Monday, September 22, 2014
TUMERUDI TENA HEWANI
BAADA YA KUKAA KIMYA KWA MUDA MREFU BLOG HII ILIKUWA KIMYA KUTOKANA NA SABABU MBALI MBALI ZA KIUFUNDI.TUNAOMBA RADHI KWA WALE WOTE WALIOKUWA WANAIFUATILIA NA KOKOSA TAARIFA MBALI MBALI KUTOKA KWENYE BLOG HII,KUANZIA SASA UTAENDELEA KUPATA HABARI NA MATUKIO MOTO MOTO NDANI NA NJE YA NCHI,KARIBUNI TENA
Saturday, July 19, 2014
NDEGE NDOGO YATUA BARABARANI KWA DHARULA NCHINI UGANDA BAADA YA KUISHIWA MAFUTA
Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dhalura katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Philip Mukasa, amesema kuwa ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Sudani ya Kusini.
Rubani wa ndege hiyo aliamua kutua katikati ya barabara baada ya kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha, ambapo aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe na kuamua kutua kwa dharura kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.
Katika dharura hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa, na watu wote wametoka salama.
Haikuweza kufahamika kwa haraka sababu zilizomfanya rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
BARAZA LA USALAMA LAKUTANA KUHUSU UKRAINE KUFUATIA AJALI YA NDEGE
| BARAZA LA USALAMA WAKATI WA DAKIKA MOJA YA UKIMYA KUWAKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA YAO KWENYE AJALI YA NDEGE |
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali nchini Ukraine, kufuatia ajali ya ndege ya Malaysia hapo jana mashariki mwa Ukraine, kwenye eneo linalodhibitiwa na waasi. Taarifa kamili na Amina Hassan
(Taarifa ya Amina)
Mwanzoni mwa mkutano wa leo, Rais wa Baraza la Usalama, Richard Gasana, amewasilisha ujumbe wa rambirambi za wanachama wake kwa familia za wahanga wa ajali hiyo, na serikali za nchi zilizopoteza raia wao
GASANA
"Naomba nyote msimame na kubaki kimya kwa dakika moja, kuwakumbuka waliopoteza maisha yao"
Akizungumza kwenye mkutano huo, Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman wakati hali inaendelea kuzorota kwa kasi nchini Ukraine, inasikitisha kuwa mwanga wa matumaini ulioonekana baada ya kutangazwa mpango wa Rais Poroshenko wa amani, ukiwemo usitishaji mapigano, sasa umedidimia haraka. Kuhusu baa la ndege ya Malaysia, ambalo chanzo chake bado hakijathibitishwa, Bwana Feltman amesema
"Katibu Mkuu amesikitishwa na ripoti zinazoonekana kuwa za kuaminika kuwa kombora la kurushwa angani lilitumiwa. Katibu Mkuu analaani vikali hiki kinachoshukiwa kuwa utunguaji wa kukusudia wa ndege ya kiraia. Tukio hili la kutia hofu ni ukumbusho wa jinsi hali mashariki mwa Ukraine ilivyo mbaya mno, na jinsi inavyoathiri nchi na familia nje ya mipaka ya Ukraine."
ANGALIA PICHA ZA WATUHUMIWA 16 WANAODAIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UGAIDI WAKIPANDISHWA KIZIMBANI NCHINI.
Monday, July 14, 2014
SHAKIRA, WYCLEF WALIVYOWASINDIKIZA GERMANY KUTWAA KOMBE LA DUNIA 2014 JANA USIKU




Mshambuliaji
wa German Mario Goetze (kushoto) akishangilia bao pekee aliloifungia
timu yake dhidi ya Argentina, katika dakika za nyongeza fainali za Kombe
la Dunia jana usiku. German ilishinda bao 1-0
TIMU
ya Germany, jana usiku imeibuka mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la
Dunia 2014 'FIFA World Cup', baada ya kuifunga Argentina kwa bao 1-0,
katika mchezo wa Fainali za Kombe la Dunia uliochezwa kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.
Timu
hizo zilimaliza dakika 90 bila ya kufungana na kuongezwa dakika 30
ambapo German iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1 lililofungwa na MARIO GOETZE, katika dakika ya 22 kati ya dakika 30 za nyongeza bao lililodumu hadi kumalizika kwa dakika hizo za nyongeza.
Germana
wameweza kutwaa Kombe hilo kwa mara ya nne sasa tangu kuanzishwa kwa
michuano hiyo ambapo kwa mara ya kwanza ililinyakuwa mnamo mwaka 1954, 1974, 1990 na hatimaye 2014.
Mchezaji
wa zamani wa Kimataifa wa Hispania, Carles Puyol, akipozi mbele ya
Kombe la Dunia na Mwanamitindo wa Brazil, Gisela Bundchen baada ya kombe
hilo kuwasili uwanjani hapo jana kabla ya kuanza kwa fainali hizo.
RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG JIJINI MBEYA.
Kutoka
kushoto ni Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali katikati
ni Rais Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro ,
wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya Sherehe kuanza Rasmi.
Askofu
Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali akitoa salam za Shukurani
kwa Mgeni Rasmi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pia kutoa Historia ya kanisa
la TAG toka lilipoanza mpaka sasa linatimiza Miaka 75.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye kilele cha Sherehe
za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God katika uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Julai 13, 2014
Baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali wakiwa katika maadhimisho hayo
Charles Mwakipesile akiwatunza watoto baada ya kusoma Bibilia kwa umakini kutoka kichwani
Sherehe zimepamba moto
Baadhi ya Wageni waalikwa kutoka Nje ya nchi waliokuja kuhudhuria Miaka 75 ya TAG
Ankali Issa Michuzi katika Sherehe hizo za Miaka 75 ya TAG
Askofu
Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali katikati akiwa anazungumza
jambo wakati walipokuwa wakijiandaa kutoa zawadi mbalimbali.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Tanzania Assemblies of God (TAG)
akiwa na Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa
kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Julai 13, 2014
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies
of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe
za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
Baadhi ya wadau
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Kanisa la TAG kutoka Marekani
Watoto wakitoa Burudani
Picha ya Pamoja baada ya Sherehe kumalizika
Picha zote na Mbeya yetu.
Wednesday, July 2, 2014
IDADI YA WATU WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MIZIGO JOMO KENYATTA LEO ALFAJIRI WAFIKIA WA
Askari
wa Jeshi la Kenya wakiwa eneo la tukio wakijaribu kutoa msaada katika
Ndege ya mizigo iliyoanguka leo asubuhi katika eneo la Utawala kwenye
Uwanja wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Taarifa
kutoka Kenya zinasema kuwa mpaka sasa imefahamika kuwa jumla ya watu
wanne akiwamo Rubani, waliokua kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufa baada
ya ndege hiyo kuanguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye
uwanja huo ikielekea Moghadishu, Somalia.
Ajali
hiyo imetokea alfajiri ya leo ambapo imeelezwa kuwa ndege hiyo ilikua
iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyinginezo kuelekea
Somalia.
Akithibitisha
ajali hiyo Mkuu wa Polisi wa Jiji la Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa kuwa Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET ilianguka kwenye paa la jengo
la kibiashara wakati likijaribu kutua ghafla baada ya kutokea hitilafu
katika ndege hiyo na kushika moto kisha kuanza kuteketea na watu wanne
waliokua ndani.
Aidha
kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Jijini Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa katika ajali hiyo walinzi wawili walijeruhiwa mmoja ametibiwa na
kuruhusiwa kurejea nyumbani huku mmoja akilalazwa katika hospitali ya
Mama Lucy.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kwenye mabaki ya ndege hiyo kuona iwapo kuna waathirika zaidi.
Saturday, June 21, 2014
WATU SITA WAMEFARIKI PAPO HAPO KATIKA AJALI BARABARA YA BAGAMOYO ENEO LA MAKONGO JIJINI DAR ES SALAAM
![]() |
| BAADHI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI HIYO |
![]() |
| HALI ILIVYOKUWA ENEO LA AJALI |
![]() |
| MOJA YA BASI LILOHUSIKA KATIKA AJALI |
![]() |
| HII NDIYO HALI HALISI ENEO LA AJALI |
![]() |
| ENEO LA AJALI |
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea wakati dereva wa gari la abiria lililokuwa likielekea Mwenge kutoka Tegeta ambaye alikuwa katika mwendo wa kasi kubwa kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa pili wa barabara na kuligonga basi lingine la abiria lililokuwa likitokea Mwenge kuelekea Tegeta.
Akielezea ajali hiyo,kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi kinondoni kamanda AWADH HAJI amesema ajali hiyo ilitokea saa saba mchana na kuhusisha magari manne moja likiwa la raia wa China ambalo liliwakanyaga majeruhi na kuwaua sita kati yao.
Mganga Mkuu wa hospiitali ya jeshi Lugalo ambako maiti na majeruhi walipelekwa brigedia jenerali Dr Makere Josiah amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita huku wengine hali zao zikiwa mbaya na kukimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
TAZAMA PICHA ZA BABU SEYA NA MWANAE PAPII KOCHA WAKITUMBUIZA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA
![]() |
| NGUZA VICKING AKILICHARAZA GITAA HUKU PAPII AKIIMBA |
![]() |
| PAPII KOCHA AKICHEZA KWA MADAHA |
![]() |
| PAPII KOCHA AKIIMBA HUKU BABA YAKE NGUZA VICKING AKIPIGA GITAA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA YALIYOFANYIKA KATIKA BWALO LA MAGEREZA SIKU YA IJUMAA 20/06/2014 DAR ES SALAAM |
![]() |
| PAPII AKITUMBUIZA NA WAFUNGWA WENZIE |
![]() |
| PAPII AKIIMBA KWA HISIA WIMBO MAALUM WA SIKU YA MAGEREZA |
![]() |
| PAPII AKIMUANGALIA BABA YAKE ANAVYOLICHARAZA GITAA |
![]() |
| NGUZA VICKING NA MWANAE WAKITUMBUIZA |
![]() |
| PAPII KOCHA MTOTO WA MFALME |
Monday, March 10, 2014
WATAALAMU WA USALAMA WA ANGA WATOA SABABU ZINAZOHISIWA ZIMESABABISHA NDEGE YA SHIRILA LA NDEGE LA MALAYSIA KUANGUKA
![]() |
| NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA BOING 777 ILIYOPOTEA NA MPAKA SASA HAIJULIKANI ILIPO IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200 |
![]() |
| WATAALAM WA VIETNAM WAKIWA KATIKA NDEGE KUFUATILIA ENEO AMBALO WANAHISI NDEGE HIYO ILIANGUKA |
![]() |
| SEHEMU HII INAONYESHA MAFUTA YAKIWA YANAELEA WATAALAM WA VIETNAM WANAHISI IMEANGUKIA HAPA |
![]() |
| SEHEMU INAPOHISIWA KUWA NDEGE YA MALAYSIA IMEANGUKA |
![]() |
| WAPENZI HAWA WALIKUWEMO KATIKA NDEGE HIYO NA INAHOFIWA WAMEPOTEZA MAISHA |
![]() |
| MOJA YA FAMILIA YA WATU WALIOSAFIRI NA NDEGE HIYO |
![]() |
| NDUGU WA ABIRIA AKILIA KWA UCHUNGU MARA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA KUPOTEA KWA NDEGE HIYO |
![]() |
| WAZAZI HAWA MAMA MWENYE SURUALI NYEUSI NA BABA MWENYE JAKETI JEUSI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIJANA WAO NA MPENZI WAKE KABLA YA KUONDOKA KUALA LUMPUR NA NDEGE ILIYOPOTEA |
Wataalam wa masuala ya anga wanasema wakati
mgumu na tete kwa ndege yeyote ni wakati inataka kuruka au kutua,mara chache
sana matukio yasiyokuwa ya kawaida huwa yanatokea pale ndege inapokuwa angani
umbali wa takribani mile saba sawa na kilometa 11 kutoka usawa wa ardhi.
Kwa
hiyo kwa kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysi awakati ikiwa
angani siku ya Jumamosi asubuhi ikiwa na abiria zaidi ya 200 katika bahari ya
kaskazini mwa China,imefanya wataalamu wa masuala ya anga kubaini kwamba
chochote ambacho kitakuwa kimetokea basi kitakuwa kimetokea ghafla na kwa
haraka mno kiasi cha kumfanya hata rubani wa ndege hiyo kushindwa kupiga simu
ya dharula.
Inaweza ikachukua miezi au hata
mwaka kwa wachunguzi wa ajali za ndege kubaini kile kilichotokea kwa ndege hiyo
ya shirika la ndege la Malaysia boing 777 iliyoruka kutoka mji mkuu wa Malaysia
Kuala Lumpur kuelekea China.
Mmoja kati ya wachunguzi hao wa
ajali za ndege bw Todd Curtis ambae ni mhandisi wa masuala ya ndege
mstaafu,amesema katika hatua ya awali kabisa ya uchunguzi wao wanajitahidi
kutafuta ukweli wa mambo ambayo mpaka sasa hawayajui.Todd ameshafanya kazi kwenye
ndege hiyo boing 777 na sasa ni mkurugenzi wa taasisi moja ya usalama wa ndege
huko Malaysia Airsafe.com foundation.
Radar ya jeshi imebashiri kwamba
ndege hiyo iliyopotea Boing 777 inaweza kuwa iligeuza safari iliyokuwa imeianza
kabla ya kupotea,Mkuu wa shirika la ndege la Malaysia amesema siku ya Jumapili
kwamba mamlaka inachunguza abiria wanne ambao utambulisho wao unamashaka.Hii
itaonyesha mazingira yalivyokuwa katika dakika za mwisho kabla ndege haijapata
ajali.Mkuu wa shirika la ndege hakubainisha muelekeo wa ndege hiyo kabla ya
ndege hiyo kupoteza uelekeo au ilikwenda umbali gani kabla ya kupotea ila
baadhi ya taarifa zinatafutwa kwa kushirikiana na radar ya mtu binafsi.
Kama zikipatikana taarifa sahihi
kuwa ndege hiyo iligeuza na kurudi ilikotoka kabla ya kupotea,basi kuna
uwezekano mkubwa kuwa ndege hiyo ilikubwa na tatizo kubwa wakati ikiwa angani
lakini maswali mengi yanaibuka kwa nini rubani hakutoa ishara yeyote katika
chumba cha kuongozea ndege ili apate msaada.Kama kulikuwa na matatizo kidogo ya
kiufundi au engine zote mbili za ndege zilizima,rubani lazima angekuwa na muda
wa kupiga radio ya upepo,Kutokupiga kwake radio ya upepo kunatoa picha kwamba
kuna kitu cha ghafla mno kilitokea hadi akashindwa kufanya chochote, alisema
William Waldock ambae anafundisha masuala ya uchunguzi wa ajali za ndege katika
chuo cha Embry-Riddle Aeronautical Arizona.
Inawezekana kuwa aidha lilitokea
tatizo la ghafla au kitu cha haraka kilichosababisha ikaanguka.Baadhi ya
wataalam wanadhani inawezekana pia likawa ni tukio la ugaidi au rubani akawa
ameiangusha kwa makusudi.
Haijalishi tukio hili limetokea kwa
namna gani,lakini ni mapema mno kusema kitu halisi kilichotokea,Kitu cha msingi
ni kusubiri mabaki ya ndege hiyo yatakapopatikana na kupatikana kwa kisanduku
kinachohifadhi sauti na uchunguzi wa tatizo.Wachunguzi wa kimarekani kutoka
FBI,Bodi ya usafiri Salama ya taifa na shirikisho la uongozi wa anga, na
wataalam wa ndege aina ya Boeing wote wameelekea Asia kusaidia uchunguzi huo.
Utafutaji wa hali ya juu
umeshafanyika baharini lakini mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa
kupatikana kwa ndege hiyo,ingawa Serikali huko Vietnam imesema kuwa Jumapili
jioni ndege yao ilikuwa inapita chini chini katika bahari iliona kitu kama cha
pembe tatu kilomita karibu 90 sawa na mile 56 kusini mwa kisiwa cha Tho
Chu,sehemu hiyo hiyo ambayo mafuta yameonekana yakielea siku ya Jumapili,lakini
gazeti la serikali limesema mkuu wa jeshi msaidizi wa Vietnam amekaririwa
akisema kitu hicho kilichoonekana baharini ni mlango wa ndege.
Baadhi ya mambo yanayohisiwa kuwa
yamesababisha ndege hiyo kupotea ni muundo wa umbo la ndege ambao ni
Alluminium,hali mbaya ya hewa,Rubani kutotambua tatizo mapema,kuzima au
kushindwa kufanya kazi kwa ingini zote mbili za ndege,kupigwa bomu au kutekwa
hizi ni baadhi ya sababu zinazohisiwa na wataalamu wa ajali za ndege na usalama
wa anga kuwa zimesanbabisha ndege hiyo kupotea.
Subscribe to:
Posts (Atom)

























.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)







