Monday, October 14, 2013

HATARI SANA: MWANDISHI MWENGINE WA HABARI MJINI TUNDUMA AVAMIWA NA MAJAMBAZI NA KUPIGWA RISASI, AJERUHIWA VIBAYA.

Jeraha katika mguu wa mwandishi wa habari Shomi Mtaki lililotokana na risasi baada ya kuvamiwa na majambazi

Shomi Mtaki akionesha jeraha lililotokana na risasi katika mguu wake wa kushoto


Mwandishi wa habari wa  wilayani Mbozi Danny Tweve alipomtembelea Shomi Mtaki kumjulia hali baada ya kuvamiwa na majambazi na kujeruhiwa kwa risasi



Mke wa Shomi Mtaki ambaye naye alijeruhiwa na baruti kifuani kwake

Sehemu ambayo risasi ilipigwa katika mlango


Mwandishi wa habari Dany Tweve akishuhudia Eneo la tukio

Namna ambavyo majambazi yalivyofanya upekuzi katika chumba cha Mtaki kutafuta fedha walizodhani kuwa amehifadhi

Shomi Mtaki aliyejeruhiwa kwa kipigwa risasi na majambazi

Ndugu na jamaa wakiifariji familia ya Mtaki baada ya tukio hilo la uvamizi na kupigwa risasi




Kamanda wa Polisi wilaya ya Momba Bw. Chitanda akimpa pole Shomi Mtaki


Nyumba na trekta katika shambani kwa Shomi Mtaki katika mji mdogo wa Mpemba Tunduma wilayani Momba



NI wiki ya majanga kwa waandishi wa habari nchini, muda mfupi baada ya kupata taarifa ya kupigwa risasi kwa Mwandishi wa habari wa ITV /Radio One Mwandishi mwingine wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma  wilayani Momba mkoani Mbeya  Shomi Mtaki amepigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi shambani kwake katika mji mdogo wa Mpemba.
Mtaki ambaye alikuwa katika nyumba iliyopo shambani kwake alivamiwa usiku wa Octoba 10 na watu watano waliokuwa na silaha aina ya bunduki kisha kumlazimisha kutoa fedha.
Wanablogu waliomtembelea shambani kwake walishuhudia majeraha aliyokuwa nayo Mtaki katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo alisema kuwa siku hiyo majira ya saa 9:00 usiku alisikia mchakato wa miguu nje ya nyumba yake na kwamba alipochungulia aliwaona vivuli vya watu wakiwa wamesimama karibu na trekta lake nje ya nyumba.
Alisema kuwa alipowashitua watu hao walitamka wazi wazi kuwa wanataka fedha na muda huo huo akasikia kishindo kikubwa katika mlango wa kuingilia sebuleni ambapo wavamizi hao walikuwa wamepiga jiwe aina ya FATUMA kwa lengo la kuuvunja mlango ili waingie ndani.
Alisema kuwa mara akasikia mlio wa risasi ikipigwa katika mlango wake na mara ukafunguka na vijana watatu waliingia sebuleni ambapo walichukua jiwe walilotumia kuvunja mlango wa sebuleni na kupiga katika mlango wa chumbani na kisha baadaye walimimina risasi katika mlango huo ambazo zilimpata katika mguu wa kushoto na kumjeruhi.
Mtaki alisema kuwa yeye na mkewe walikuwa wakihangaika na kujaribu kujiokoa maisha yao ambapo mkewe aliposikia mlio wa risasi aliingia chini ya mvungu wa kitanda ili kujinusuru.
‘’Nilijiona nakikaribia kifo vijana walimimina risasi katika mlango wa chumbani zikanikuta mguuni na kunijeruhi vibaya, mlango ukafunguka wakaingia vijana watatu ambao hawakujiziba sura zao,’’alisema.
Alisema kuwa mara baada ya kuingia walianza kumuamrisha atoe fedha, akawajibu kuwa hana fedha ndipo walipoanza kumpiga mgongoni huku wakitishia kumuua na kwamba wakati huo mkewe alikuwa amejificha katika mvungu wa kitanda.
‘’Wale wavamizi walianza kupekuwa vitu mbalimbali, wakachukua simu yangu ya mkononi ambayo mtu wa mwisho kuwasiliana naye alikuwa ni shemeji yangu ambaye ni Mwanajeshi,’’alisema na kuongeza.
‘’Wavamizi wale walichukua simu tatu, simu moja ikajipiga kwa bahati shemeji yangu aliipokea, akasikia vurumai iliyokuwa ikiendelea nyumbani na namna ambavyo tulivyokuwa tukijitetea ili tusiuawe, muda huo huo akaenda kutoa taarifa polisi,’’alisema.
Alisema kuwa wavamizi hao waliingia katika mji wake majira ya saa 8:45 na kuendelea kuwepo pale hadi majira ya saa 9;00 usiku ambapo walichukua simu tatu, tv seat ya nchi 22, ving’amuzi viwili kimoja cha Startimes na kingine cha Zuku vyote vikiwa na thamani ya sh. Milioni 2.
Alisema kuwa mara baada ya wavamizi hao kumaliza kukusanya vitu walivyoona vinafaa waliwaamrisha kuingia chumbani na wao wakatokomea upande wa mashariki na muda mfupi baadaye polisi walifika eneo la tukio wakatukuta mien a mke wangu tukiwa tumekumbatiana huku tukilia na kumuomba Mungu.

MTU MMOJA AMEKUTWA AMEJINYONGA MKOANI MOROGORO

PICHA IKIONESHA MWILI WA MWANAMME MMOJA AMBAE JINA LAKE HALIJAFAHAMIKA MARA MOJAUKIWA UNANING'INIA JUU YA MTI BAADA YA KUJINYONGA MKOANI MOROGORO,PEMBENI WANAONEKANA ASKARI POLISI WAKISHUHUDIA

ASKARI WA JESHI LA POLISI AKIPANDA JUU YA MTI ILI KUFUNGUA KAMBA ALIYOITUMIA MTU HUYO KUJINYONGA

ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI MOROGORO WAKISAIDIANA KUUTOA MWILI HUO KWENYE MTI

MWILI WA MTU HUYO UKIWA UMELAZWA KWENYE GARI BAADA YA KUTOLEWA KWENYE MTI

ALICHOKIANDIKA SAM MAHELA WA ITV KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK KUHUSU HALI YA UFOO SARO

HALI YA MWANDISHI WA ITV UFOO SARO INAENDELEA VIZURI JAPO AMELAZWA KATIKA CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI YAANI ICU KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM.

SAA 12 ASUBUHI LEO NILIWAHI KUFIKA HOSPITALINI KWA AJILI YA KUMJULIA HALI MWANDISHI MWENZANGU, NILIFANIKIWA KUMUONA JAPO KWA DAKIKA CHACHE NA KUMPA POLE NA KUMJULISHA KUWA WATU WENGI WALIFIKA TANGU JANA KUMJULIA HALI LAKINI KUTOKANA NA YEYE UFOO SARO KUHITAJIKA KUPUMZIKA,WENGI WALIZUILIWA KUMUONA KUTOKANA NA UTARATIBU WA HOSPITALI ILI APUMZIKE.

BAADA YA KUMUONA DADANGU HUYO, NILICHUKUA JUKUMU LA KUMUOMBEA KWA MUNGU MWENYE MAMLAKA YOTE ILI AMGUSEHAPO ALIPO KITANDANI, MUNGU AMPE NGUVU, MUNGU AMPONYE HARAKA NA KUMWAMBIA NENO MOJA KUWA MUNGU HAWEZI KUMUACHA PEKE YAKE HIVYO TUMAINI LAKE AWEKE KWA MUNGU PEKE YAKE.

ASANTENI KWA WOTE WANAOENDELEA KUMUOMBEA MWANDISHI MWENZETU UFOO SARO ILI APONE HARAKA.....MUNGU AWE NANYI.

Sunday, October 13, 2013

ANGALIA UJASIRIAMALI WA MBABE WA NGUMI TANZANIA FRANCIS SMG CHEKA

MTAMBO ANAOUTUMIA KUSAGIA CHUPA

WAFANYAKAZI WAKE WAKIWA MZIGONI

SEHEMU YAKUKUSANYIA CHUPA

FRANCIS CHEKA AKIWA NA BONDIA ANAEKUJA KWA KASI YA KIMBUNGA AMOS MWAMAKULA

MTAMBO WA KUSAGA CHUPA

CHEKA AKIWA KWENYE CHUMBA CHA KUHIFADHIA CHUPA TAYARI KWA KUSAGWA

NYUMBA YA FRANCISCHEKA ANAYOITUMIA KUKUSANYIA CHUPA

BONDIA AMOS MWAMAKULA AKIWA NA MWENYEJI WAKE FRANCIS CHEKA AKIONYESHA JARIDA LENYE PICHA YA FRANCIS CHEKA

MWANDISHI WA ITV UFOO SARO AHAMISHIWA ICU BAADA YA KUJERUHIWA KWA RISASI



UFOO SARRO
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi na mtu anaedaiwa kuwa ni mchumba wake na pia mtu huyo kumpiga risasi mama mzazi wa Ufoo na kisha yeye mwenyewekujipiga risasi  na kufariki dunia papo hapo leo alfajiri eneo la kibamba jijini Dar esSalaam
.
Awali taarifa zilizosikika katika vyombo vya habari vya ipp ambapo Ufoo anafanyia kazi  zilisema kuwa Mwandishi wa habari wa Kituo Cha Habari cha ITV na Radio One UFO SARO amepigwa risasi mbili na anayesemekana kuwa ni Mchumba Wake aliyekuwa akifanya Kazi Sudan Kupitia UN.
 Sababu ya Kupigwa Risasi yeye UFO SARO na Mama yake Mzazi Ufo Saro ambaye amepoteza maisha papo hapo ni ugomvi ambao haujajulikana na huku Aliyewapiga risasi UFO SARO pamoja na Mama yake Mzazi Ufo kajipiga risasi chini ya kidevu na kupoteza maisha papo hapo..

Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema Ufoo kwa sasa amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Kwa uangalizi zaidi.
tuendelee kumuombea ili apate unafuu na arejee katika kazi zake za kila siku za kuhabarisha umma.tutaendelea kuwahabarisha zaidi kwa kadri tutakavyokuwa tunapata taarifa kuhusu hali yake.

Thursday, October 10, 2013

PINGAMIZI LA SERIKALI KUHUSU TOZO LA LINE ZA SIMU LATUPILIWA MBALI NA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), na kuzikubalia kampuni tano za simu nchini kujiunga katika kesi ya kupinga tozo ya kodi za simu ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa mwezi. Kampuni hizo zinaungana na Chama cha Kutetea Walaji kupinga utekelezaji wa kodi hizo uliotakiwa kuanza Julai mwaka huu, baada ya kupitishwa bungeni Juni mwaka huu.

Akitoa uamuzi wa jopo, Mwenyekiti wa Jopo la majaji, Jaji Aloysius Mujuluzi, alisema wamekubaliana na hoja zilizowasilishwa na wakili wa kampuni tano za simu, Fatuma Karume, kwamba hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani na wateja wake iko sahihi.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimwakilisha AG aliwasilisha pingamizi la awali kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi akidai kwamba, hati ya kiapo ilikosewa kisheria kwani aliyeapa ni mmoja, Tumaini Shija wa Kampuni ya TTCL.

“Tunakubaliana na hoja za Karume kwamba hoja za kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi hayana msingi, kwa sababu sheria ina ruhusu mtu kuapa kwa niaba ya wengine.

“Kampuni tano za simu, MIC Tanzania Limited, Vodacom, Airtel, ZANTEL na TTCL zimekubaliwa kuingia katika kesi, watakuwa mlalamikaji namba mbili mpaka sita, mlalamikaji namba moja ni Chama cha Kutetea Walaji,” alisema Jaji Mujuluzi.

Jaji Mujuluzi alisema walalamikaji hao baada ya kuungana watafanya marekebisho ya hati ya maombi yao, na Oktoba 15 mwaka huu wataiwasilisha mahakamani, Jamhuri itawasilisha majibu, kisha Oktoba 21 maombi ya kupinga tozo za simu yatasikilizwa.

Mdaiwa katika kesi hiyo ni Wizara ya Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chama cha Walaji kiliwasilisha maombi mahakamani dhidi Wizara ya Fedha hivi karibuni wakipinga tozo hiyo kwa madai kwamba inawaumiza wateja wao.

Wakili Karume akiziwakilisha kampuni za simu, aliwasilisha maombi mahakamani wakitaka waruhisiwe kujiunga katika kesi hiyo na wamekubaliwa.

Majaji wanaosikiliza kesi hiyo ni majaji watatu, Aloysius Mujuluzi (Mwenyekiti wa jopo), Jaji Laurence Kaduli na Jaji Salvatory Bongole.

Walalamikaji hao sita wamewasilisha maombi mahakamani hapo wakipinga sheria mbalimbali zinazokiuka Katiba.


Wanadai wateja wao hawana uwezo wa kulipa kodi ya Sh 1000 kwa kila laini ya simu iliyopitishwa bungeni Juni mwaka huu, hivyo wanaitaka Mahakama kuzuia utekelezaji wa kutoza kodi.

WATU WOOTE WA RAHA HASA WANAOKUMBUKA ZAMANI,TUKUTANE CASSA COMPLEX MASTERS CLUB


Sunday, October 6, 2013

KAZI ZA WANANCHI

Mh Joseph Mbilinyi akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa vyoo alivyoahidi kuvijenga

akiwa na ujumbe wake na viongozi wa shule

vyoo vilivyoanza kujenga
Kazi za wananchi : Mbunge akikagua ujenzi wa vyoo kwenye shule ya msingi ikuti kata ya Iyunga- Mbeya mjni...mbunge aliahidi kujenga vyoo hivi alipoombwa na walimu kwenye mahafali ya darasa la saba mwaka jana ambapo alikuwa mgeni rasmi...

Saturday, October 5, 2013

ANGALIA PICHA ZA AJALI YA BASI LA MACHINGA NA LORI LEO ASUBUHI

DEREVA WA BASI LA MACHINA AKITOLEWA KWENYE BASI HILO BAADA YA KUFARIKI KUTOKANA NA AJALI HIYO

UPANDE WA DEREVA ULIVOHARIBIKA

MASHUHUDA ENEO LA AJALI

WASAFIRI NA MASHUHUDA WA AJALI HIYO KATIKA ENEO LA TUKIO

SEHEMU YA DEREVA YA BASI LA MCHINGA LILIVYOHARIBIKA (PICHA NA MAULID KAMBAYA)
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la abiria la machinga na lori eneo la Ngunja kimanzichana leo asubuhi.

Aliyefariki ni dereva wa basi hilo na walioshuhudia ajali hiyo wamesema chanzo ni mwendo kasi wa magari hayo jambo lililosababisha yagongane uso kwa uso
.
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mtwara lina namba za usajili T607 BYT,limeharibika vibaya hasa sehemu ya dereva hali iliyosababisha kifo cha dereva huyo.

LUKUVI AONGOZA MAZIKO YA DADA YAKE FREEMAN MBOWE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge,William Lukuvi, ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mwanamke wa kwanza nchini kusajiliwa na Bodi ya Wahandisi, Grace Aikael Mbowe (57), ambaye ni dada wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Wakati, Lukuvi akiongoza waombolezaji kwa niaba ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo alisimama wakati wa kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk.Wilbrod Slaa na kuwaonya waombolezaji na viongozi wa vyama vya siasa waliojitokeza msibani kutothubutu kutumia msiba huo kama sehemu ya kuhubiri siasa na badala yake waonyeshe upendo wao katika kuwatia nguvu wafiwa
.
Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Lukuvi alisema serikali imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na kwamba ofisi yake inaungana na familia ya Freeman Mbowe katika kipindi kigumu inachopita kwa sasa.

Grace alifariki katika ajali ya gari wiki iliyopita katika eneo la Kabuku,Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga wakati akielekea jijini Dar es Salaam.

Alikuwa mwanamke wa pili kusajiliwa na bodi ya wahandisi nchini akiwa kama Ofisa mpimaji (Quantity Surveyer) baada ya kuhitimu elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,kitengo ardhi (ARU).

Lukuvi na viongozi wengine wa serikali pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi na wabunge kadhaa wa Chadema, waliongoza waombolezaji kumzika Grace katika makaburi ya familia, Kijiji cha Nshara-Lambo,Tarafa ya Machame Wilaya ya Hai.

Katika mazishi hayo yaliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, msemaji wa Chadema na mbunge wa jimbo la Moshi,  Ndesamburo, alisema Chadema imetoa rambirambi ya  Sh.mil. 1,000,000.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma, alisema kifo cha Grace kimeacha pengo kubwa katika familia ya Mbowe na kwamba hali hiyo isiwafanye watanzania wakaacha kujenga undugu walionao na badala yake kiwafanye kuwa wamoja zaidi.

EATV KUWASHUSHA KWA MARA NYINGINE TENA PSQUARE NCHINI TANZANIA



Wakali kutoka Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye “P-Square” wanatarajia kutua Bongo (Tanzania) mwishoni mwa mwezi November….kwa mujibu wa chanzo chetu kimesema jamaa hao watakuja kupiga show iliyopangwa kufanyika tare 23/11 jijini DSM kwa hisani ya East Africa Television (EATV).

Wakali hao wakiwa ni wasanii pekee kutoka Afrika wenye kusumbua ulimwengu kwasasa kwa kuwa na vibao vikali kama Alingo, Personally na vingine kibao watatua bongo ikiwa ni mara yao ya pili sasa kuja tangu waje kwenye concert iliyopewa jina la “DO ME CONCERT”…enzi izo wanatamba na kibao chao cha Do Me.


Ujio wao huu ni wa mara ya pili kwani mara ya kwanza wasanii hawa walitua nchini kwa mara ya pili chini ya EATV na Radio

Friday, October 4, 2013

NATHAN MPANGALA NADHANI UNAUTANI NA WATU.............

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c2e509d429&view=att&th=141834dd21938d6b&attid=0.1&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P_qNf1fwJHMY4YUihxxfq0b&sadet=1380898025569&sads=ikqRPf-7loDkaDIdSjMt269PSCM

POLISI MOMBASA WADAIWA KUUA VIJANA WANNE BAADA YA KUWASHUKU NI AL SHAABAB MARA BAADA YA SALA YA IJUMAA LEO



Imeelezwa kuwa hali si shwari huko Mombasa baada ya milio ya risasi kurindima mara baada ya sala ya Ijumaa leo mchana.
 
Habari zilizoifikia blog hii zinasema polisi wamewaua vijana wanne wakiwashuku ni Al Shabaab.
Waumini waliokuwa wanatoka msikitini wamechoma makanisa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...