Wednesday, January 8, 2014

KICHANGA CHAOKOLEWA KUTOKA KWENYE TUNDU LA CHOO

Mtoto mchanga mwenye umri wa siku mbili amenusurika kufa baada ya mama yake mzazi, Hadija Pangani (29) Mkazi wa Kijiji cha Mpiruka Wilaya Nachingwea, Lindi kumfunga kwenye kiroba na kumtumbukiza chooni.
 
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpiruka, Simon Rashidi alisema mtoto huyo aligunduliwa na Techla Sameul baada ya kusikia sauti ya kulia alipokuwa anajisaidi kwenye choo hicho.
 
Simon alisema baada ya kusikia kelele za mtoto huyo, Techla alitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji hicho, ambao kwa pamoja na kushirikiana na jamii na kufanikiwa kumwokoa mtoto huyo ambaye alikutwa hai akiwa amezungushiwa gagulo na kufungwa kwenye kiroba.
KWA HISANI YA EMMANUEL SHILATU BLOG

Tuesday, January 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA SARAFU YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI IKULU DAR LEO.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo  kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (kushoto) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu baada ya kukabidhiwa Sarafu maalum ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito wa g 16, baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiitazama  Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, baada ya kuipokea kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka  hayuko kwenye picha wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo  kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. Picha na OMR

MAZISHI YA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima baada ya kuweka shada la maua   wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga Marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mjane wa  Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,

Mama Salma Kikwete   akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mama mzazi wa  Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole wananchi wa Kalenga  wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole machifu    wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa,



PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga Marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, 

BREAKING NEEEEEEEEWS,.ZITTO KABWE ASHINDA KESI YAKE DHIDI YA CHADEMA

MAHAKAMA KUU TANZANIA IMEKUBALIANA NA OMBI LA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI MH ZITTO KABWE KUWA ASIJADILIWE NA KAMATI KUU YA CHAMA HICHO HADI KESI YA MSINGI ALIYOIFUNGUA ITAKAPOSIKILIZWA.

WAKILI WA CHADEMA BW KIBWATALA AMESEMA KUFUATIA TARATIBU ZA KIUWAKILI,MAHAKAMA IKITOA UAMUZI WOWOTE LAZIMA UUPOKEE KWANZA NA BAADAE WANAKAA KUJADILI NINI CHA KUFANYA NA MWENZAKE TUNDU LISSU KAMA KUKATA RUFAA AU LA.

ZITTO KABWE MWENYEWE BAADA YA MAAMUZI KUTOLEWA HAKUWEZA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWANI ALIKUWA KWENYE ULINZI MKALI NA ALITOLEWA KWENYE MLANGO MAALUM HUKU WAFUASI WAKE WAKISHANGILIA KABLA YA KUTAKIWA KUTAWANYIKA NA JESHI LA POLISI.

Monday, January 6, 2014

KUAGWA KWA MWILI WA MAREHEM WILLIAM MGIMWA


RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAMA SALMA WAKITOA HESHIMA ZA MWISHO KUAGA MWILI WA MAREHEM WILLIAM MGIMWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji familia yake wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam

BAADHI YA MAWAZIRI WAKIBEBA JENEZA LENYE MWILIWA ALIEKUA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu na familia yake wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam

TAZAMA PICHA ZA WATU WALIOKUFA MAJI NA WENGINE KUOKOLEWA KWENYE AJALI YA BOTI NUNGWI VISIWANI ZANZIBAR

BAADHI YA WATOTO WALIOOKOLEWA

MOJA KATI YA MAITI ZILIZOOPOLEWA

MAITI ILIYOOPOLEWA BAHARINI BAADA YA KUZAMA MAJI KWENYE BOTI HUKO NUNGWI

WATU WALIOOKOLEWA



ZOEZI LA UOPOAJI LIKIENDELEA

Friday, January 3, 2014

ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MKUPUO AENDELEA VIZURI AOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA. MBEYA



Aida Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.

Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.

Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.


kikosi cha blog ya www.mbeyayetu.blogspot.com  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida.
Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto  wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5  na  2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa.
Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.
Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb  po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.
Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye.

Na Mbeya yetu

MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI LA KUSHUSHIA CONTAINER BANDARI KAVU KARIBU NA MWANANCHI COMMUNICATION,......TAHADHARI BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILI ZINATISHA

WAFANYAKAZI WA BANDARI KAVU PAMOJA NA POLISI WA KITUO CHA MAGOMENI USALAMA BAADA YA KUUKUSANYA MWILI WA MAREHEMU WAKIUPAKIA KWENYE GARI LA POLISI

ASKARI WA KIKOSI CHA DEFENDER MAGOMENI WAKIUSHUSHA MWILI WA MAREHEMU MARA BAADA YA KUFIKISHWA KWENYE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

MWILI WA MAREHEMU BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI LA KUPAKULIA CONTAINERS

AFANDE ISSA MMOJA WA ASKARI MAHILI WA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI AKIUANGALIA MWILI WA MAREHEMU KWA HUZUNI BAADA YA KUUKUSANYA NA KUUPAKIA KWENYE GARI ILI KUPELEKWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

UBONGO WA MAREHEMU UKICHANGANYIKA NA DAMU

HILI NDILO GARI LILILOMGONGA MAREHEM

BAADA YA KUGONGWA UKIWEKWA KWENYE MFUKO ILI KUPELEKWA MUHIMBILI

MARA BAADA YA TUKIO

GARI LILILOSABABISHA KIFO CHA MTU HUYO

MWENYE SURUALI NYEUPE NDIYE BOSI WA MAREHEMU AKITOA MAELEZO KWA POLISI




MWILI BAADA YA KUFIKISHWA MUHIMBILI


BAADAE GARI LILIENDELEA NA KAZI KAMA KAWAIDA YA KUPAKIA CONTAINERS
 MTU MMOJA AMBAE JINA LAKE HALIKUFAHAMIKA MARA MOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA KUSHUSHA NA KUPAKIA CONTAINERS KATIKA BANDARI KAVU ENEO LA TABATA ARMY RELINI  KARIBU KABISA NA KITUO CHA POLISI NA OFISI ZA GAZETI LA MWANANCHI.

TUKIO HILO LILITOKEA JANA MAJIRA YA JIONI BAADA YA GARI HILO KUMGONGA MTU HUYO AMBAE INASEMEKANA NI MMOJA KATI YA MADEREVA WA MALORI YANAYOPAKIA NA KUSHUSHA CONTAINER ENEO HILO.

MASHUHUDA WANASEMA MTU HUYO ALIKUWA AMEJIPUMZISHA NA GARI HILO KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUPAKIA CONTAINERS WAKTI LIKIRUDI NYUMA DEREVA WAKE HAKUMUONA NA NDIPO AKAMGONGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

BAADAE POLISI WA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI WA KITUO CHA MAGOMENI USALAMA AMBAO WALIKUWA DORIA WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANYA KAZI NGUMU YA KUUKUSANYA MWILI WA MAREHEMU AMBAO ULIHARIBIKA VIBAYA ILI KUUPELEKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI




Wednesday, January 1, 2014

MABONDIA WALIVYOTIFUANA MKESHA WA MWAKA MPYA


Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo 
Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana kakonde na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao wa raundi sita kwa ajili ya kufunga mwaka king class mawe alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point 

Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point 
USHINDI RAHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKINULIWA MKONO JUU BAADA YA KUMDUNDA MUSTAFA DOTTO WAKATI WA KUSHEREKEA USIKU WA MWAKA MPYA ZAIDI TEMBELEA 
Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makone na Ibrahimu Maokola wakati wa mpambano wao ulifanyika kwa ajili ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya Kalama  alishonda kwa k,o ya raundi ya pili  
Bondia Iddy Mnyeke  kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao wa kuuwaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya mpambano huo ulito droo  picha na 

Cosmas Cheka na Iddy Mnyeke wakipambana

MABONDIA WAKISUBILI MATOKEO AMBAYO YALIKUWA NI DROO
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...