Monday, September 16, 2013

POLISI YAUA JAMBAZI DAR BAADA YA KUPORA FEDHA KATIKA DUKA VINGUNGUTI,TAHADHARI NA TUNAOMBA RADHI BAADHI YA PICHA ZINATISHA

MTU ANAEDHANIWA NI JAMBAZI BAADA YA KUUAWA NA POLISI LEO ENEO LA SUKITA JIJINI DAR

KIKOSI CHA DEFENDER CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKOSI CHA POLISI MAGOMENI

WAZEE WA KAZI MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA

MOJA KATI YA WATU WANAODAIWA KUPORA FEDHA VINGUNGUTI BAADA YA KUUAWA NA POLISI
Jeshi la polisi kikosi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumuua mmoja kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mara baada ya kurushiana risasi na polisi eneo la SUKITA jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo saa tano asubuhi maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la tukio.

Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao, alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea kusikojulikana

2 comments:

  1. HONGERA JESHI LA POLICE KWA KAZI NZURI, YAPO MENGINE MBEZI BEACH NJOON NA HUKU JAMAN

    ReplyDelete
  2. Kumbe hata askari anauwa mtu anaedhaniwa kafanya kosa, raia akichoma mwizi utasikia "unajichukuria sheria mkononi". Wao mbona hawakumlenga miguu wakampeleka mahakamani. Au kwenye mafunzo wanajifunza kulenga kichwa tu?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...