Saturday, July 27, 2013

MWANARIADHA WA KENYA IRENE CHEBET CHEPTAI AANGUKA NA KUZIMIA MARA BAADA YA KUMALIZA MBIO ZA OLYMPIC LONDON MITA 3000

Mwanariadha wa mbio ndefu wa Kenya Irene Chebet Chepai alikimbizwa hospitalini baada ya kuzimia mara tu alipomaliza mbio za mita 3000.Irene alimaliza mbio hizo akiwa katika nafasi ya 11 na alitumia muda wa 8:56.20 na alianguka na kuzimia mara tu alipovuka mstari wa mwisho
DAKTARI WA KWANZA KUMFIKIA IRENE CHEPTAI MARA BAADA YA KUANGUKA

Collapsed: Irine Chebet Cheptai was rushed to hospital after collapsing following the 3,000m
MADAKTARI WAKIMPA HUDUMA YA KWANZA MARA BAADA YA KUANGUKA


Daktari aliyekuwa karibu yake alimkimbilia na kumuwekea oxygen ili imsaidie kupumua,baadae alichukuliwa kwenye machela akiwa hajitambui kabisa lakini taarifa zilizopatikana alivyofikishwa hospitali alizinduka na hali yake ikawa inarudi taratibu.
treatment: Chebet Cheptai left the track unconscious but, according to reports, later regained consciousness in hospital
CHEPTAI AKIWEKEWA HEWA YA OXYGEN MARA BAADA YA KUZIMIA
Kwa kawaida Irene huwa anakimbia mita 5000 na ameshashiriki mashindano ya Diamond ya msimu huu mara mbili na katika mashindano ya Shanghai aliweka rekodi ya muda wa 14:50.99



The Kenyan finished 11th in the race
IRENE CHEPTAI AKICHUANA VIKALI



Friday, July 26, 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA KAMBI YA KABOYA, BUKOBA, MKOANI KAGERA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mkuki katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013
Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu
Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.Katika maadhimisho haya alikuwepo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman MakunguPICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wazee waliopigana vita miaka ya zamani wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ulinzi,Mh. Shamsi Vuai Nahodha wakati walipokutana na kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na wa pili kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Davis Mwamunyange. PICHA NA IKULU

Thursday, July 25, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI MJINI BUKOBA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba leo Julai 24, 2013.
Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013
mjini Bukoba.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Bukoba baada ya ufunguzi wa jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013 mjini Bukoba.
Picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa Mji wa Bukoba,waliofika kumuona jioni ya leo.PICHA NA IKULU.

Wednesday, July 24, 2013

RAIS WA ZANZIBAR APATA MAPOKEZI MAKUBWA BUKOBA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Masawe, alipowasili katika kiwanja cha Ndege cha Bukoba leo mchana,akiwa katika Mkoa huo Rais atashiriki katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa,ambapo Kitaifa yatafanyika kesho Mkoani Kagera.[Picha na Ramadhan Othman,Mkoani Kagera.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozimbalimbali wa Mkoa wa Bukoba mara alipowasili katika kiwanja cha Ndege cha Bukoba leo mchana,ambapo atashiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa,ambapo Kitaifa yatakuwa kesho katika Mkoa huo. [Picha na Ramadhan Othman,Mkoani Kagera.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kagera mara alipowasili katika kiwanja cha Ndege cha Bukoba leo mchana,ambapo atashiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa,ambapo Kitaifa yatakuwa kesho katika Mkoa huo. [Picha na Ramadhan Othman,Mkoani Kagera.]

DR SHEIN AFUTURU NA WATEJA WA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR PBZ

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziAlhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Abdullrahman Mwinyijumbe,(kulia) na MKurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Juma Amour,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani hoteli alipoalikwa Futari na Uongozi wa Benki jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
>

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi Khamis,(kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Abdullrahman Mwinyijumbe,na MKurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Juma Amour,(kushoto)wakiwa katika Futari iliyotayarishwa na Benki ya Watu wa Zanzibar katika Ukumbi wa Bwawani Hoteli Mjini Unguja jana,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Abdullrahman Mwinyijumbe,wakichukua chakula cha Futari iliyotayarishwa na Benki ya Watu wa Zanzibar katika Ukumbi wa Bwawani Hoteli Mjini Unguja  

 Wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Mjini Unguja jana,ambapo Benki hiyo imetimiza miaka 47 tokea kuanzishwa.
Wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na Wananchi mbali mbali wa walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Mjini Unguja jana,ambapoBenki hiyo inasherehekea kutimiza miaka 47 tokea kuanzishwa

MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE APELEKWA AFRIKA KUSINI

picha hii ni ya sheha wa shehia ya tomondo wilaya ya magharibi unguja Mohammed Omar Said,alipomwagiwa tindikali huko Zanzibar,Tukio kama hili limemkuta mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre bw Said Mohammed Saad
MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Taarifa zilizopatikana Jumatano na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, zinaeleza kuwa alipelekwa Afrika Kusini juzi.

Kamanda Wambura alisema ni kweli kuna taarifa kuwa mfanyabiashara huyo aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Trauma (AMI) iliyopo Msasani, amesafirishwa kupelekwa Afrika Kusini lakini hana taarifa zaidi kuhusiana na mwenendo wa tukio zima kwasababu wakati linatokea hakuwapo jijini Dar es Salaam.

Alisema hadi sasa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, hivyo hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kutokana na unyama huo.

Hata hivyo chanzo cha habari toka ndani ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, kililidokeza  kuwa tukio hilo bado halijapangiwa askari kwa ajili ya upelelezi, hivyo taarifa kamili kuhusiana na mwenendo wa tukio lenyewe bado hazijakamilika.

Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.(HABARI KWA HISANI YA MTANZANIA)

Tuesday, July 23, 2013

IGP AKIWA KATIKA ZIARA UNGUJA NA PEMBA



Wanafunzi wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa  upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani, Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Hapsa Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar baada ya IGP Saidi Mwema kufanya  uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

Monday, July 22, 2013

YANGA YACHOMOA DAKIKA ZA LALA SALAMA YATOKA SARE YA 2-2 NA URA


 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kuzawazisha dhidhi ya URA ya Uganda, lililofungwa na Jerson Tegete katika dakika ya 90 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-2. Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki umefanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa URA ya Uganda, Lutimba Yayo akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Yanga, Ibrahim Job na Rajabu Zahir  katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa URA ya Uganda, Lutimba Yayo akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Jerson Tegete katika mchezo wa kimataiafa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
Wachezaji wa URA wakishangilia bao la pili la timu hiyo.
 Heka heka.
PICHA NA MZUKA WA FUNGO BLOG

MASKINI!! PAPII KOCHA AMLILIA TENA RAIS KIKWETE


MUIMBAJI Nyota wa zamani wa bendi ya FM Academia, Papii Kocha amemuandikia ombi jingine maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kumuomba MSAMAHA wa kufutiwa adhabu yake ya kifungo cha maisha jela alichopewa yeye na wanafamilia yake kwa kesi ya kubaka.
Ujumbe huo unaelezwa ni wa mara nyingine tena kwa msanii huyo aliyepo gerezani na baba yake, japo hakujawa na hakika kama barua hizo zinamfikia Mheshimiwa na kuzisoma au la. Ebu isome mwenyewe barua hiyo ya 'Mwana Mfalme' Papii Kocha kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete...inaumiza!

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza
(Papii Kocha) Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais....Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo.

Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlaka wakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi.

Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki. Wako mtiifu

Mfungwa NO:836'04 JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
kwa hisani ya Blog ya Udaku Specially

WILSON KAZAURA ASHUSHA MZIGO MPYA WA SAMAKI NA VYAKULA VYA ASILI KUTOKA KAGERA

SAMAKI AINA YA MBOJU AU KITOGA WABICHI MZIGO USHASHUKA KWA KAZAURA

KAMONGO

SATO

MBOJU AU KITOGA

VYAKULA MBALI MBALI VYA ASILI KUTOKA MKOANI KAGERA


KAZAURA FISH CENTER WAMESHUSHA MZIGO MPYAA SAMAKI WA UHAKIKA KAMA SATO,SANGARA,KAMONGO,MBOJU WABICHI,KASHULI,MASHASHA NK,FIKA SINZA MORI KARIBU NA OFISI ZA TAMWA ANATAZAMANA NA KWA CHARLES HILARY,WEKA ORDER MAPEMA KABLA MZIGO HAUJAISHA,KWA ORDER PIGA SIMU 0717 365846 AU FIKA SINZA MORI UJIONEE MWENYEWE

ANGALIA BEACH YA ZIWA TANGANYIKA ILIVYO

ZIWA TANGANYIKA


MDAU WA MWAIPAYA BLOG RASHID KASSOLO AKIWA KATIKA MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA

ANGALIA BEACH YA ZIWA TANGANYIKA ILIVYO SAAFI

TAZAMA PICHA 10 ZA DARAJA LA KIKWETE LILILOPO MTO MALAGARASI











Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...