Friday, January 3, 2014

ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MKUPUO AENDELEA VIZURI AOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA. MBEYA



Aida Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.

Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.

Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.


kikosi cha blog ya www.mbeyayetu.blogspot.com  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida.
Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto  wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5  na  2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa.
Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.
Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb  po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.
Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye.

Na Mbeya yetu

MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI LA KUSHUSHIA CONTAINER BANDARI KAVU KARIBU NA MWANANCHI COMMUNICATION,......TAHADHARI BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILI ZINATISHA

WAFANYAKAZI WA BANDARI KAVU PAMOJA NA POLISI WA KITUO CHA MAGOMENI USALAMA BAADA YA KUUKUSANYA MWILI WA MAREHEMU WAKIUPAKIA KWENYE GARI LA POLISI

ASKARI WA KIKOSI CHA DEFENDER MAGOMENI WAKIUSHUSHA MWILI WA MAREHEMU MARA BAADA YA KUFIKISHWA KWENYE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

MWILI WA MAREHEMU BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI LA KUPAKULIA CONTAINERS

AFANDE ISSA MMOJA WA ASKARI MAHILI WA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI AKIUANGALIA MWILI WA MAREHEMU KWA HUZUNI BAADA YA KUUKUSANYA NA KUUPAKIA KWENYE GARI ILI KUPELEKWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

UBONGO WA MAREHEMU UKICHANGANYIKA NA DAMU

HILI NDILO GARI LILILOMGONGA MAREHEM

BAADA YA KUGONGWA UKIWEKWA KWENYE MFUKO ILI KUPELEKWA MUHIMBILI

MARA BAADA YA TUKIO

GARI LILILOSABABISHA KIFO CHA MTU HUYO

MWENYE SURUALI NYEUPE NDIYE BOSI WA MAREHEMU AKITOA MAELEZO KWA POLISI




MWILI BAADA YA KUFIKISHWA MUHIMBILI


BAADAE GARI LILIENDELEA NA KAZI KAMA KAWAIDA YA KUPAKIA CONTAINERS
 MTU MMOJA AMBAE JINA LAKE HALIKUFAHAMIKA MARA MOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA KUSHUSHA NA KUPAKIA CONTAINERS KATIKA BANDARI KAVU ENEO LA TABATA ARMY RELINI  KARIBU KABISA NA KITUO CHA POLISI NA OFISI ZA GAZETI LA MWANANCHI.

TUKIO HILO LILITOKEA JANA MAJIRA YA JIONI BAADA YA GARI HILO KUMGONGA MTU HUYO AMBAE INASEMEKANA NI MMOJA KATI YA MADEREVA WA MALORI YANAYOPAKIA NA KUSHUSHA CONTAINER ENEO HILO.

MASHUHUDA WANASEMA MTU HUYO ALIKUWA AMEJIPUMZISHA NA GARI HILO KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUPAKIA CONTAINERS WAKTI LIKIRUDI NYUMA DEREVA WAKE HAKUMUONA NA NDIPO AKAMGONGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

BAADAE POLISI WA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI WA KITUO CHA MAGOMENI USALAMA AMBAO WALIKUWA DORIA WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANYA KAZI NGUMU YA KUUKUSANYA MWILI WA MAREHEMU AMBAO ULIHARIBIKA VIBAYA ILI KUUPELEKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI




Wednesday, January 1, 2014

MABONDIA WALIVYOTIFUANA MKESHA WA MWAKA MPYA


Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo 
Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana kakonde na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao wa raundi sita kwa ajili ya kufunga mwaka king class mawe alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point 

Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point 
USHINDI RAHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKINULIWA MKONO JUU BAADA YA KUMDUNDA MUSTAFA DOTTO WAKATI WA KUSHEREKEA USIKU WA MWAKA MPYA ZAIDI TEMBELEA 
Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makone na Ibrahimu Maokola wakati wa mpambano wao ulifanyika kwa ajili ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya Kalama  alishonda kwa k,o ya raundi ya pili  
Bondia Iddy Mnyeke  kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao wa kuuwaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya mpambano huo ulito droo  picha na 

Cosmas Cheka na Iddy Mnyeke wakipambana

MABONDIA WAKISUBILI MATOKEO AMBAYO YALIKUWA NI DROO

AJALI YAUA MKESHA WA MWAKA MPYA JIJINI MBEYA

 Boda boda Mbili zikiwa zimegongana
 Mashuhuda
 Gari Jengine lililo husika na ajali hiyo
 Watu wakiwa wanatazama ajali hiyo
 Boda ikiwa imeharibika vibaya
 Gari dogo likiwa limeharibika baada ya ajali hiyo
 Hii maiti ya Dereva wa bodaboda ambaye alifariki hapo hapo
Watu wakiwa wanashuhudia ajali hiyo
Picha zote na Mbeya yetu Blog

RAIS KIKWETE ASHTUSHWA NA TAARIFA YA KIFO CHA WAZIRI WAKE WA FEDHA MH DR WILLIAM MGIMWA AFRIKA KUSINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
 
Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.
Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi kuliko suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.
 
Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu Mgimwa, Rais Kikwete amesema:  “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mgimwa. Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye Hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”
 
Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu.”
 
“Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana-familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” amesema Rais Kikwete.
 
Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.

WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI DR WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI

ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI MAREHEM DR WILLIAM MGIMWA

SIKU ALIYOKUWA ANAWASILISHA BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2012/2013
Waziri wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63) amefariki dunia.
 
Taarifa za hivi punde zinasema Waziri huyo wa fedha katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete amefariki dunia hii leo baada ya kuugua na kulazwa nchini Afrika Kusini.
Mgimwa aliyezaliowa January 20, 1950 na kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Binafsi ya Milpark ya nchini humo.
 
Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Monday, December 23, 2013

INASIKITISHA SANA: KAKA AKIRI KUMCHINJA MDOGO WAKE BAADA YA BABA YAKE KUMUANDIKISHA MALI ZOTE MTOTO WA MKE MDOGO


Mtoto Kalebu Simwelu(6) enzi za uhai wake, mtoto huyu alichinjwa na kaka yake kwa madai kuwa baba yake alimrithisha mali zote.
Mwili wa marehemu Kalebu ukiingizwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia.
Ibada ya mazishi ikiendelea katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia
Umati wa waombolezaji uliohudhuria maziko ya mtoto Kalebu ambaye aliuawa kwa kuchinjwa na kaka yake aliyedai kuwa baba yao amemuandikisha mali zote.
Jamaa na ndugu wakiendelea na mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia ambako mtoto Kalebu alizikwa.
KATIKA hali isiyo ya kawaida mmoja wa watoto wa Diwani wa Kata ya Nkangamo Weston Simwelu(55) ambaye watoto wake waliuawa kwa kuchinjwa na kunyongwa,Enock Simwelu(23) amekiri kufanya mauaji hayo kwa madai kuwa yametokana na baba yao kumrithisha mali zote marehemu mdogo wao.
Mauaji hayo yalitokea Disemba 19 eneo la TAZARA katika mji mdogo wa Tunduma ambapo wauaji walivamia nyumbani kwa Diwani huyo na kufanya mauaji ambapo walimchinja kwa kisu mtoto Kalebu Simwelu(6) na mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge(17) na miili yao kuficha sebuleni nyuma ya kochi.
Imeelezwa kuwa Enock pamoja na nduguye wa mama mmoja Gabriel walishirikiana kwa pamoja kufanya mauaji hayo kwa madai ya baba yao kufanya upendeleo kwa  mdogo wao Kalebu(6) ambaye ni mtoto wa mke mdogo wa baba yao.
‘’Chanzo cha mauaji hayo kimebainika, mtoto wa mke mkubwa wa Diwani, Enock amekiri kuhusika na mauaji hayo ameshirikiana na nduguye Gabriel Simwelu, madai yao, baba yao amemwandikisha mali zote marehemu Kalebu, mtoto wa mke mdogo wa Diwani,’’amesema Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda Masaki ni kwamba mmoja wa watuhumiwa walioshikiliwa kwa ajili ya mahojiano ambaye ni kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Enock Simwelu(23) amedai kukiri kufanya mauaji hayo akishirikiana na mdogo wake aliyemtambulisha kwa jina la Gabriel Simwelu(19).
Kulingana na taarifa hiyo ni kwamba mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye amehusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na tatizo la baba yake kuandikisha mali zote kwa mdogo wao ambaye ni mtoto wa mke mdogo Kalebu Simwelu.
Kamanda Masaki alisema kuwa mauaji hayo pia yalifanywa kwa kushirikiana na jirani na rafiki yao aliyefahamika kwa jina la Patrick Msigwa(18) mkazi wa eneo la Majengo katika mji mdogo wa Tunduma.
Mara baada ya kutokea kwa mauaji hayo Jeshi la Polisi liliwanasa watu watano wakiwemo watoto wa mke mkubwa wa Diwani Simwelu ambapo kulingana na madai ya awali ni kwamba chanzo kilitokana na mgogoro wa kifamilia.
Wakati tukio hilo la mauaji linatokea Baba wa marehemu Simwelu alikuwa shambani katika kijiji cha Kipaka ilhali mama mzazi wa mtoto Tumaini Yohana(29) alikuwa kazini katika Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Aidha mazishi ya mtoto Kalebu yalifanyika Disemba 21 kwenye makaburi ya Nakonde katika mji mdogo uliopo nchini Zambia na kuhudhuria na umati wa wakazi wa mpakani mwa Tanzania na Zambia ambapo mwili wa mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge yalifanyika katika kijiji cha Isansa wilayani Mbozi.(PICHA KWA HISANI YA SHOMI MTAKI-TUNDUMA) PAMOJA NA RASHID MKWINDA BLOG

TAARIFA YA YANGA YA KUSITISHA MKATABA WA KOCHA WAKE MHOLANZI BRANDTS


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbE15WHhTj1r0NP6sBGQaY2dcPq0jAxbq0tGA0sOKQp7xQTqFkNwLfZZH2z1UZ2gcX488pP5L1HNnDtq_iA8nmsYjBn16PKQflLM7jwXC-htSsWem7V1ocrNjgNSINPHKeeTvlAFXsR_Wy/s1600/BIN+KLEB.jpg
UONGOZI wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
 
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
 
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
 
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
 
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
 
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
 
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
 
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.

Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

Friday, December 20, 2013

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA,OKWI ATUA DAR NA KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA

Okwi akizungumza na Waandishi wa Habari
Anatoka kuelekea kwenye gari
Anasindikizwa na Polisi
Ndani ya gari kiti cha nyuma na Katabaro
Dereva Seif Magari anaondoa gari 'mdogo mdogo' (PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBEIR)
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi amewasili jana mchana majira ya saa 9:45 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda Air.


Okwi amekuja kujiunga na timu yake mpya Yanga SC ambayo ataanza kuitumikia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kimataifa.
Mara baada ya kuwasili JK Nyerere Okwi alipokelewa na vipngozi wa kamati ya mashindano sambamba na washabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla.
Okwi akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege amesema anashukuru kwa kufika salama jijini Dar es Salaam na hasa katika timu yake mpya ya Yanga.
Kikubwa ameahidi kucheza kwa uwezo wake wote kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri katika mashindano yote.
Okwi mara baada ya kuwasalimia washabiki na wanachama wa Yanga uwanja wa Kaunda moja kwa moja ameungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo Protea kujiandaa na mchezo wa jumapili.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...