ethiopia waliokamatwa wilayani Muheza baada ya kuingia katika bandari bubu zilizopo jirani na eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Kwa upande wa watuhumiwa walipohojiwa mara baada ya kutiwa mbaroni na askari wa uhamiaji mmoja wapo aliyefahamika kwa jina la Mwaveso aliyekuwa anaangua kilio wakati akihojiwa na mwandishi wa blog hii,amesema kuwa hausiki kabisa na biashara hii na amemsukumia lawama bosi wake kuwa ndiye aliyekuwa anawasafirisha baada ya yeye kuombwa akawakatie tiketi ya basi wahabeshi hao hali ya kuwa yeye hawafahamu.

Inadaiwa wasafirishaji wa wahamiaji haramu hupata kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wahamiaji hao ili waweze kuwasafirisha na mara nyingi wamekuwa wakiwasafirisha kwa njia ya malori hali ambayo imeshasababisha vifo vya wahamiaji haramu wengi sana kutokana na kukosa hewa na wengine wengi kukamatwa.

HOMA YA PAMBANO LA MAYWEATHER NA CANELO YAZIDI KUPANDA

Mpambano wa kufa mtu unasubiriwa kwa hamu kati ya bondia asiyepigika Floyd Mayweather na Canelo Alvarez.

Mamilioni ya mashabiki wa mchezo huu na washabiki wa mabondia hawa wamekua na shauku kubwa siku ya pambano hilo lifike huku kukiwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa mabondia hawa.

Mpambano wao unatarajiwa kufanyika wiki ijayo September 14 pale MGM GRAND,sehemu ambayo mapambano mengi makubwa ya ndondi huwa yanafanyika.

Tusubiri ni nani ataibuka kidedea siku hiyo,ni MAYWEATHER au CANELO 



Floyd Mayweather kushoto na   Canelo Alvarez wakitunishiana misuli

Tuesday, September 3, 2013

ANGALIA VIDEO MPYA YA DIAMOND-MY NUMBER 1

KASHFA YALIKUMBA JESHI LA POLISI TENA....... CAMERA ZA CCTV ZAZIMWA KURUHUSU UJAMBAZI


SIKU chache baada ya tukio la wizi mkubwa wa fedha katika Benki ya Habibu mjini Dar es Salaam, siri nzito zimeanza kuvuja kuwa polisi wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo kwa kuhujumu kamera za usalama za CCTV zinazomilikiwa na jeshi hilo. 
 
Katika tukio hilo, watu wanaodaiwa kuwa majambazi walipora dola za Marekani 20,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 32 za Tanzania.

Katika tukio hilo, Polisi Mkoa wa Ilala inamshikilia askari mmoja kwa kosa la kuhusika katika tukio hilo kutokana na kushindwa kuchukua hatua za haraka wakati tukio linatokea.

Habari za uhakika kutokana ndani ya jeshi hilo, zinasema siku ya tukio polisi waliokuwa zamu kuongoza mitambo hiyo, kwa namna moja au nyingine wanadaiwa kufanya hujuma hiyo, kwa lengo la kupoteza mawasiliano na maeneo mengi ya polisi.

Chanzo chetu hicho, kiliongeza kuwa siku ya tukio eneo lote la mzunguko wa barabara ya Uhuru na maeneo ya jirani na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), sehemu zote hazikuwa na huduma ya kamera za usalama, jambo ambalo si la kawaida kutokea.

“Hatua iliyofikia sasa ni mbaya, huwezi amini siku ya tukio kamera za CCTV zinazotumiwa na polisi zilizimwa kabisa, kitendo hiki kilisababisha polisi makao makuu wasijue nini kinachoendelea pale.

“Ndiyo maana utaona kuna askari mmoja anashikiliwa katika tukio lile, haiwezekani kituo kikuu kishindwe kubaini uwapo wa tukio hili, wakati kuna mawasiliano ya kutosha, umefika muda wa kulisafisha jeshi letu kwa kasi,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho, kilisema mitambo ya kamera hizo, ilizinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa mwaka 2004 na imekuwa ikifanya kazi bila matatizo yoyote.

“Nimekuwapo hapa tangu mwaka 2004, kamera hizi zilipozinduliwa rasmi na hazijawahi kuharibika hata siku moja, iwe siku ya tukio zisifanye kazi,” kilihoji chanzo chetu.

Askari aliyekamatwa katika tukio hilo, anadaiwa anafanya kazi katika kituo cha Oysterbay Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alithibitisha kukamatwa kwa askari huyo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa na MTANZANIA jana, alisema ameipokea taarifa hiyo na wanaifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

“Taarifa hii tumeipokea, tunaifanyia kazi haraka sana ili kupata ukweli, naomba tuwe na subira,” alisema kwa kifupi Kamishna Kova.

Alisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba watu waliokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya dola
.CHANZO MTANZANIA.

WAFANYAKAZI WA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI STRABAG,WAFUNGIWA NJE NA UONGOZI LICHA YA MKUU WA MKOA WA DSM KUWATAKA KURUDI KAZINI LEO

WAFANYAKAZI HAO WAKIWA NJE YA OFISI HIZO WASIJUE LA KUFANYA BAADA YA UONGOZI KUWAFUNGIA




MIJADALA YA HAPA NA PALE IKIENDELEA YA NINI KIFANYIKE



NYUSO ZILIZOPOTEZA MATUMAINI (picha na ujiji raha)
Mgomo wa wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam ya Strabag,umeingia katika sura nyingine leo baada ya  uongozi wa kampuni hiyo kuwafungia wafanyakazi nje na kuwazuia kuendelea na kazi licha ya tamko la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick kuwataka kuendelea na kazi.

MWANAMKE ALAZWA HOSPITALI AKIJARIBU KUTOA TUMBONI FEDHA DOLA 5,000 ZA MAREKANI ALIZOZIMEZA

Christie Black
Mwanamke wa kimarekani Christie Black(43),amelazwa hiospitalini baada ya kuumia vibaya kooni na tumbaoni wakati akijaribu  kutoa kiasi kikubwa cha fedha alizozimeza kwa kutumia ufagio wa kusafishie choo.

Christie mkazi wa Bulls Gap katika jimbo la tennessee alipata majuraja hayo baada ya kushindwa kutoa dola za kimarekani 5,000, sawa na shilingi milioni nane za Tanzania alizomuibia mpenzi wake Bobby Gulley.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi wa jimbo hilo,Christie alichukua uamuzi huo ili kukwepa kugawana fedha hizo na mpenzi wake huyo baada ya kutengana.

Taarifa zinasema mara baada ya kujiingiza ufagio huo kupitia mdomoni,mwanamke huyo alisikia maumivu makali kutokana na michubuko iliyosababisha atokwe na damu nyingi sana mfululizo.

Inasemekana hali yake inaendelea vizuri hospitalini hapo baada ya kuwwahishwa na kupatiwa matibabu kwa haraka.

Ppolisi wanasema walipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa mpenzi wa Christie,Bobby Gulley ambae alikwenda kushitaki kuibiwa fedha hizo na baada ya upelelezi walimbaini mwanamke huyo ndiye muhusika wakati yuko taabani hospitali.

Christie alipoulizwa kuhusu sababu ya kumeza kiasi hicho kikubwa cha fedha,alisema alikuwa anataka zikamsaidie kimaisha baada ya kupata taarifa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa na mpango wa kumuacha.

Mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya wizi wa fedha na mara atakapopata nafuu atapandishwa kwa pilato ili kujibu mashitaka yake hayo.

Sunday, September 1, 2013

BREAKING NEWSSSSS!!!!!!!!!!!!!!

PICHA NA MAKTABA IKIONYESHA MOJA KATI YA AJALI ZILIZOWAHI KUTOKEA
WATU WATATU WAMEPOTEZA MAISHA NA WENGINE ZAIDI YA WATANO WAMEJERUHIWA VIBAYA BAADA YA BASI DOGO AINA YA HIACE KUGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MIZIGO LILILOKUWA LINAFANYA SAFARI KUTOKA ARUSHA KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA KIJIJI CHA MKATA MKOANI TANGA.

MWANDISHI WA BLOG HII ALIEPO ENEO LA TUKIO ANASEMA MASHUHUDA AKIWEMO KONDAKTA WA BASI HILO DOGO WANASEMA CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA DEREVA LA HIACE NA ALIKUWA AMELEWA KWA KUWA ALIKUNYWA POMBE KABLA HAJAANZA SAFARI NA KABLA YA KUANZA SAFARI ALITAKA KUENDESHA YEYE KUTOKANA NA DEREVA KUWA KATIKA HALI YA ULEVI LAKINI DEREVA HUYO ALING'ANG'ANIA KUENDESHA HADI ILIPOTOKEA AJALI.

MAJERUHI WAMELAZWA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA MKATA KWA HUDUMA YA KWANZA KWANI WAMEUMIA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUKATIKA VIUNGO VYAO VYA MWILI AKIWEMO DEREVA WA HIACE AMBAYE AMEKATIKA KABISA MIKONO YAKE.

TUTAENDELEA KUWAPA TAARIFA ZAIDI IKIWA NI PAMOJA NA PICHA KWA KADRI TUTAKAVYOZIPATA.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...