Tuesday, August 27, 2013

PICHA ZAIDI KUHUSU MOTO ULIOTEKETEZA KABISA PUB YA SAMAKI SAMAKI MBEZI

ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIENDELEA NA JUHUDI ZA UZIMAJI WA MOTO ULIOTEKETEZA KABISA MGAHAWA WA SAMAKI SAMAKI

MAJI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO YAKIZIMA MOTO KWENYE MOJA YA NGUZO ZILIZOSHIKA MOTO

WANANCHI WA MITAA YA MBEZI WAKIANGALIA JINSI MOTO ULIVYOKUWA UNATEKETEZA SAMAKI SAMAKI

JUHUDI ZA UZIMAJI ZIKIENDELEA

HALI ILIVYO ENEO LA TUKIO

SAKI SAMAKI MBEZI IKIWA IMETEKETEA KABISA

MABAKI YA SAMAKI SAMAKI MBEZI

HIVI NDIVYO SAMAKI SAMAKI MBEZI ILIVYOBAKI

ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIENDELEA NA HARAKATI ZA UZIMAJI

BREAKING NEWS,,JENGO LA SAMAKI SAMAKI MBEZI BEACH LAUNGUA MOTO MUDA HUU

JENGO LA SAMAKI SAMAKI MBEZI BEACH AMBALO TAARIFA ZILIZOTUFIKIA LINAUNGUA MUDA HUU.

JENGO LA SAMAKI SAMAKI MBEZI BEACH LINAUNGUA MOTO MUDA HUU,KWA MUJIBU WA SHUHUDA ALIYEKO ENEO LA TUKIO ANASEMA CHANZO CHA MOTO HUO NI UKARABATI UNAOFANYWA NA DAWASCO KUHAMISHA BOMBA LA MAJI NA WAMEGUSA NYAYA ZA TANESCO AMBAZO ZIMESABABISHA MOTO HUO,,PICHA NA HABARI ZAIDI ZITAKUIJIA HIVI PUNDE

Monday, August 26, 2013

GOLI LA KUFUNGUA MSIMU LA HARUNA NIYONZIMA ,FABRIGAS

VIJANA WAHIMIZWA KULINDA NCHI YAO

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Nalicho(Picha na Maktaba)
---------------------------------------------------------------------------
Na Steven Augustino wa Demashonews , Tunduru
 
MKUU wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Chande Nalicho amewataka
vijana kujenga tabia ya kujitokeza na kupata mafunzo ya Ulinzi wa nchi
yao ambayo yamekuwa yakitolewa katika maeneo yao kupitia proglamu ya
mafunzo ya jeshi la akiba la Mgambo
.
Dc, Nalicho alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya Jeshi la Ulinzi
la Mgambo yanayoendelea katika Tarafa ya Lukumbule Wilayani humo na
kwamba mbali na vijana hao kupatiwa mafunzo hayo ya ukakamavu  lakini
pia hupatiwa mbinu za kuwakabili maadui wa nchi yetu.

Akifafanua taarifa hiyo Dc, Nalicho alisema kuwa endapo kundi hilo
litategea katika ulinzi wa nchi yao ni sawa na kukubali kuiweka rehani
nchi yao na kuiacha ichukuliwe na wanyang’anyi huku wao wakibakia kuwa
watazamaji.

 
Aidha Dc, Nalicho akaendelea kuwatia moyo wapiganaji hao wa Jeshi  la
akiba kuwa ujuzi watakao upata kupitia mafunzo hayo pia yatawawezesha
kufungua ukurasa mpya utakao wawezesha kupata pia ajira hasa wakati
huu ambao makampuni mengi yatafunguliwa baada ya Wilaya yao kufunguka
kwa kuunganishwa na Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupiti ujenzi wa
Barabara ya Lami.

Awali afisa tarafa wa Lukumbule Godfrey Manyahi alimweleza Mkuu wa
Wilaya huyo kuwa pamoja na kupelekwa kwa fulsa hiyo Katika Tarafa yake
Vijana hao hawajaonesha moyo wa kushiriki katika mafunzo hayo na
kwamba hata 49 waliojitokeza na kuandikishwa nao pia wamekuwa watoro
wa kuhudhulia mafunzo hayo.

Manyahi alioendelea kueleza kuwa wanao hudhulia ni chini ya idadi
hiyo ambapo kati yao wasichana ni 2 tu kati ya Vijana zaidi ya 100
waliotarajiwa, idadi ambayo alisema kuwa ni ndogo mno ikilinganishwa
na mahitaji ya askari wa jeshi hilo katika tarafa yao iliyo mpakani
mwa nchi jirani ya msumbiji.

 
Alisema hivi sasa kumbukumbu za ofisi ya Tarafa hiyo zinaonesha kuwa
imebakia na hazina ya asikali mgambo wawi (2) tu ambao walipatiwa
mafunzo ya mwisho miaka 28 iliyopita yaliyofanyika mwaka 1985 nakwamba
hivi sasa ni Wazee hali inayo onesha uwepo wa umuhimu kwa Vijana hao
kujitokeza kwa wingi kwani mafunzo mengine kama hayo pia watachukua
muda mrefu kuwafikia tena katika maaeneo yao.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo Mshauri wa mgabo wa Wilaya ya Tunduru
Benedikti Komba aliwataka viongozi wa Tarafa hiyo kuto watumia vibaya
askari wanaotoa mafunzo hayo kwa vijana wao ili kuwawezesha kushirika
kikamirifu katika zoezi hilo.

 
Alisema Mafunzo hayo yatakayo dumu kwa kipindi cha miezi mitatu idara
yake imepeleka askari wakakamavu na wenye uzoefu mkubwa katikautoaji
wa mafunzo ya aina hiyo na akatumia nafasi hiyo kuwahimiza Vijana
ambao walianza kuregalega katika ushiriki wao kutokana tama na kwa
wanaohitaji waende na kuungana na wenzao kwani vijana wake wapo tayali
kuanzisha kikosi cha pili ili kuongeza idadi ya wahitimu.

NATHAN MPANGALA NA KAMPENI YAKE YA WAFANYE WATABASAMU KATIKA PICHA

Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano, SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, akiteta jambo na wachoraji nje ya Jengo la Watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, walipokutanishwa na mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Nathan Mpangala. Mradi huo ulikwenda kuwafariji, kuwapa zawadi kisha kuchora na watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani hospitalini hapo, ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. Kutoka kushoto Gadi Ramadhan (Art director), Nathan Mpangala (ITV, Mratibu Wafanye Watabasamu), Said Michael ‘Wakudata’ (Tanzania Daima) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ (Nipashe).  Mengi kuhusiana na mradi huu

Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Kijasti’ (mwenye kijibegi mgongoni), akisaidiana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuteremsha zawadi kwa ajili ya watoto wanaoumwa saratani, Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Karibu na ‘Kijasti’ kulia ni ‘Mama Kijasti’. 


Baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakionesha uhodari wa kuchora wakati walipotembelewa na mradi wa Wafanye Watabasamu, unaoratibiwa na Nathan Mpangala, Jumamosi iliyopita. Watoto hao wapatao 80, walizawadiwa sabuni za kuogea/kufulia, dawa za meno, biskuti, toilet papers, mafuta ya kupakaa, matunda na vifaa mbalimbali vya kuchorea toka kwa marafiki wa mradi huo

Wachora vibonzo, Nathan Mpangala ‘Mtukwao’ wa ITV, (kulia) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ wa Nipashe, wakichora na malaika wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu, hospitalini hapo. Mengi kuhusu zoezi hili

Rafiki wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni katunisti wa magazeti ya Mwananchi, Masoud Junior, akishuhudia umahiri wa kuchora toka kwa baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu.

Ilikuwa jambo la kutia moyo kuona watoto hawa wanasahau maumivu ya saratani kwa muda na kujikita kwenye uchoraji. Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala, anawashukuru wachoraji wenzake, ndugu na marafiki wote waliochangia muda, sadaka na tabasamu kwa watoto hao.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, (kushoto), yeye aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuungana na marafiki wa Wafanye Watabasamu, ili kuwafariji watoto waoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi

Mratibu wa wafanye watabasamu na mchoraji wa vibonzo mashuhuri hapa nchini Nathan Mpangala akiwasaidia baadhi ya watoto katika uchoraji

Watoto mbali mbali wanaosumbuliwa na saratani katika hospitali ya Taifa Muhimbili  wakiendelea na uchoraji

Mtoto said akiendelea na uchoraji

Mmoja wa watoto hao akiishangaa kamera huku akiendelea kuchora

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI RUVUMA WAWAFARIJI WAGONJWA HOSPITAL YA MKOA

  Police wakike akionyesha mapenzi kwa mtoto aliyoko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakati walipotembelea hospitali hiyo na kuwafariji wagonjwa
Askari wakipewa maelezo na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  Walta Soko
Askari wa kike akitoa msaada wa kitenge kwa mgonjwa aliyelala kitandani hapo
------------------------------------------------------------------ 
Na Nathan Mtega wa Demashonews,Songea


MTANDAO  wa polisi wanawake mkoani Ruvuma umeanza maadhimisho ya wiki ya polisi wanawake kwa kutembelea na kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake na watoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea.


Akizungumza mwenyekiti wa mtandao huo wa polisi wanawake Mrakibu msaidizi wa polisi Anna Tembo amesema lengo la kutembelea katika hospitali hiyo ni kutoa msaada kidogo pole na hongera  kwa wagonjwa waliolazwa ambao ni wanawake waliojifungua  watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na kuwafariji wagonjwa kwa ujumla.


Amesema pia ni kuifanya jamii itambue kuwa polisi ni sehemu ya jamii ambayo inapaswa kushirikiana na jamii kwa kila jambo na si kwa masuala ya kulinzi na usalama wa watu na mali zao pekee na ushirikiano huo unapaswa kuwepo kwenye idara zote na jamii kwa ujumla.


Amesema kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na wazazi ambao ni wanawake na wanaume hivyo maadhimisho hayo yatatumika pia kwa kuifanya jamii kujenga upendo miongonimwao na hasa kwa watoto ambao wamekuwa ndiyo waathirika wakubwa wa matukio hayo ukatili ambao umekuwa ukifanywa na wazazi wao kwa sababu mbali mbali huku baadhi ya wanawake wakiwatupa watoto wao baada ya kujifungua kwa kushirikiana na wanaume baada ya kudanganyana kuhusu kuoana.


Mwenyekiti wa mtandao huo pamoja na kuiasa jamii kuhusu vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake ambavyo baadhi vimekuwa vimekuwa vikitokea kwa sababu ya kukosekana kwa upendo kwa wanandoa ameshauri kuutumia mtandao huo wa polisi ambao unafanya kazi kwa ushirikiano na kituo cha msaada wa kisheria cha mjini Songea kwa kuwsilisha matatizo yao mbali mbali ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya amani.


Akizungumzia ujio huo wa askari polisi wanawake hospitalini hapo Afisa muuguzi kiongozi wa hospitali hiyo  Marcella Wella mbali ya kuwashukuru askari polisi hao kwa uamuzi huo lakini ameiomba jamii kutambua kuwa polisi nao ni sehemu ya jamii na wanaonesha ushirikiano mkubwa na jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.


Amesema kuwa jamii imekuwa na mtazamo hasi kwa askari wa jeshi la polisi kwa kujengeka na imani kuwa askari polisi wapo kwa ajili ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao tu lakini kitendo cha askari polisi hao kupitia mtandao wao kufika na kuwafariji wagonjwa wakiwemo wanawake na watoto kwa kutoa msaada wa vitu mbali mbali zikiwemo sabuni,madishi na nguo ni ishara kuwa askari polisi nao ni wana jamii ambao wnaonesha ushirikiano mkubwa na jamii wanayoitumikia hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.


Naye mkuu wa kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea mrakibu msaidizi wa polisi  Mashimbi ameitaka jamii kukitumia kitengo hicho cha mtandao wa polisi wanawake kwa kutoa malalamiko yao yanayohusiana na unyanyasaji wa aina yoyote kwa sababu vitendo hivyo vipo kwa kila mmoja na si kwa wanawake pekee.


Amesema kuwa zipo taarifa za wanaume kunyanyaswa na wanawake lakini wamekuwa wakiona aibu kutoa taarifa za unyanyasaji wanaofanyiwa hali ambayo hupelekea kujichukulia sheria mkononi na kuleta madhara makubwa kwa wanafamilia hivyo ni vyema wakautumia mtandao huo wa polisi wanawake kutatua matatizo yao na kujenga utamaduni wa upendo miongoni mwao.

BAADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA SEGEREA KUNUSURIKA KULIPULIWA NA MOTO BOMU LINGINE LIMEKUTWA KWENYE KANISA LA KKKT KIJITONYAMA

SIKU mbili baada ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea, jijini Dar es Salaam kunusurika kuteketea kwa moto uliotokana na milipuko ya mabomu, bomu lingine limekutwa kwenye uzio wa Kanisa hilo Usharika wa Kijitonyama.


mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma
mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma
Hali hiyo ilizua taharuki kubwa kwa wakazi wanaioshi jirani na kanisa hilo ambako pia kuna tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku).
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia NIPASHE jana jioni, viongozi wa kanisa hilo walitoa taarifa polisi na ask
ari kufika eneo hilo ndani ya dakika kumi.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliliambia NIPASHE kuwa baada ya maofisa wa polisi kuwasili katika eneo hilo, walikuta bomu hilo halijalipuka na kuondoka nalo.

Kutokana hofu kuwa bomu hilo lingeweza  kulipuka wakati wowote, baadhi ya wakazi eneo hilo walianza kuondoka katika makazi yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,  Camilius Wambura, alithibitisha kukutwa kwa bomu hilo na kwamba limeanza kufanyiwa uchunguzi haraka.
Wambura alisema polisi walipewa taarifa saa kati ya saa 10:00 na 10:30 jioni kuwa  kuna kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kimewekwa karibu na kanisa hilo.


Alisema baada ya polisi kufika walichukuliwa na kukabidhi kwa wataalam kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulifanyia uchunguzi ili kubaini lilikotengezwa.
“Uchunguzi wa kitu hicho kinachodaiwa kuwa bomu umeanza na taarifa itatolewa rasmi,” alisema.


Usiku wa kuamkia juzi kanisa hilo Usharika wa Segerea, jijini Dar es Salaam nalo lilinusurika kuteketea kwa moto uliotokana na milipuko ya mabomu .
Mabomu hayo  matatu ya kienyeji yaliyorushwa ndani ya kanisa hilo na watu wasiofahamika, yalitengenezwa kwa chupa zilizojazwa mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli na kuwashwa moto.
Moto huo uliunguza eneo la madhabahu na sehemu kubwa ya gari la mchungaji wa kanisa hilo,  Noah Kipingu.

  
Mchungaji Kipingu  alikaririwa akisema kuwa chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu la utambi ziliwashwa moto ili kuchochea milipuko.

Hata hivyo, alisema hakuna majeruhi wala vifo vilivyotokea kwenye mlipuko huo licha ya watu kukumbwa na taharuki.

Kadhalika, kanisa hilo lililojengwa kwa mbao na mabati lilinusurika kuungua pamoja na samani hasa viti vya plastiki, ala za muziki-ngoma, vipaza sauti  na vifaa vya ibada kama mimbari ya kioo havikuathirika.


Alisema waumini zaidi ya 30 wakiwa wameshikana mikono kwenye mduara huku katika ibada ya mkesha wa kuombea mkutano wa Injili uliotarajiwa kuanza jana, walikumbwa na taharuki baada ya kusikia kishindo cha mlipuko kilichoambatana na moto.
Alisema watu wasiofahamika waliokuwa nje ya kanisa hilo, walirusha chupa tatu zilizopitia kwenye mtambaa wa panya na kuangukia ndani ya kanisa sehemu ya madhabahu na kuunguza kurasa chache za Biblia zilizokuwa zimefunguliwa, mto wa kupigia magoti, kipande cha sakafu ya altare na nyaya za spika.


Alisema bomu lingine lilitegwa chini ya gari lake kwenye tangi na lilipolipuka liliunguza. Mabomu hayo yalitupwa kati ya saa 7:45 na saa 8:00 usiku, kipindi hicho waumini  Polisi na waumini huo walipokagua eneo la tukio waliokota chupa nyingine tatu ambazo hazijalipuka zikiwa zimetupwa na watu hao ambao hadi sasa hawajafamika.
Mchungaji huyo alisema hajui sababu ya mashambulizi hayo na hawezi kumtuhumu mtu yeyote kuhusika na tukio hilo.CHANZO: NIPASHE.

Sunday, August 25, 2013

KAMANDA MAALIM GURUMO ATANGAZA KUSTAAFU RASMI MUZIKI KATIKA KIPINDI CHA SUNDAY SPECIAL RADIO ONE LEO

 GURUMO AKIWA STUDIO ZA RADIO ONE

AKIJIBU SWALI KUTOKA KWA MWANAMUZIKI MWINGINE WA ZAMANI CHECHNIE 
MKURUGENZI WA RADIO ONE AMBAE PIA NI MTAYARISHAJI WA KIPINDI CHA SUNDAY SPECIAL DEOGRATIAS RWEYUNGA AKIZUNGUMZA NA MAALIM GURUMU JUU YA KUUSTAAFU KWAKE LEO
MAALIM GURUMO AKIJIBU SWALI LA DEOGRATIAS RWEYUNGA
KAMANDA MAALIM GURUMO
AKIELEZEA HISTORIA YAKE KATIKA MUZIKI

Saturday, August 24, 2013

RAIS KIKWETE AITAKA HALMASHAURI KUU YA CCM KUJADILI KWA KINA MAONI YA WANACHAMA JUU YA KATIBA


RAIS JAKAYA KIKWETE AKIFUNGUA MKUTANO WA CCM MJINI DODOMA
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) rais Jakaya Kikwete amewataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kuhakikisha wanapitia na kujadili kwa kina maoni ya wanachama wao kuhusu mabadiliko ya katiba  ili kupata katiba itakayoliwezesha taifa kuendelea,kudumisha tunu zake za amani umoja na maelewano na kuondoa tofauti zilizoanza kujitokeza.
Rais Kikwete ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mjini Dodoma iliyokutana kama taasisi kujadili maoni ya wanachama wake kuhusu mabadiliko ya katiba ambapo rais Kikwete amesema katiba mpya ndio itakuwa dira ya maendeleo amani na ustawi wa taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho.
 
Akimkaribisha rais Kikwete kufungua mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Abdurahmani Kinana amesema CCM imefanikiwa kukusanya  maoni ya wanachama zaidi ya milioni mbili na laki sita idadi ambayo mpaka sasa haijaweza kufikiwa na chama chochote cha siasa.
Kabla ya kufungua kikao hicho rais Kiwete alizindua Baraza la Ushauri la Wazee la CCM ambalo litakuwa na majukumu ya kutoa ushauri kwa chama na serikali katika mambo mbalimbali ambapo mwenyekiti wake ni rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe Alhaji Ali Hasan Mwinyi  na katibu wake akiwa makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM Mhe Pius Msekwa.

Katika hatua nyingine chama hicho kimetoa ufafanuzi kuhusu sakata la kufukuzwa kwa madiwani nane huko Bukoba ambapo katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kamati kuu imeagiza Mweyekiti wa CCM na katibu wa Mkoa wa Kagera, mbunge wa Bukoba, meya wa Manispaa ya Bukoba, pamoja mwenyekiti wa CCM Bukoba mjini na katibu wake waitwe kujieleza mbele ya kamati kuu kuhusu sakata hilo na baadaye kamati kuu itatoa maamuzi kuhusu sakata hilo.Kamati kuu ya CCM na Halmashauri kuu ya chama hicho zinakutana mjini Dodoma kujadili mambo mbalimbali huku ajenda kuu katika vikao hivyo ikiwa ni kupitia maoni ya wanachama kuhusu mabadiliko ya katiba mpya na kisha maoni hayo kuwasilishwa tume ya mabadiliko ya katiba ambapo ccm inatoa maoni yake kama taasisi.
.

WAFANYE WATABASAMU WATEMBELEA TENA WATOTO MUHIMBILI LEO

Mchoraji katuni wa magazeti ya Mwananchi, ambaye pia ni mdau wa mradi wa Wafanye Watabasamu, Masoud Junior, akichora na baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, leo. Mradi huo ulioanzishwa na kuratibiwa na Nathan Mpangala, hutembelea watoto waliolazwa kipindi kirefu mahospitali ili kuwafariji, kuwapa zawadi kisha kuchora nao michoro mbalimbali. Uchoraji kwa watoto wagonjwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia kama inavyoonekana katika picha, kwani pamoja na maumivu waliyonayo, waliweza kunyanyuka vitandani na kujiachia sakafuni

Mkurugenzi kitengo cha mawasiliano SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, akiteta jambo na wachoraji nje ya Jengo la Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, leo, walipokutanishwa na mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Nathan Mpangala. Mradi huo hutembelea watoto waliolazwa hospitalini muda mrefu, ukilenga kuwafariji, kuwazawadia zawadi, kisha kuchora nao michoro mbalimbali ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. Kutoka kushoto ni Gadi Ramadhani (Art Director), Nathan Mpangala (ITV, mwanzilishi/mratibu wa mradi), Said Michael (Tanzania Daima), na Abdul King O (Nipashe)

NDIVYO SIVYO,UNAPATA PICHA GANI HAPO??


Friday, August 23, 2013

RAIS KIKWETE ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MUGABE WA ZIMBABWE JIJINI HARARE


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mama Salma Kikwete wakiwasili katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Mugabe Agosti 22, 2013.
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Robert Gabriel Mugabe katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais huyo Agosti 22, 2013.
Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakimpongeza Rais Robert Mugabe katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa rais huyo Agosti 22, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wengine jukwaa kuu uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wengine jukwaa kuu uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.
Marais wastaafu Mzee Benjamin Mkapa na mkewe mama Anna Mkapa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.
Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakiwasili katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoka katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini zimbabwe, Mhe Adadi Rajabu.PICHA NA IKULU

Thursday, August 22, 2013

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI YA MAZIKO YA BABA YAKE MAULID KITENGE




KITENGE AKIPEWA POLE NA WAFANYAKAZI WENZIE ANAEONEKANA KUSHOTO KWAKE NI MAULID KAMBAYA

NIXON,KAMBAYA,PIUS PAUL NA LUGENDO MADEGE WALIKUWA KARIBU SANA NA MAULID KATIKA KUMFARIJI


NASAHA ZA HAPA NA PALE KUTOKA KWA NIXON

MMILIKI WA BLOG HII ABDALLAH MWAIPAYA AKIWA NA IRAQ HUDU BONDIA WA ZAMANI TUKIMPA FARAJA MAULID KITENGE

TULIHAKIKISHA KILA KITU KINAENDA SAWA KWA KUFANYA MAWASILIANO HUKU NA KULE



NYUMBANI KWA KINA KITENGE KISOMO KIKIENDELEA JET LUMO MWISHO WA LAMI

BAADHI YA KINA MAMA WALIOHUDHURIA WAKIWA MSIBANI

MWILI WA MZEE BARAKA ABDALLAH KITENGE UKISWALIWA

MWILI WA MZEE KITENGE UKISWALIWA NJE YA NYUMBA YAKE

MIJADALA YA HAPA NA PALE


MAULID KAMBAYA,LUGENDO MADEGE NA IMANI MADEGA KATIKA PICHA YA PAMOJA

HAPA MADEGA ANAMTANIA MADEGE KUWA ANANG'ARA KWA SABABU JINA LAKE LINA FANANA NA LAKE

SUNDAY KAYUNI MKUU WA BENCHI LA UFUNDI TFF AKITETA JAMBO NA IMANI MADEGA

MWILI UKIONDOLEWA NYUMBANI


MWILI WA MZEE BATRAKA KITENGE UKIONDOLEWA NYUMBANI KUELEKEA MAKABURI YA KISUTU

WAOMBOLEZAJI WAKIJIPANGA KUUBEBA MWILI

MAULID KITENGE AKIPEWA POLE

HUYU NDO MZEE WETU,BABA WA MAULID KITENGE MZEE BARAKA ABDALLAH KITENGE,M/MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI INSHAALLAH

MSAFARA KUELEKEA MAKABURINI KUTOKA JET LUMO,SHUKRANI ZA DHATI KWA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WALIHAKIKISHA MSAFARA HAUSIMAMI KWENYE FOLENI


SHUGHULI YA UCHIMBAJI WA NYUMBA YA MILELE YA MZEE KITENGE UKIWA KATIKA HATUA YA MWISHO


HAPA NDIPO ALIPO LALA MZEE WETU



WATU WAKIANGALIA SHUGHULI YA UCHIMBAJI WA KABURI ILIVYOKUWA INAENDELEA

MASTER TINDWA AKIWA NA KINYOZI MKUU WA MAULID KITENGE ILIBIDI NIWAPIGE PICHA KWA KUWA WANA FANANA SANA NA SI NDUGU

MWILI ULIVYOKUWA UKIWASILI MAKABURINI


ISSAC GAMBA,MIMI PAMOJA NA MWALIMU WANGU WA MAMBO HAYA YA UTANGAZAJI MIAKA KUMI ILIYOPITA PALE RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM,SWEDY MWINYI NILIFURAHI KUKUTANA NAE KWENYE MSIBA HUU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...