Friday, June 21, 2013

MAPOKEZI YA DAVID BECKHAM CHINA YASABABISHA WATU KUKANYAGANA NA BAADHI WAUMIA VIBAYA WAKIWEMO MAAFISA USALAMAM


MAAFISA USALAMA WAKIWA KATIKA WAKATI MGUMU KUWAZUIA MASHABIKI

AFISA USALAMA ALIEJERUHIWA




ANGALIA KILA MMOJA ALIINUA SIMU YAKE JAPO APATE PICHA INGEKUWA BONGO SIJUI KAMA KUNA SIMU INGESALIMIKA HAPO

UMATI UKIHANGAIKA JAPO KUPATA PICHA

WENGINE WALIONA BORA WAGUSE HATA GARI TU




Watu watano wamejeruhiwa vibaya katika mapokezi ya David Beckham nchini China baada ya umati mkubwa kujitokeza kumlaki na kutaka japo kumgusa.Licha ya kuustaafu lakini bado mashabiki wake walifurika katika jiji la Shanghai hali iliyosababisha watu watano kujeruhiwa akiwemo polisi.
Katika ratiba yake hiyo jana Beckham alikuwa atembelee chuo kikuu cha Shanghai cha Tongji.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid alikuwa akutane na wachezaji wa timu ya chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba kuitangaza ligi kuu ya China imayptambulika kama Chinese Super League.
Hata hivyo kufuatia umati mkubwa kujitokeza kwa lengo la kumlaki kiungo huyo wa zamani wa England kumesababisha zoezi hilo kushindikana ambapo baadae aliomba radhi kwa mashabiki wake hao kupitia mtandao wa kijamii wa facebook na Sina Weibo.
Maafisa Usalama walishindwa kuzuia vurugu hizo ambapo walikuwa wakisonga mbele licha ya kuwekewa kizuizi.
Katika ujumbe wake Beckham amenukuliwa akisema"Samahani sikuweza kutokea uwanjani kuiona timu kwani ilikuwa ni vigumu kupenya kati kati ya mashabiki.Nimesikia kulikuwepo na watu waliojeruhiwa,Nina matumaini wako salama na nawatakia heri wapone haraka''
Takriban watu 1000 inaaminika walikuwa wanataka japo kumkaribia Beckham na polisi wamethibitisha kuwa maafisa wake watatu walijeruhiwa katika vurugu hizo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 38 alistaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuisaidia Paris-Saint Germain kutwaa taji la ligi ya Ufaransa maarufu kama league 1.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...