Saturday, May 11, 2013

WANANCHI WACHOTA MAFUTA BAADA YA AJALI YA LORI BARABARA YA MOSHI ARUSHA

BAADHI YA WANANCHI ENEO LA KIA WAKIJAZA MAGALONI YAO MAFUTA BAADA YA LORI LA MAFUTA KUPATA AJALI KATIKA ENEO HILO
IDADI KUBWA YA WANANCHI WAKIGOMBEA KUCHOTA MAFUTA,HII NI HATARI NA BADO HATUJAJIFUNZA KUTOKANA NA MATUKIO YA AINA HII AMBAYO YALISHAGHARIMU MAISHA YA WATANZANIA WENGI SANA MKOANI MBEYA
FOLENI ENEO LA AJALI


WENGINE WALIKUWA MASHUHUDA TU

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI AKIPIMA AJALI

MABASI YA ABIRIA YALIKWAMA KWA MUDA ENEO LA TUKIO (habari na picha kwa hisani ya mdau wa blog hii gift shine)
 LORI  la mafuta lililokuwa linatoka njia ya Moshi - Arusha, likiwa na shehena ya mafuta limepindika eneo la kibaoni mbele kidogo tu ya uwanja wa ndege wa kimataifa KIA,karibu na kituo cha mafuta cha penone na kusababisha kundi la watu kuvamia eneo hilo na kuanza kuchota mafuta.

Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni mwendo kasi na lori hilo lilikuwa linataka kulipita gari lingine ndipo likakosa mwelekeo na kupinduka

BAADA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI, MICHEZO,VIJANA NA UTAMADUNI KUTANGAZA KUVALIA NJUGA MZOZO WA RUGE NA LADY JAYDEE,RUGE AFUNGUKA TENA

RUGE MUTAHABA

NAIBU WAZIRI HABARI NA MICHEZO AMOS MAKALLA
LADY JAYDEE
Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Mwandishi wa blog hii ambaye alimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshatoa fuara taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungua jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.

REDDS MISS KIBAHA 2013 CONTAINER KIBAHA 17.05.2013

WAREMBO WANAOWANIA MISS REDDS KIBAHA 2013 KATIKA POZI
USIKU wa Jumatano utabaki kuwa simulizi kwa mashabiki na wadau wa urembo katika jiji la Dar es Salaam ambao walifurika juzi usiku kwenye utambulisho wa warembo wanaowania taji la Redds Miss Kibaha 2013 uliofanyika kwenye ukumbi wa Club ya Kimataifa Club Bilicanas.
 Warembo hao ambao walitambulishwa ikiwa ni sehemu Bilicanas pamoja na kuwajengea kujiamini wawapo jukwaani jambo ambalo walifanikiwa isavyo ikiwa ni pamoja na kulimudu jukwaa. Warembo hao ambao walipanda jukwaani saa saba na nusu usiku wakitambulishwa na Kiongozi wa bendi ya The African Stars Entertainment Twanga Pepeta ambao ndiyo waliotoa burudani katika utambulisho huo.
 Wakati wakipita jukwaani warembo hao walishangiliwa kuanzia mshiriki wa kwanza hadi wa mwisho ambapo walikuwa washiriki 11 kati ya 12 ambao watapanda jukwaa Mei 17 katika ukumbi wa Conteainer Kibaha .
Kiingilio VIP ni sh. 10,000 na siti za kawaida shi 6,000. Kalili anawataja | wadhamini waliothibitisha kuling’arisha shindano hilo ambao ni Michuzi Media Group (MMG), ASET, Chuo cha MC Donald Live Line (Morogoro), Club Bilicanas, PR Promotion Company, Santorine Holiday Resort (Kiluvya), Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Premium Cold, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice Dstv, Image Pub, AKO Catering Services Ltd, Panandi Panandi na Amazon Night Club.

TWANGA PEPETA WALIVYOITEKA DODOMA AT DODOMA ROYAL VILLAGE















Wednesday, May 8, 2013

LWAKATARE AFUTIWA MASHTAKA MATATU YA UGAIDI

MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHADEMA WILFRED LWAKATARE AKIWA CHINI YA ULINZI WA POLISI
MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA BW WILFRED LWAKATARE ALIEKUWA ANAKABILIWA NA MASHTAKA MANNE,AMEFUTIWA MASHTAKA MATATU NA KUBAKIWA NA SHTAKA MOJA LA KULA NJAMA YA KUMLISHA SUMU MHARIRI WA GAZETI LKA MWANANCHI BW DEUS MSAKI

BRAEKING NEWS...SIR ALEX FERGUSON AACHIA NGAZI MAN U



KOCHA WA MANCHESTER UNITED SIR ALEX FERGUSON (71)AMESTAAFU RASMI KUIFUNDISHA TIMU HIYO KWA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MIAKA 26 NA KUIPA VIKOMBE 38 TANGU MWAKA 1986,HIVI KARIBUNI AMEIPATIA UBINGWA WA ENGLAND KUTOKA KWA MANCHESTER CITY.

Sunday, May 5, 2013

PICHA MBALI MBALI ZA MLIPUKO ULIOTOKEA ARUSHA

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA OLASISI KULIPOTOKEA MLIPUKO HUO
MEYA WA MANISPAA YA ARUSHA AKIWASILI ENEO LA TUKIO

POLISI WALIKUWEPO KUIMARISHA USALAMA

ENEO LINAKOSADIKIWA KUANGUKAKITU KINACHODHANIWA NI BOMU BAADA YA KULIPUKA

JAMAA HUYU ALIJERUHIWA VIBAYA NA MLIPUKO HUO


HALI YA TAHARUKI ILIWAKUMBA WAKAZI WENGI WA ARUSHA HIVYO WENGI WALIKUWA WANAKIMBILIA ENEO LA TUKIO KUSHUHUDIA NA KUWATAFUTA NDUGU NA JAMAA WALIOKUWEPO KWENYE TUKIO

POLISI WAKITAFAKARI

KATIKA TUKIO HILI WATU WENGI WAMEUMIA MIGUU


HALI ILIVYOKUWA MARA TU BAADA YA MLIPUKO(PICHA KWA HISANI YA BLOG MBALIMBALI)

MAJAMBAZI YAPORA NA KUUA DAR

Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi yamemuua kwa kumpiga risasi dada mmoja ambae hakufahamika jina lake mara moja kisha kuondoka na kiasi cha shilingi milioni kumi ambazo dada huyo alizichukua wakati akitoka benki ya CRBD tawi la uhuru jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo saa 11:16 jioni na watu hao inadaiwa walikuwa wanamfuatilia dada huyo kwa pikipiki  kisha wakaligonga gari lake,alivyoshuka kuangalia kama gari limeumia,ndipo mmoja wa watu hao waliokuwa kwenye pikipiki akashuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokome na kiasi hicho cha fedha kusikojulikana.
Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio hilo.
mwanamke alieuawa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi akiwa chini baada kupigwa risasi na watu hao kisha kuondoka na fedha kiasi cha shilingi milioni kumi alizokuwa nazo dada huyo(picha nablog ya wananchi)

BREAKING NEWS....

KUMETOKEA MLIPUKO  MKUBWA KATIKA KANISA KATOLIKI  LA MT.YOSEPH MFANYAKAZI PAROKIA YA OLASISI JIJINI ARUSHA ARUSHA NA KUSABABISHA WATU KADHAA KUJERUHIWA WAKATI WA IBADA YA UZINDUZI WA KANISA ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA BALOZI WA PAPA ASKOFU FRANCISCO PADILA IKIENDELEA..BLOG HII ITAENDELEA KUKUPA TAARIFA ZAIDI KWA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA PAMOJA NA PICHA ZA TUKIO HILO

Saturday, May 4, 2013

PICHA NA HABARI ZAIDI KUHUSU KUUAWA KWA WATU WANAOSHUKIWA MAJAMBAZI MKOANI MBEYA

KAMANDA WA POLISIMKOANI MBEYA AKIWAONYESHA WANAHABARI WATU WALIOUWAWA KWA KUSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI

KAMANDA DIWANI AKITOA MAELEZO ZAIDI KUHUSU MAITI ZA WATU HAO

MIILI YA WATU HAO WANAOSHUKIWA NI MAJAMBAZI BAADA YA KUUAWA NA POLISI

SILAHA WALIZOKUTWA NAZO

HILI NDILO GARI WALILOKUWA WANALITUMIA WATU HAO

SILAHA WALIZOKUWA NAZO

SILAHA ZAO

KAMANDA WA POLISI MKOANI MBEYA DIWANI ATHUMANI AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU POLISI WALIVYOWANASA WATU HAO

ASKARI KANZU NA WATU WENGINE WAKIWA MBELE YA SILAHA WALIZOKUWA NAZO MAJAMBAZI HAO
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG


MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
 
Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

WATU 5 WANAOSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI WAMEUAWA NA POLISI MKOANI MBEYA

Watu watano wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuwawa na polisi mkoani Mbeya leo mchana baada ya kurushiana risasi na polisi.
Mashuhuda wanasema polisi walilitilia shaka gari lao hivyo wakati wanalifuatilia,watu hao wakaamua kuwafyatulia risasi polisi ndipo walipo
jibu mashambulizi na kuwaua woote watano
WATU WATANO WANAOSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI MBEYA BAADA YA KUUAWA NA POLISI
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...