BAADHI YA WASAFIRI WALIOKOSA NAFASI KATIKA MABASI YAENDAYO TANGA,PICHA HII IMEPIGWA LEO SAA 12 ALFAJIRI |
ABIRIA WAKIKAA BILA YA MATUMAINI YA KUSAFIRI KUTOKANA NA MAGARI KUJAA |
BAADHI YA ABIRIA WAKISUBIRI PENGINE WAPATE NAFASI KATIKA BASI LA RATCO LAKINI WALIKATA TAMAA BAADA YA KUAMBIWA MABASI HAYO YAMEJAA HADI KESHOKUTWA HAYANA NAFASI |
UBUNGO LEO ALFAJIRI KUMRADHI PICHA HAIONEKANI VIZURI KUTOKANA NA HALI GIZA ALFAJIRI |
HALI YA SINTOFAHAMU KWA WASAFIRI WA TANGA |
BASI LA RAHA LEO AMBALO LIMEJAA HADI KESHOKUTWA |
RAHA LEO MOJA KATI YA MAGARI YANAYOTEGEMEWA SANA KWA WASAFIRI WA TANGA |
HAYA NI MABASI MAPYA KWA NJIA YA TANGA RATCOAMBAYO HAPO YAMEJAA NA HAYANA NAFASI KWA WASAFIRI WA TANGA HADI KESHOKUTWA |
Hali hii imeelezwa kuwa ni kutokana na wenyeji wengi wa mkoa huo kuanza kurejea jijini humo ili kusherehekea siku kuu ya Eid.
Kwa mujibu wa mawakala wa baadhi ya mabasi wanasema hali hiyo huwa inajitokeza mara kwa mara hasa wakati zinapokaribia siku kuu na hali huwa tete kwa wakazi wa Tanga wakati wa sikuu kuu ya Eid kama inavyokuwa kwa wasafiri wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakati wa siku kuu za Xmas na Pasaka.
"Kuhusu nauli wale ambao wamebahatika kupata ticket wamelanguliwa kwani nauli ya Tanga ni shilingi elfu 12 hadi 13,ila baadhi ya magari yamewakatia watu ticket kwa shilingi elfu 15 hadi 25 na abiria imewalazimu kutoa kiasi hicho kutokana na hali ilivyo",alisema mmoja wa mawakala ambae hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kwa kusema kuwa Hali ni tete sana kwa wasafiri wa Tanga kwa sababu kuna abiria wengi sana wa kwenda Tanga lakini hakuna wa kurudi ndo maana kumekuwa na tatizo kwa wasafiri wanaoelekea huko .
No comments:
Post a Comment