Thursday, June 27, 2013

SIMBA YAMPA KISOGO KIPA WAO NAMBA MOJA JUMA KASEJA

JUMA KASEJA

WAKATI ALIPOKUWA TIMU YA YANGA

AKIBEBWA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA KUFANYA VIZURI UWANJANI

AKIWA KAZINI

Kipa namba moja wa timu ya Simba  na Taifa Stars Juma Kaseja,amepewa kisogo na klabu yake yenye maskani yake mtaa wenye pilika nyingi za kila siku Kariakoo.
Akiongea katika kipindi cha michezo cha Radio One stereo mwenyekiti wa kamati ya usajili Hans Pope amesema hawatamsajili tena kipa huyo hivyo atafute sehemu ya kwenda.
Juzi iliripotiwa kwenye gazeti la Nipashe kuwa kocha mkuu wa timu hiyo alisema anamshauri Juma Kaseja kama mwanae kuwa atafute kitu kingine cha kufanya kwani mashabiki wengi ambao wamekuwa wakifika kwenye mazoezi ya timu hiyo wamekuwa wakimpigia kelele kocha hhuyo kuwa hawataki kumuona tena kipa huyo katika timu hiyo kwani amekuwa akiwababaisha sana.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba kipa huyo amegoma kusaini mkataba mpya na klabui yake hiyo kwa kutokubali kiasi timu ilichopanga kumpatia na yeye alikuwaa anataka kiwango cha juu zaidi.Lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Juma Kaseja ilikuwa apewe milioni 20 ili asaini mkataba mpya na yeye hakukubaliana na kiwango hicho akitaka apewe  milioni 40 kiasi ambacho kamati ya usajili ya timu hiyo imesema hakina pesa hizo za kumlipa kipa huyo hivyo atafute pa kwenda na hawatampa mkataba tena.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...