|
| MBUNGE WA KASULU MJINI MH MOSES MACHALI
Habari kutoka
Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha
NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana , tukio hilo
limetokea jana jioni wakati Mh. Machalli
akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya
kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili
wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na
kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari
ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka
ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya
nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.
Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio
anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo
lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika
kipigo.
Mhe
Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na
kumkuta anaendelea vyema na matibabu.
.(HABARI KWA HISANI YA LEWIS MBONDE
BLOG)
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment