Thursday, March 14, 2013

HATIMAE PAPA MPYA APATIKANA NI JORGE MERIO BERGOGLIO WA AGENTINA

WANANCHI WALIOKUSANYIKA KATIKA VIWANJA VYA SAINT PETER'S SQUARE VATICAN WAKIFURAHIA KUPATIKANA KWA PAPA MARA BAADA YA KUONA MOSHI MWEUPE
MOSHI MWEUPE UKIASHIRIA KWAMBA PAPA MPYA AMEPATIKANA
PAPA JORGE BERGEGLIO MUDA MFUPI BAADA YA KUCHAGULIWA
KADINALI JORGE MERIO BERGOGLIO WA AGENTINA KABLA SIKU CHACHE KABLA HAJACHAGULIWA PAPA

Wednesday, March 13, 2013

MNYAMA AVAMIA UWANJA NA KUZUA TAFRANI

LOIS BENITO AKIKITOA KIMNYAMA HICHO NJE YA UWANJA KABLA HAJAPIGWA MENO
AKIPIGWA JINO LINGINE
BENITO AKING'ATWA NA KANYAMA HICHO
BENITO AKIKIFUKUZA KABLA YA KUKIKAMATA NA KUKITOA NJE YA UWANJA

Mnyama jamii ya panya alizua tafrani uwanjani wakati wa mechi ya mpira wa miguu kwenye michuano  ya Swiss Super League  mchezo kati ya Thun na Zurich.

 Mnyama huyo alikatiza uwanjani kwa mara ya kwanza hali iliyofanya referee  asimamishe kwanza mchezo ila baada ya kupuliza kipyenga kuashiria mchezo uendelee kimnyama hicho kilirudi tena uwanjani hapo ilibidi zitafutwe nyavu kumkamatia ili wamtoe nje ya uwanja, lakini jambo la kushangaza alizichana na akatoka tena kurudi uwanjani, ndipo mchezaji wa Zurich Loris Benito anaeonekana pichani alipoamua kumkimbiza mnyama huyo na kumshika ili amtoe lakini aliambulia kung’atwa kidoleni lakini hakumuachia na akamtoa nje ya uwanja kupisha mchezo uendelee na baadae akapatiwa matibabu ya huduma ya kwanza kwa kujeruhiwa kidoleni, huku kwetu tungesema mambo ya ndumba.Mambo ya kamnyama hayoo!!!!

JUSTINE BIEBER AKATISHA MAONYESHO YAKE UK KUTOKANA NA KULAZWA HOSPITALI


BIEBER AKIFANYA VITU VYAKE

Kufuatia kulazwa kwa mwanamuziki mahiri Justin Bieber, imebidi ahairishe maonyesho yake yote alokuwa ameyandaa,kutokana na hili imemlazimu kufuta show ya Portugal na msemaji wake amethibitishwa kuhusu kufutwa kwa show hizo,na alipangiwa kufanya show March 12,2013.
Alhamisi iliyopita Bieber  msanii mdogo mwenye miaka 19 alipoteza fahamu kwa takriban dakika ishirini wakati akiwa jukwaani akifanya vitu vyake huko London, hali iliyolazimika awekewe Oxygen imsaidie kupumua.Licha ya kulazwa hospitali lakini Bieber bado anatengeneza vichwa vya habari huko U.K kwani ana mashabiki wengi na walikuwa wanamsubiri kwa hamu sana.









Friday, March 8, 2013

KIJANA MDOGO MWENYE MIAKA 19 ASHINDA UCHAGUZI KENYAK

Kijana mdogo nchini Kenya KIBWOTT MUNGE(19),ameandika historia mpya katika siasa za Kenya na huenda katika ukanda wa Africa mashariki kuwa kijana mdogo kushinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika Jumatatu nchini Kenya.
KIBWOTT MUNGE
 "Nimefurahi sana na huu ni ushindi kwa vijana wenzangu woote na ni ishara tosha kuwa vijana tunaweza",alisema KIBWOTT wakati alipopewa nafasi ya kuwashukuru waliompigia kura kumchagua kuwa diwani.

CUNEYT CAKIR REFEREE WA FIFA AMBAE BADO ANALAUMIWA NA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITE KWA KUMPA NANI KADI NYEKUNDUC

CUNEYT CAKIR akimtoa nje mchezaji wa mancherster United NANI kwa KADI NYEKUNDU baada ya kumchezea rafu ARBELOR wa REAL MADRID,kitendo hiki kimeonekana kuwakera mashabiki wa mashetani wekundu kwa madai aliitoa kimakosa na ikaigharimu timu yao na kulala kwa mabao 2-1.
CUNEYT CAKIR

MFAHAM MARK ELLIOT ZUCKERBERG MTALAAM WA COMPUTER AMBAE KUPITIA UBUNIFU WAKE AMEWEZA KUWAUNGANISHA WATU BILLIONI MOJA DUNIANI KUPITIA MTANDAO WAKE WA FACEBOOK

MARK ZUCKERBERG FACEBOOK CEO




MARK AKIWA NA MKEWE PRISCILLA


RANDI


Randi Zuckerberg dada yake mark ambaye ni mmoja wa maofisa wa juu wa facebook Inc






Mark Elliot Zuckerberg alizaliwa May 14,1984,ni mtaalam wa programmes za computer na mjasiliamali wa masuala ya tovuti wa kimarekani,anajulikana zaidi kama miongoni mwa watu watano waasisi wa mtandao wa kijamii,facebook. Zuckerberg ni mwenyekiti na mtendaji mkuu wa kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook inc na utajiri wake ambao umetokana na mtandao huu wa kijamii facebook unakadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni 9.4,na mahesabu haya ni kwa mwaka 2012.

Zuckerberg alizaliwa na kukulia  New York Marekani, alianza kujishughulisha na mambo ya computer akiwa middle school kama hobby tu, kwa msaada wa baba yake na mwalimu wake aliyependa kumwita Zuckerberg jina la prodigy. Akiwa high school  Phillips Exeter Academy alipendelea sana fasihi katika lugha.
 
Baadae akajiunga na Havard College hapo akachukuwa masomo ya computer science na saikolojia.Akiwa chuoni hapo aliwahi kubuni mtandao aliouita FACEMASH, ambao uliwawezesha wanafunzi kupitia mtandao wa chuo kupiga kura.Kutokana na kubuni mtandao huu kupitia mtandao wa chuo,ulisababisha mtandao huu ufungwe na akachukuliwa hatua za kinidhamu.

Pamoja na wanafunzi aliokuwa anakaa nao katika chumba kimoja na baadhi ya aliokuwa nao katika chuo kikuu cha Havard ambao ni Eduardo Saverin, Andrew Mc Collum, Dustin Moskovitz na Chris Hughes wakaizindua Facebook katika chumba cha bweni lao.Baadae wakaisambaza katika  vyuo vingine huko Marekani na mtandao ukawawezesha wanafunzi kuwasiliana na kutumiana picha kupitia mtandao huu na kabla hajaenda  Palo Alto,Califonia.

Mwaka 2007 Facebook ikampa utajiri mkubwa na kuwa miongoni mwa mabilionea ulimwenguni akiwa na umri wa miaka 23 tu.Hadi kufikia mwaka 2010 facebook ilikadiriwa kuwa na watumiaji  million 500 duniani na hadi kufikia mwaka 2012 facebook imekuwa na watumiaji  billion 1,na kumpa utajiri unaokadiriwa kufikia dola za kimarekani billion 9.4

Sunday, March 3, 2013

RAIS ROBERT MUGABE AFANYIWA BONGE LA PARTY KWA KUTIMIZA MIAKA 89

A
Rais Robert Mugabe akila keki kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 89
Akifurahia maputo yalopambwa kwenye sherehe yake
Akiwa na mkewe kabla ya kukata keki
 
Wafuasi wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamekusanyika katika mji wa Bindura wenye migodi ili kusherehekea rasmi Bwana Mugabe kutimiza miaka 89

Ripoti zinasema sherehe hiyo inagharimu dola 600,000 kutokana na mchango wa makampuni.
Wenye maduka mjini Bindura wanasema waliamrishwa kufunga maduka mapema hapo jana, ili kusaidia kusafisha mji kwa ajili ya party ya siku ya kuzaliwa ya Bwana Mugabe.

Hii ni sherehe ya pili ya Bwana Mugabe kutimiza miaka 89.

Katika party ya kwanza iliyofanywa mwezi uliopita Bwana Mugabe alisema jukumu lake la kuongoza Zimbabwe amepewa na Mungu - ni amri ya Mwenyezi Mungu.

Wapinzani wake wana wasi-wasi kuwa wafuasi wa Bwana Mugabe wanapanga kuanza tena ghasia na vitisho wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu utaofanywa mwaka huu.

Wanasema tayari ofisi za makundi yanayochunguza uchaguzi zimeshambuliwa na polisi wamenyang'anya watu mamia ya redio za kuweza kusikiliza matangazo ya mbali.

Zimbabwe itafanya kura ya maoni kuhusu katiba mpya katika majuma mawili yajayo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...