Friday, September 13, 2013

BINTI AKUTWA AMEKUFA KATIKA CHUMBA CHA KUFANYIA BIASHARA DAR

WANANCHI KATIKA ENEO LA TUKIO

BAADHI YA MAJIRANI KATIKA ENEO LA MWANANYAMALA KISIWANI WAKIKUSANYIKA KUSHUHUDIA MWILI WA BINTI HUYO

MAMA MWENYE NYUMBA AKIMPATIA MAELEZO MTANGAZAJI WA RADIO ONE STEREO OMARY KATANGA ANAETAZAMANA NAE KULIA JINSI TUKIO LILIVYOTOKEA

MWILI WA ASHA RASHID HUSSEIN ALIYEFARIKI KATIKA CHUMBA CHA BIASHARA WAKATI AKITENGENEZA CHAPATI KUSHOTO KWAKE INAONEKANA CHAPATI ALOKUWA ANAITENGENEZA

WANAHABARI WAKICHUKUA PICHA MBALI MBALI ZA MWILI WA MAREHEM KATIKA ENEO LA TUKIO
Msichana mmoja aliyetambulika kwa jina la Asha Rashid Hussein amekutwa amekufa katika chumba ambacho huwa anafanya biashara ya vyakula katika eneo la mwananyamala Kisiwani karibu kabisa na bar ya Paradise.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne wakati binti huyo alipowasha moto katika chumba hicho Alfajiri kwa ajili ya kutengeneza chapati kwa ajili ya chai kwa wateja wake ambao kwa kawaida huwa wanakwenda kununua chai mahali hapo kila siku asubuhi.

Akisimulia jinsi alivyogundua tatizo hilo mama mwenye nyumba ambako tukio hilo limetokea,amesema alishangaa kuona hadi asubuhi ile mlango wa sehemu hiyo ya biashara ulikuwa haujafunguliwa na haikuwa kawaida kwa Asha kwani huwa anafungua mapema sana.

Alipojaribu kuusukuma akagundua kuwa mlango  huo ulikuwa umerudishwa tu na kuwekwa komeo dogo kwa ndani,walipochungulia ndipo akamuona bvinti huyo kalala huku chapati alokuwa anatengeneza ikiwa kwenye kibao na jikoni alikuwa kabandika chai.

Baadae polisi walipofika eneo la tukio walifungua mlango huo na kuuchukua nmwili huo hadi katika hospitali ya Mwananyamala.

Diwani wa kata hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kupata ripoti ya daktari,amesema sababu ya kifo cha binti huyo ni kuvuta hewa ya sumu inayotoka kwenye mkaa kabla haijakolea Carbon Monoxide ambayo kwa kawaida kama ukiwasha mkaa na eneo husika likawa halina sehemu ya kutosha kupitisha hewa basi husababisha umauti kwa dakika chache sana.

Katika chumbga alichokutwa Asha amekufa hakukuwa na dirisha hata moja na alijifungia wakati anawasha moto huo.

Binti huyo alizikwa juzi kijijini kwao huko kibaha mkoani pwani na habari zinasema alikuwa mgeni katika eneo hilo na ndiyo kwanza alikuwa ameletwa kwa ajili ya kufanya kazi ya mama lishe.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Asha Rashid Hussein mahala pema peponi Amin.

MUNGU MKUBWA!!!!!!!! AUNT ASU AOKOKA,AACHANA KABISA NA MAMBO YA USHOGA

Aliyekuwa shoga maarufu aliyekuwa akijulikana kwa jina la anti asu ameokoka rasmi na kuachana kabisa na shughuli hiyo ambayo ni kinyume kabisa na maadili yetu ya kitanzania.

Blog hii ilianza kupata taarifa zake kwenye ukurasa wa instagram wa dida shaibu mtangazaji wa kipindi cha mitikisiko ya pwani wa kituo cha radio times fm.

Katika ukurasa wake huo dida ameandika aunt asu aacha ushoga amrudia mungu,na kuambatanisha picha kadhaa zikimuonesha aunt asu kabla hajaokoka na nyingine ikimuonesha baada ya kuokoka.

Aunt Asu alitangaza uamuzi wake huo katika kipindi cha mitikisiko ya  pwani cha kituo cha times fm ambapo huwa ni mahususi kwa kupiga nyimbo za taarabu na habari zinazuhusu wanamuziki wa taarab na wadau wa muziki huo hapa nchini na kinaendeshwa na mtangazaji huyo Dida Shaibu mwenye masham sham mengi katika kukichagiza.

Watu kadhaa wameonekana kutoa maoni yao tofauti wakimpongeza kwa hatua yake hiyo huku wengi wakisema ama kwa hakika mungu mkubwa na inapaswa woote wenye  tabia kama alizoziacha aunt asu waacha mara moja na kumrudia mungu.

Katika picha zilizooneshwa katika mtandao huo,wengi walionekana kutotambua kama aunt asu ni mwanamke au mwanaume kutokana na mavazi ya kike aliokuwa ameyavaa.
Lakini picha ya pili inamuonesha akiwa amevalia suti yu[po kanisani mara baanda ya kutangaza kuokoka.

Angalia picha zake hapa chini.

AUNT ASU KABLA HAJAOKOKA WAKATI AKIWA SHOGA
PICHA NYINGINE YA AUNT ASU
AUNT ASU KABLA HAJAOKOKA
BAADA YA KUOKOKA


NDANI YA SUTI BAADA YA KUOKOKA

WAZIRI WA WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS BI. FATMA ABDULHABIB FEREJI AKIZINDUA BODI MPYA YA MAKAMISHNA WA TUME YA UKIMWI ZANZIBAR KWENYE OFISI YA TUME YA UKIMWI SHANGANI.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS BI FATMA ABDULHABIB FEREJI  AKIZUNGUMZA NA MAKAMISHNA WAPYA WA TUME YA UKIMWI ZANZIBAR



Friday, September 6, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA JIJINI KAMPALA


0L7C3096  
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda.
0L7C3115 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.(picha na Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. 

Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda. 

Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili. 

Viongozi hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)” unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort. 

Viongozi wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU). 

Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea mjini Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma. 
 
Rais Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa la Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza. 
 
Imetolewa na;
 Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, 
DAR ES SALAAM. 
 05 Septemba, 2013

BAADA YA DAYNA KULALAMIKA KUIBIWA BEAT NA DIAMOND,ANGALIA ALICHOKIANDIKA LEKADUTIGITE MWENZAKE BABA LEVO KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

 
BABA LEVO

ANGALIA JINSI MH JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU ALIVYOBEBWA MSOBWE MSOBWE NA ASKARI WA BUNGE

ASKARI WA BUNGE WAKIMBEBA MH MBILINYI ILI WAMTOE NJE

PICHA ZA VURUGU BUNGENI DODOMA JANA

 
 Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini 
 Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
 Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni 
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo 
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo. hata hivyo   Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
  Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
 Mbunge  wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa  na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya  hivyo na Naibu Spika wa  Bunge, Job Ndugai 
 Mbunge wa Mbeya Mjini  akizuiwa na wabunge  wa CHADEMA ili asiambane na polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
PICHA ZOTE NA BLOG YA JAMII

Wednesday, September 4, 2013

JWTZ YAKAMATA WANAJESHI WANNE WA RWANDA WALIOKUWA KONGO WAKIWASAIDIA WAASI WA M23

SKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Kongo (Monusco), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamedai kuwakamata maofisa wanne wa jeshi la Rwanda, katika mapigano ya wiki iliyopita nchini Kongo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa askari aliyepo ndani ya kikosi cha JWTZ huko nchini Kongo, alisema maofisa hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizi za sasa zinakuja wakati ambapo kumekuwa na madai ya muda mrefu, ambayo yamekuwa yakitolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani kwamba, Rwanda imekuwa ikiwasaidia waasi wa kundi la M-23.

Pamoja na kwamba Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo, kitendo chake cha wiki iliyopita cha kuamua kupeleka bataliani mbili zenye wanajeshi 1,700 ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa ni kishindo cha vikosi vya Umoja wa Mataifa vyenye jukumu la kulinda amani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa kirasilimali, kinatokana na waasi wa M23 kupata kipigo kikali.

Chanzo chetu hicho kutoka uwanja wa mapambano nchini Kongo, kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao wa Jeshi la Rwanda waliwakamata katika mapigano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja, ambayo tayari yamewakimbiza waasi wa M23.

“Askari wa Rwanda tuliowakamata, ni maofisa wa ngazi za juu kabisa jeshini, tena walikuwa na sare za jeshi hilo… walikuwa wakiwasaidia hao M23, lakini kwa kuwa sisi tulikuwa makini tulifanikiwa kuwatandika hadi tukawakamata,” kilisema chanzo chetu hicho.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika zinaeleza kwamba, hatua hiyo ya kuwakamata maofisa hao pamoja na kuondoka kwa waasi wa kikundi cha M23, imefanikisha kushinda vita hiyo kwa zaidi ya asilimia 95.

Mtoa taarifa wetu huyo kutoka Kongo, ameliambia gazeti hili kuwa, tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baada ya kufanikisha hatua hiyo.

MAPIGANO YALIVYOKUWA
Akielezea namna walivyofanikiwa kutoa kibano kwa M23, askari huyo kwanza alikiri kuwa mapigano yalikuwa makali, kutokana na kikundi hicho cha waasi kusheheni vifaa vya kisasa na msaada wanaoupata kutoka Serikali ya Rwanda.

“Kwa kweli mapigano yalikuwa makali sana, lakini kwa upande wetu sisi tulikuwa tunajiamini kutokana na vifaa ambavyo pia ni vya kisasa hususani ikizingatiwa jeshi letu ni la Umoja wa Mataifa.

“Tulifanikiwa kuteka ngome yao kwa kutumia mbinu mbalimbali za kijeshi na kuwafanya watawanyike kabisa katika eneo hilo.

“Ngome yao ilikuwa ni kubwa sana, ina ukubwa wa zaidi ya viwanja vitatu vya mpira… na katika eneo hilo kulikuwa kumesheheni vifaa vyao vya kivita, kama makombora, mafuta, mizinga pamoja na vifaa vingine kama magari na baadhi ya silaha nyingine kubwa kubwa za kivita,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, sasa hali ni shwari ndani ya nchi hiyo ya Kongo.

“Baada ya kuwasambaratisha sasa wamekimbilia eneo moja lililopo karibu na mpaka wa Uganda. Kama unavyofahamu hawa jamaa walikuwa wakitumia mbinu za kujihami kwa kurusha mabomu katika eneo la Rwanda, ili ionekane kuwa sisi tumerusha,” alisema askari huyo.

“Lakini tunamshukuru Mungu, tupo salama ingawa tumempoteza askari mmoja na askari wengine wenzetu wa Tanzania ambao ni wanne, wamepata majeraha kidogo lakini wanaendelea vizuri.

“Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu waendelee kutuombea turudi salama, kwa sababu kazi sasa imeshakamilika,” alisema askari huyo.

Juhudi za gazeti hili kumpata msemaji wa Monusco, Luteni Kanali Prosper Basse kuzungumzia juu ya taarifa hizo, zilishindikana.

Taarifa ambazo tumezinasa kwa siku kadhaa sasa kutoka uwanja wa mapambano na ambazo zimegusa vichwa kadhaa vya habari zinaeleza kuwa, brigedia maalumu ya vikosi vya UN yenye dhamana ya kujibu mashambulizi (FIB), katikati ya wiki iliyopita iliendesha operesheni kubwa iliyoharibu kabisa ngome muhimu ya waasi wa M23, hali inayotajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ndiyo iliyoishtua Serikali ya Rwanda ambayo inatuhumiwa kuwasaidia waasi hao.

Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa, FIB ambayo inaundwa na wanajeshi wapatao 3,000 kutoka Tanzania na Afrika Kusini chini ya Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limejizatiti kwa zana za kisasa za kivita zikiwamo mizinga na helikopta za kivita.

Taarifa kutoka mashariki ya Kongo zinaeleza kwamba, mashambulizi dhidi ya waasi wa M23 ambao hivi karibuni waliripotiwa kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Tanzania aliye katika jeshi la UN, yamesababisha waasi hao kukimbilia katika eneo la milima lililopo umbali wa kilomita tano kutoka mji mdogo wa Kanyaruchinya Mashariki mwa Goma.

M23 WAZUNGUMZA
MTANZANIA Jumatano jana lilifanikiwa kuzungumza na Rais wa M23, Bertrand Bisiimwa, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza sababu za vikosi vyao kuondoka katika ngome yao ya kivita sambamba na taarifa za kuibuka kwa mapigano mapya ya hivi karibuni.

Katika hilo, Bisiimwa alikiri kikosi chake kurudi nyuma siku nne zilizopita, huku akiitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ilitokana na wao kutotaka vita baada ya majeshi ya Kongo kuanza kuwarushia mabomu kwenye kambi yao.

“Sisi tuliamua kurudi nyuma tusiendeshe vita, tunajua aliyetupa hayo mabomu ambayo yalifika mpaka Rwanda, tunaitaka Umoja ya Mataifa ikuje ifanye uchunguzi wake…wakuje waangalie vifaa yetu waone kama inaweza kurusha mabomu hadi Rwanda,” alisema.

Hata hivyo, Bisiimwa alisema kuwa sio kweli kama majeshi ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na JWTZ yaliwasambaratisha katika ngome yao.

“Sio kweli walikuja Kanyaruchina tukiwa tumeondoka na tuliondoka si kwa sababu ya kuwakimbia, hapana tulitaka UN wafanye uchunguzi yake juu ya kurushwa mabomu, kwa sababu wanataka kutuvalisha mambo ya uongo mchafu,” alisema Bisiimwa.

Bisiimwa alijigamba kuwa majeshi ya Kongo hayawawezi na kwamba walikwishawashindwa, lakini akakiri kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaweza kuwaondoa.

“Ninakiri hiyo kwa sababu Umoja wa Mataifa inaweza kututoa, unajua inakuwa na nguvu ya hatari,” alisema Bisiimwa kwa Kiswahili cha tabu.

CHANZO-Mtanzania

TAZAMA PICHA SITA ZA LORI LILILOANGUKA KARIBU KABISA NA KITUO CHA MABASI CHA MOROGORO

Add caption





MWANAFUZI ALIESHINDA NA KUONGOZA TOKA DARASA LA KWANZA HADI LA SABA


Mwanafunzi Zainab Aboubakary Mlawa wa shule ya msingi St Magreth iliyopo kimara jijini Dar essalaam akiwa na vyeti vyake  alivyotunukiwa katika mahafali ya darasa la saba  baada ya kufauru katika masomo yote toka alipoanza darasa la kwanza katika shule hiyo mpaka alipofika darasa  la saba na kutunukiwa vyeti vya  nafasi za kwanza kwa kila darasa anapoingia anafanya vizuri na kuongoza masomo yote toka alipoanza darasa la kwanza mpaka anamaliza la saba.
 

Baba mzazi wa mwanafunzi Zainab,  Aboubakary Mlawa  akilimsha keki mtoto wake mpendwa  mara baada ya kunukiwa vyeti katika mahafali ya kumalizika darasa la saba mtoto zainab  ambayo alipata zawadi zote za kitaaluma na nidhamu kwa wanafunzi wote wa darasa la saba toka alipoanza shule miaka saba iliyopita

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALLY IDDI AZINDUA KITUO KIPYA CHA AFYA UNGUJA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikifungua rasmi kituo cha Afya cha Sheia ya Chuini kilichopo Wilaya ya Magharibi.

Balozi Seif akifurahia kitendo cha Mtoto Ikram Silima akipimwa uzito na Watendaji wa Kituo cha Afya cha Chuini mara baada ya kukizindua rasmi ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia nusu karne.

Bibi Lny Paul na Mumewe ambaye hayupo Pichani akisisitiza umuhimu wa wananchi kujenga tabia ya kutunza mazingira katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Chuini uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Bwana Paul Jonson mmoja wa wahisani wakubwa waliochangia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chuini akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima iliyotolewa na wananchi wa Chuini kama ishara ya kumbu kumbu kutokana na mchango wake huo.
Uongozi wa Shehia zinazobahatika kupata wawekezaji katika maeneo yao hapa nchini umetakiwa kujenga uhusiano mwema na wawekezaji hao kwa lengo la kupata maendeleo ya haraka yatakayosaidia kustawisha hali za wananachi wao.


Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hafla fupi ya kuzindua Kituo kipya cha Afya katika Kijiji cha Chuini Wilaya ya Magharibi ikiwa ni mwanzoni mwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 sawa na nusu Karne.


Balozi Seif alisema Uzoefu unaonyesha kuwa wawekezaji wengi hapa nchini hupendelea kuchangia maendeleo ya wananchi lakini mara nyingi hukatishwa tamaa kwa matumizi mabaya ya misaada wanayoitoa kunaofanywa na baadhi ya Viongozi wa shehia  kwa kushirikiana na watendaji wabadhirifu wa Taasisi za Serikali na zile zisizokuwa za Kiserikali. 


Alionya kwamba tabia hiyo mbaya inarejesha nyuma maendeleo ya Taifa na wananchi kwa jumla, hivyo hakuna budi kwa wenye hulka hiyo kuachana nayo mara moja.


“ Mara nyingi na baadhi ya maeneo wawekezaji wetu hukatishwa tamaa na udokozi wa baadhi ya wenzetu ambao hujisahau bila ya  kuzingatiwa kuwa wawekezaji hao ni wageni wetu tuliyokwenda kuwatafuta ili waje kuwekeza nchini mwetu “. Alifafanua Balozi Seif.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wananchi na viongozi wa Shehia ya Chuini kwa kuwepuka matumizi mabaya ya misaada ya wahisani jambo ambalo limesaidia kuwaletea maendeleo ya haraka.


    Balozi Seif alifahamisha kwamba wananchi wa Chuini wamefanikia

    kuwa na uadilifu mkubwa uliopelekea kulinda na kuheshimu michango

    inayotolewa na wahisani, wadau na washirika wa maendeleo ndani na

    nje ya Nchi.


Akizungumzia huduma za afya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameiasa jamii kujenga utamaduni wa kuvitumia vituo vya afya katika kujipatia huduma bora za afya pamoja na kupata taaluma ya kinga ya maradhi tofauti.



Alisema tabia ya baadhi ya watu wakiumwa kufikiria wamerogwa na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji haina tija kwao na  kwa kiasi kikubwa inaweza  kuhatarisha maisha yao.


“ Tunapougua ni vyema tukakimbilia vituoni ili kutibiwa. Tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kila mara, bila ya sababu za msingi tuziache mara moja “. Alisisitiza Balozi Seif.


Aliwahakikishia Wananchi wa Shehia ya Chuini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake, itajitahidi kuona dawa muhimu kwa ajili ya wananchi hao zinapatikana kituoni hapo pamoja na wafanyakazi wa kutosha.


Kuhusu hali ya ukimwi hapa Nchini Balozi Seif alisema maambukizi ya maradhi hayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi badala ya kupungua kama inavyoonekana sehemu nyengine duniani.


Alieleza kwamba Jitihada za Serikali za kupambana na ukimwi hazitaweza kuleta mafanikio bila ya wananchi kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya maambukizi na maradhi hayo ya Ukimwi. 


Alitahadharisha kuwa ukimwi hauna tiba, hivyo wananchi wajitahidi kujiepusha na vitendo vyote vinavyochangia kusambaa kwa ukimwi hapa nchini, kama vile uzinifu, ngono zembe pamoja na  utumiaji wa dawa za kulevya.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika kuunga mkono juhudi za wananchi hao wa Chuini ameahidi kuchangia matofali elfu moja kwa ajili ya kuongeza nguvu za ujenzi wa jengo jipya la Madaktyari wa Kituo hicho cha afya cha Shehia hiyo.


Katika risala yao wananchi hao wa shehia ya Chuini iliyosomwa na katibu wa Kamati ya maendeleo wa shehia hiyo Bibi Narie Mbaraka Kaite alisema Kituo hicho kilichogharimu jumla ya shilingi Milioni 28,000,000/- kitakuwa na huduma zote za msingi.


Bibi Narie alisema uongozi na wananachi wa shehia hiyo hivi sasa wamejikita katika ujenzi wa nyumba ya familia mbili ya daktari ikiwa katika hatua ya msingi ili jamii ya kijiji hicho ifikie hatua ya kupata huduma za afya wakati wote.


Katibu huyo wa kamati ya maendeleo ya shehia ya Chuini kwa niaba ya wananachi na viongozi wa shehia hiyo amewashukuru wafadhili, wahisani na washirika wa maendeleo waliosaidia michango iliyokamilisha ujenzi wa Kituo hicho cha afya.


Naye Mwakilishi wa wahisani na wafadhili wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya Bwana Paul Jonson na Mkewe Bibi LNY wakitoa salamu zao walisema Kituo hicho kitasaidia ukombozi wa kiafya kwa wananchi walio wengi katika shehia hiyo.


Bwana Paul aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara inayohusika na masuala ya Afya kukipatria vifaa vya kazi kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora na za kisasa.


Bibi Lny Paul akaisisitiza jamii ya wazanzibari kujenga tabia ya kupenda kulinda na kutunza mazingira ili visiwa vya Zanzibar viendelee kuwa na haiba nzuri.


Kituo cha Afya cha Chuini kitakuwa kikitoa huduma zote za msingi ikiwemo mama wajawazito, watoto, maradhi ya kawaida, ushauri nasaha pamoja namaabara.
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...