Leo ni Jumanne tarehe 28 Ramadhani 1434 Hijria sawa na Agosti 6, 2013.
Siku kama ya leo miaka 132 iliyopita alizaliwa Alexander Fleming tabibu, mwana biolojia na mtaalamu wa madawa wa Scottland.
Tabibu huyo pamoja na wasomi wenzake wawili Chain na Florey waligundua mada ya dawa ya antibiotic yaani Penicillin wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka 1945, wasomi hao watatu kwa pamoja walitunukiwa tuzo ya Nobel katika taaluma ya tiba kutokana na ugunduzi wao huo muhimu. Penicillin inatumika sana hivi sasa katika elimu ya tiba.
Miaka 68 iliyopita Marekani, kwa mara ya kwanza iliushambulia vikali kwa bomu la nyuklia na kuuharibu kabisa mji wa Hiroshima huko Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Bomu hilo lilikuwa na nguvu kubwa na uharibifu sawa na ile ya tani elfu 20 za mada za milipuko za TNT. Katika mashambulizi hayo watu zaidi ya elfu tisini waliuawa na wengine 75 elfu walijeruhiwa. Hii ni katika hali ambayo pamoja na kupita miongo kadhaa tangu kujiri mashambulizi hayo ya nyuklia ya Marekani katika mji wa Hiroshima huko Japan, athari zake mbaya bado zinaendelea kushuhudiwa hadi hii leo. Muda mfupi baada ya kuushambulia mji wa Hiroshima, Marekani iliishambulia kwa mabomu ya nyuklia mji wa Nagasaki huko huko Japan na kuilazimisha nchi hiyo kusalimu amri. Maafa hayo ya kutisha na kusikitisha yaliyofanywa na Marekani katika miji miwili ya Japan yanaonyesha uhatari wa silaha za nyuklia zinazomilikiwa na nchi zinazopenda kujitanua duniani kama Marekani na ndio maana kuna udharura wa kusimamiwa na kudhibitiwa silaha hizo na hatimaye kutokomezwa kabisa kwa ajili ya usalama wa dunia.
Na siku kama ya leo miaka 51 iliyopita Jamaica inayopatikana huko Amerika ya Kati ilipata uhuru. Jamaica iligunduliwa mwaka 1494 na mvumbuzi Christopher Columbus na kuwa chini ya himaya ya Uhispania kuanzia karne ya 16 hadi ya 18. Nchi hiyo baadaye ilikoloniwa na Uingereza; na maghasibu wa Ulaya wakawafukuza wenyeji wa kisiwa hicho na badala yake wakawachukua makumi ya maelfu ya watumwa weusi kwa ajili ya kuwalimia mashamba yao.

No comments:
Post a Comment