Monday, September 22, 2014

JOSE MOURINHO ADAI MAPENZI YA FRANK LAMPARD KWA CHELSEA YAMEKWISHA!


Jose Mourinho says Frank Lampard's love story with Chelsea ended when he joined a title competitor
 
Lampard slots home from inside the penalty area to send the City fans into ecstasy against his former employers
Lampard akiteleza katika eneo la penalti na kuifungia City bao.

Jose Mourinho anasema mapenzi ya Frank Lampard kwa Chelsea yalikwisha baada ya kujiunga na washindani wake

JOSE  Mourinho amesema mapenzi ya Frank Lampard kwa Chelsea yamekwisha baada ya jana kuifungia Manchester City bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi uwanja wa Etihad.
 
Nyota huyo mwenye rekodi ya kufunga mabao mengi kwa muda wote Chelsea, alitokea benchi na kuiadhibu timu yake hiyo ya zamani, lakini Mourinho aligoma kukubali kuwa mchezaji huyo anayecheza kwa mkopo Man City ana mapenzi ya kweli kwa Chelsea.
 
Alisema: "Frank ni mchezaji wa Man City, siamini hadidhi zake na mapenzi ya moyoni kwake, labda mimi ni mshamba wa mpira"
"Alipoamua kwenda kwa washindani wa moja kwa moja na Chelsea, mapenzi kwa timu yalikwisha. Alifanya kazi yake kiuweledi.
 
"Alipokelewa vizuri England na hii ndio England na hii ndio Chelsea. Watu wa Chelsea kamwe hawasahau kile watu wa Chelsea walifanya".
 
"Iliwahi kunitokea hata mimi  nikiwa kocha wa Inter. Ni utamaduni na uzuri wa Chelsea".

CHADEMA IRINGA YATANGAZA MAANDAMANO YA AMANI JUMATATU, POLISI WAYAPIGA MARUFUKU


Frank Nyalusi Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini
Kama kawaida salamu za chama hicho za Peopleziii zilisika
Mlemavu huyo aliuliza swali katika mkutano huo akitaka kujua kati ya Samwel Sitta na Rais jakaya Kikwete ni nani ana madaraka makubwa zaidi kuhusu mchakato wa Katiba
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Iringa Mjini, kimetangaza kufanya maandamano ya amani LEO Jumatatu ikiwa ni hatua ya kuitikia wito wa mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wa kufanya maandamano hayo nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba.

Mwenyekiti wa Chadema wa Iringa Mjin, Frank Nyalusi alitoa tangazo hilo jana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika mtaa wenye machinga wengi maarufu kama Magari Mabovu, Kitanzani.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na vijana kadhaa huku ukiwa umezungukwa na askari Polisi kila kona, Nyalusi alisema “wapende wasipende, kesho tutafanya maandamano, tunaomba Polisi washiriki kulinda usalama wetu, kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani.”

Alisema maandamano hayo yanalenga kupeleka ujumbe wa kusitishwa kwa mchakato wa bunge hilo kwa kuwa hauna maridhiano na fedha zitakazonusurika zitumike katika shughuli zingine za kijamii.

“Hatuwezi kupata Katiba kwa staili hiyo, tumemuomba Rais asitishe mchakato huo lakini tumepuuzwa na sasa tunadhani ni zamu ya watanzania wote kupaza sauti zao ili bunge hilo lisitishwe,” alisema.

Alipoulizwa baadaye maandamano hayo yataanzia wapi, Nyalusi hakuwa tayari kutaja ni eneo gani yataanzia kwa kile alichosema hawataki wapinzani wao wajue.

Kabla ya kutangazwa kwa maandamano hayo ya kesho jumatatu, jeshi la Polisi liliripotiwa na chama hicho kuwazuia kufanya maandamano kama hayo Jumamosi iliyopita.

Badala yake kwa mujibu wa Nyalusi, jeshi hilo liliwaruhusu kufanya mkutano wa hadhara katika eneo hilo la Magari Mabovu.

Katika mahojiano na gazeti hili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema jeshi lake halijapokea maombi ya maandamano hayo kutoka katika chama hicho.

 Aliwataka wafuasi wa chama hicho kuzingatia sheria, taratibu na kanuni wakati kikipanga na kufanya mambo yake.

Akitoa ufafanuzi huo kwa njia ya simu, Mungi alisema; “nchi hii kama zilivyo nchi nyingine inaendeshwa kwa sheria. Kwahiyo watu binafsi, serikali, vyama vya siasa na wengine wote ni lazima wazingatie hilo.”

Alisema mji wa Iringa upo shwari na kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana na hali yoyote ile itakayoonekana inataka kuhatarisha amani.
 
CREDIT:FRANCIS GODWIN

MANCHESTER CITY YATOSHANA NGUVU NA CHELSEA


IMG_7407.JPG
Baada ya Man United kupokea kipigo kutoka kwa Leicester City, miamba mingine ya ligi kuu ya Uingereza Chelsea ilijitupa uwanjani kucheza na Manchester City.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad umeisha kwa matokeo ya sare 1-1.Dakika chache baada ya Pablo Zabaleta kutolewa kwa kadi nyekundu Chelsea walipata goli la kwanza kupitia mchezaji aliyetokea benchi Andry Schurrle.
Akitokea benchi mchezaji wa zamani wa Chelsea Frank Lampard aliunganisha krosi ya James Milner na kuisawazishia Man City.
Mpaka mpira unamalizika Man City 1-1 Chelsea.

VAN GAAL AKUBALI KUPOTEZA MECHI

VAN GAAL

Louis van Gaal amesema timu yake ya  Manchester United imepoteza pointi tatu muhimu baada ya kuchapwa mabao 5-3 na Leicester City.

Manchester ilianza kwa kuwa mbele kwa mabao mawili lakini cha ajabu mabao hayo yalirudishwa na kuongezwa mengine katika kipindi cha pili na kuiacha Manchester United ikiendelea kupata uhaba wa ushindi.

“Van Gaal amesema huezi kuamini kuwa unaongoza kwa mabao 3-1 na upo mbele kwa goli mbili zaidi katika kipindi cha kwanza,tulitakiwa kumaliza mchezo kwa ushindi lakini tulishindwa kufanya hivyo,tulitengeneza nafasi nzuri na tukashinda magoli  mazuri lakini hayakudumu kwa dakika zote 90 tulizocheza uwanjani",amesema Van Gaal.

Mchezo ulianza kuwageukia Manchester United pale muamuzi wa mchezo Mark Clarrenburg alipowapa penati baada ya Reafael kumfanyia madhambi Jamie Vardy katika eneo la penati ambayo Van Gaal alikataa kusema chochote kuhusu maamuzi hayo ya mwamuzi.

"wakati matokeo yanasomeka 3-2 hakukuwa na tatizo,tulidhani tutaumaliza mchezo kwa ushindi,tutautawala mchezo wote ambao tuliutawala katika dakika zote kumi za mwanzo na kufunga mabao maridadi,lakini hatukuwa makini tukaupoteza mchezo" alisema Van Gaal.

Hadi mwamuzi Mark Clarrenburg anapuliza kipyenga cha mwisho,Manchester United ilikuwa imelala kwa mabao 5-3.

TUMERUDI TENA HEWANI

BAADA YA KUKAA KIMYA KWA MUDA MREFU BLOG HII ILIKUWA KIMYA KUTOKANA NA SABABU MBALI MBALI ZA KIUFUNDI.TUNAOMBA RADHI KWA WALE WOTE WALIOKUWA WANAIFUATILIA NA KOKOSA TAARIFA MBALI MBALI KUTOKA KWENYE BLOG HII,KUANZIA SASA UTAENDELEA KUPATA HABARI NA MATUKIO MOTO MOTO NDANI NA NJE YA NCHI,KARIBUNI TENA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...