Saturday, November 23, 2013

PSQURE WALIVOTINGA NDANI YA VIUNGA VYA EATV/RADIO

PSQUARE NDANI YA STUDIO ZA EAST AFRICA RADIO





MMILIKI WA BLOG HII AKILA SHAVU LA PICHA NA MAPACHA HAO

NDANI YA STUDIO ZA EATV





WAKIWA NA WAFANYAKAZI WA EATV/RADIO

Tuesday, November 12, 2013

TAZAMA PICHA YA JOKA LILILOMMEZA MWANAMKE MMOJA HUKO DURBAN AFRICA KUSINI

Picha hapo juu imewekwa na mwandishi wa habari wa Africa kusini Linda Laina Nyatoro kwenye ukurasa wake wa face book akieleza jinsi alivyoshuhudia mwanamke aliyemezwa na chatu.

Kwa mujibu wa Linda joka hilo lilimmeza mwanamke huyo siku mbili zilizopita karibu na kaskazini ya mji wa Durban Africa kusini.


MWILI WA MTUHUMIWA ALIYEFARIKI DUNI AKIWA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA WATAMBULIWA NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU.

 BABA MZAZI  WA MAREHEMU   KASSIM  MZEE SAID  ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60,AKIONGEA NA MWANDISHI WA HABARI WA MBEYA YETU KABLA YA KUUCHUKUA MWILI WA KASSIM
MWILI WA MARHEMU KASSIM KABLA YA KUANZA SAFARI YA KWENDA DSM
MOJA YA MAAFISA WA POLISI AKIANDIKA MAELEZO MAFUPI TOKA KWA MZAZI WA KASSIMU KABLA YA KUKABIDHIWA MWILI HUO NA JESHI LA POLISI
BABA MZAZI  WA MAREHEMU   KASSIM  MZEE SAID  ATHUMANI MBOYA MWENYE KOTI JEUSI AKIBEBA MWILI WA MWANAE HUKU AKISAIDIWA NA BAADHI YA WALIOFIKA KUMSAIDIA MZEE HUYO
SAFARI YA KUELEKEA DSM YAANZA


  MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM  SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID  ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA  MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM.

  BAADA YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA  ALIKUWA  ANAITWA KASSIM  SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.

  AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM  SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA AKIWA KATIKA TARATIBU ZA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.

   BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.

  WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.

  MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA,  PIPI HIZO ZINA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140.TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA  MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA MADAWA HAYO.

  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI  KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.

Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Picha na Mbeya yetu

AKOSA KAZI KUTOKANA NA KUWA NA VIDOLE 12 SASA ATAKA KUHAMIA UINGEREZA

Man with 12 fingers seeking typist job
VIJAY SINGH AKIONESHA MIKONO YAKE YENYE VIDOLE 12
Vijay Singh mzaliwa wa India aliezaliwa na vidole 12 anataka kuhama India kwenda Uingereza kutafuta kazi ya ukatibu muktasi baada ya kutafuta kazi nchini mwake bila mafanikio licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuchapa maneno 100 kwa dakika.

Vijay ambae pia anavidole 12 vya miguu sita kila upande anampango wa kuhamia Uingereza baada ya kushindwa kupata kazi India ya kutuma maombi ya kutafuta kazi 50.

Vijay mwenye umri wa miaka 48 kutoka Agra kaskazini mwa India anasema sehemu nyingi alizoomba kazi wanataka msichana mrembo na si mwanaume tena mwenye vidole 12.

Tofauti na watu wengine ambao huwa na vidole vya ziada lakini havifanyi kazi,kwa Vijay ni bahati kubwa kwani vidole vyake vyote 12 vinauwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa speed ya hatari.

Sunday, November 10, 2013

ONYESHO LA USIKU WA KHANGA YA KALE WAFANA

 


 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku Novemba 8, 2013 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mwakilishi wa Micuzi Media Group, Othman Michuzi, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Mkurigenzi wa Gazeti la Jambo Leo,Benny Kisaka, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Mratibu wa Hafla ya Usiku wa Khanga za kale,Asia Idarus, kwa kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Mkurugenzi wa bendi ya Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akijumuika na baadhi ya kinamama kusherehesha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa kucheza miondoko ya Taarab kutoka kwa mwanadada Aisha Mashauzi aliyekuwa akitoa burudani wakati wa sherehe hizo. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akijumuika na baadhi ya kinamama kusherehesha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa kucheza miondoko ya Taarab kutoka kwa mwanadada Aisha Mashauzi aliyekuwa akitoa burudani wakati wa sherehe hizo. 
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo ya Usiku wa Khanga za Kale.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo ya Usiku wa Khanga za Kale.
 Sehemu ya kinadada na kinamama waliohudhuria sherehe hiyo ya Usiku wa Khanga za Kale.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus.
 Mratibu wa Usiku wa Khanga za Kale,Asia Idarus,akipita jukwaani na mwanamitindo wake aliyevalia moja kati ya mavazi yake aliyokuwa akizindua wakati wa hafla hiyo.
 Mwanamitindo,akipita jukwaani na vazi la Asia Idarusi.
 Mwanamitindo Bibi Bomba wa 2013, ....akipita jukwaani kwa mbwembwe akiwa amevalia vazi la Asia Idarus.
 Mwanamitindo Bibi Bomba wa 2013, ....akipita jukwaani kwa mbwembwe akiwa amevalia vazi la Asia Idarus.
 Msanii wa Filam na Muziki nchini,Shilole,akipita jukwaani na vazi la Asia Idarusi.
 Richa Adhia, akipita jukwaani na vazi la Asia Idarus.
 Mwanamitindi na mbunifu wake wakipita jukwaani.
 Mshiriki akipita jukwaani na vazi la Asia Idarusi.
Wanamitindo wakipozi jukwaani na vazi la Asia Idarusi.PICHA NA SUFIAN MAPHOTO

MTUHUMIWA MMOJA AFARIKI DUNIA AKIWA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA TUMBONI. KYELA MBEYA


[DIWANI ATHUMANI- ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  WA KWANZA KUSHOTO AKIANGALIA MWILI WA MAREHEMU  KASSIM SAID KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA MBEYA
 PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZILIZOKUTWA  TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.




§  MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM  SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI.
§  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI  AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA  NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM  MUECK MICHAEL,  AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI  SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§  AWALI BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§  WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
§  KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
§  TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA  MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
§  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
                                                                              
                                                                   [DIWANI ATHUMANI- ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...