Maelfu ya wananchi wa Japan leo tarehe 6 Agosti inayosadifiana na
siku ya kukumbuka tukio chungu na maafa ya kutisha yaliyotokana na
shambulizi la bomu la nyuklia lililofanywa na Marekani dhidi ya mji wa
Hiroshima, wamekusanyika katika Bustan na Amani mjini humo na
kuwakumbuka wahanga wa shambulizi hilo la kinyama.
Shughuli ya kumbukumbu ya tukio hilo chungu hufanyika kila mwaka tarehe 6 Agosti kunzia saa mbili na dakika 15 asubuhi, sambamba na wakati Marekani ilipofanya mashambulizi ya bomu la nyuklia huko Hiroshima. Shughuli hiyo huhudhuriwa na wananchi, jamaa wa wahanga waliofariki dunia katika maafa hayo, viongozi wa serikali na wawakilishi wa nchi za kigeni.
Mwaka huu shughuli hiyo imeanza kwa hotuba ya Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ambaye amesisitiza juu ya udharura wa kuharibiwa silaha zote za nyuklia duniani. Vilevile manusura wa mauaji hayo ya kinyama wamehadithia na kueleza masaibu yaliyowapata wakijaribu kuwakumbusha tena walimwengu hatari za silaha angamizi za nyuklia.
Meya wa mji wa Hiroshima pia amehutubia mkusanyiko mkubwa wa watu wa mji huo akiwapa mmono wa pole jamaa wa wahanga wa mauaji hayo na akahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha kwamba, silaha za nyuklia zinaangamizwa kote duniani.
Tarehe 6 Agosti ya kila mwaka huwakumbusha Wajapani jinai kubwa ya Wamarekani na maafa makubwa ya kushambuliwa kwa mabomu ya nyuklia. Katika tukio hilo chungu la kihistoria, rais wa wakati huo wa Marekani Harry Truman aliamuru kufanyika mashambulizi ya bomu la nyuklia dhidi ya watu wasio na hatia wa Japan na kusababisha maafa ambayo kamwe hayatasahaulika katika historia ya mwanadamu. Dakika za mwanzoni baada ya shambulizi hilo kulitukea mlipuko mkubwa na wimbi kubwa la moto likatanda katika anga ya mji wa Hiroshima ambalo lilienea katika ukubwa wa kilomita moja na kuteketeza kila kitu. Katika sekondi chache tu kisiwa cha kupendeza cha Hiroshima na watu wake kilibadilika na kuwa rundo kubwa la majivu. Mjini Hiroshima pekee watu laki moja elfu arubaini waliuawa katika shambulizi hilo la kinyama na maelfu ya wengine walipoteza maisha kadiri miaka ilivyopita kutokana na athari mbaya za miale ya radioactive iliyosababishwa na bomu hilo. Maelfu ya watoto walizaliwa na wangali wanazaliwa wakiwa vilema na maelfu ya wengine wamefariki dunia kutokana na maradhi mbalimbali kama saratani.
Siku kama hii ya leo kila mwaka wananchi wa Japan huomba dua wakitaka kuwepo dunia isiyo na silaha za nyuklia na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za kivitendo za kuangamiza silaha hizo hatari. Hata hivyo kilio na dua hizo za Wajapan hukumbana na sikio lililotiwa pamba la madola makubwa yanayomiliki silaha za atomiki zikiongozwa na Marekani. Marekani ndiyo inayomiliki maghala makubwa zaidi ya silaha za nyuklia duniani na ingali inafanya jitihada za kutengeneza silaha za kisasa zaidi za aina hiyo.
Kwa sasa Marekani inafanya mikakati ya kutengeza kizazi kipya cha silaha za nyuklia zinazoweza kutumiwa katika vita vya kikanda. Silaha za aina hiyo zinatambuliwa kuwa hatari kubwa sana kwa dunia kwa sababu zitaiwezesha Marekani kushambulia nchi yoyote bila ya kuwa na wasiwasi wa kutokea taathira kubwa za mazingira zinazosababishwa na mabomu ya kawaida ya nyuklia.
Meya wa mji wa Hiroshima ameeleza kushangazwa sana na majaribio mapya ya mabomu ya nyuklia huko Marekani na kusema inastaajabisha mno kuona Rais Barack Obama wa Marekani ambaye alisema kuwa anataka kuwapo dunia isiyo na silaha za nyuklia, akiruhusu kufanya majaribio hayo.

No comments:
Post a Comment