Saturday, July 19, 2014

NDEGE NDOGO YATUA BARABARANI KWA DHARULA NCHINI UGANDA BAADA YA KUISHIWA MAFUTA


Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dhalura katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
 Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Philip Mukasa, amesema kuwa ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Sudani ya Kusini.

Rubani wa ndege hiyo aliamua kutua katikati ya barabara baada ya kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha, ambapo aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe na kuamua kutua kwa dharura kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.

Katika dharura hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa, na watu wote wametoka salama.

Haikuweza kufahamika kwa haraka sababu zilizomfanya rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.

BARAZA LA USALAMA LAKUTANA KUHUSU UKRAINE KUFUATIA AJALI YA NDEGE


BARAZA LA USALAMA WAKATI WA DAKIKA MOJA YA UKIMYA KUWAKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA YAO KWENYE AJALI YA NDEGE

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali nchini Ukraine, kufuatia ajali ya ndege ya Malaysia hapo jana mashariki mwa Ukraine, kwenye eneo linalodhibitiwa na waasi. Taarifa kamili na Amina Hassan
(Taarifa ya Amina)
Mwanzoni mwa mkutano wa leo, Rais wa Baraza la Usalama, Richard Gasana, amewasilisha ujumbe wa rambirambi za wanachama wake kwa familia za wahanga wa ajali hiyo, na serikali za nchi zilizopoteza raia wao
GASANA
"Naomba nyote msimame na kubaki kimya kwa dakika moja, kuwakumbuka waliopoteza maisha yao"
Akizungumza kwenye mkutano huo, Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman wakati hali inaendelea kuzorota kwa kasi nchini Ukraine, inasikitisha kuwa mwanga wa matumaini ulioonekana baada ya kutangazwa mpango wa Rais Poroshenko wa amani, ukiwemo usitishaji mapigano, sasa umedidimia haraka. Kuhusu baa la ndege ya Malaysia, ambalo chanzo chake bado hakijathibitishwa, Bwana Feltman amesema
"Katibu Mkuu amesikitishwa na ripoti zinazoonekana kuwa za kuaminika kuwa kombora la kurushwa angani lilitumiwa. Katibu Mkuu analaani vikali hiki kinachoshukiwa kuwa utunguaji wa kukusudia wa ndege ya kiraia. Tukio hili la kutia hofu ni ukumbusho wa jinsi hali mashariki mwa Ukraine ilivyo mbaya mno, na jinsi inavyoathiri nchi na familia nje ya mipaka ya Ukraine."

ANGALIA PICHA ZA WATUHUMIWA 16 WANAODAIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UGAIDI WAKIPANDISHWA KIZIMBANI NCHINI.

ASKARI WA KUTULIZA GHASIA FFU PAMOJA NA WA MAGEREZA WAKIWEKA ULINZI MKALI WAKATI WATUHUMIWA WA UGAIDI WAKIFIKISHWA MAHAKAMANI


Baadhi ya watuhumiwa wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi  
Monday, July 14, 2014

SHAKIRA, WYCLEF WALIVYOWASINDIKIZA GERMANY KUTWAA KOMBE LA DUNIA 2014 JANA USIKU


Mshambuliaji wa German Mario Goetze (kushoto) akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake dhidi ya Argentina, katika dakika za nyongeza fainali za Kombe la Dunia jana usiku. German ilishinda bao 1-0

TIMU ya Germany, jana usiku imeibuka mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Dunia 2014 'FIFA World Cup', baada ya kuifunga Argentina kwa bao 1-0, katika mchezo wa Fainali za Kombe la Dunia uliochezwa kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 bila ya kufungana na kuongezwa dakika 30 ambapo German iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1 lililofungwa na MARIO GOETZE, katika dakika ya 22 kati ya dakika 30 za nyongeza bao lililodumu hadi kumalizika kwa dakika hizo za nyongeza.

Germana wameweza kutwaa Kombe hilo kwa mara ya nne sasa tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo ambapo kwa mara ya kwanza ililinyakuwa mnamo mwaka 1954, 1974, 1990 na hatimaye 2014.
Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Hispania, Carles Puyol, akipozi mbele ya Kombe la Dunia na Mwanamitindo wa Brazil, Gisela Bundchen baada ya kombe hilo kuwasili uwanjani hapo jana kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG JIJINI MBEYA.


Kutoka kushoto ni Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali katikati ni Rais Dkt Jakaya Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro , wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya Sherehe kuanza Rasmi.
 Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali  akitoa salam za Shukurani kwa Mgeni Rasmi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pia kutoa Historia ya kanisa la TAG toka lilipoanza mpaka sasa linatimiza Miaka 75.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya  Julai 13, 2014
 Baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali wakiwa katika maadhimisho hayo 
 Charles Mwakipesile akiwatunza watoto baada ya kusoma Bibilia kwa umakini kutoka kichwani
 Sherehe zimepamba moto
 Baadhi ya Wageni waalikwa kutoka Nje ya nchi waliokuja kuhudhuria Miaka 75 ya TAG
 Ankali Issa Michuzi katika Sherehe hizo za Miaka 75 ya TAG
 Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali katikati akiwa anazungumza jambo wakati walipokuwa wakijiandaa kutoa zawadi mbalimbali.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya  Julai 13, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
 Baadhi ya wadau
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Kanisa la TAG kutoka Marekani 
 Watoto wakitoa Burudani 
Picha ya Pamoja baada ya Sherehe kumalizika
Picha zote na Mbeya yetu.

Wednesday, July 2, 2014

IDADI YA WATU WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MIZIGO JOMO KENYATTA LEO ALFAJIRI WAFIKIA WA254
Askari wa Jeshi la Kenya wakiwa eneo la tukio wakijaribu kutoa msaada katika Ndege ya mizigo iliyoanguka leo asubuhi katika eneo la Utawala kwenye Uwanja wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa mpaka sasa imefahamika kuwa jumla ya watu wanne akiwamo Rubani, waliokua kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufa baada ya ndege hiyo kuanguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye uwanja huo ikielekea Moghadishu, Somalia.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo ambapo imeelezwa kuwa ndege hiyo ilikua iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyinginezo kuelekea Somalia.
Akithibitisha ajali hiyo Mkuu wa Polisi wa Jiji la Nairobi, Benson Kibue, amesema kuwa kuwa Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET ilianguka kwenye paa la jengo la kibiashara wakati likijaribu kutua ghafla baada ya kutokea hitilafu katika ndege hiyo na kushika moto kisha kuanza kuteketea na watu wanne waliokua ndani.
Aidha kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Jijini Nairobi, Benson Kibue, amesema kuwa katika ajali hiyo walinzi wawili walijeruhiwa mmoja ametibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku mmoja akilalazwa katika hospitali ya Mama Lucy.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kwenye mabaki ya ndege hiyo kuona iwapo kuna waathirika zaidi.

Saturday, June 21, 2014

WATU SITA WAMEFARIKI PAPO HAPO KATIKA AJALI BARABARA YA BAGAMOYO ENEO LA MAKONGO JIJINI DAR ES SALAAM

BAADHI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI HIYO

HALI ILIVYOKUWA ENEO LA AJALI

MOJA YA BASI LILOHUSIKA KATIKA AJALI

HII NDIYO HALI HALISI ENEO LA AJALI

ENEO LA AJALI

Watu sita wamekufa papo hapo na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne yakiwemo mawili ya abiria iliyotokea eneo la Makongo barabara ya bagamoyo jijini Dar es Salaam leo saa saba mchana.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea wakati dereva wa gari la abiria lililokuwa likielekea Mwenge kutoka Tegeta ambaye alikuwa katika mwendo wa kasi kubwa kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa pili wa barabara na kuligonga basi lingine la abiria lililokuwa likitokea Mwenge kuelekea Tegeta.

Akielezea ajali hiyo,kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi kinondoni kamanda AWADH HAJI amesema ajali hiyo ilitokea saa saba mchana na kuhusisha magari manne moja likiwa la raia wa China ambalo liliwakanyaga majeruhi na kuwaua sita kati yao.

Mganga Mkuu wa hospiitali ya jeshi Lugalo ambako maiti na majeruhi walipelekwa brigedia jenerali Dr Makere Josiah amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita huku wengine hali zao zikiwa mbaya na kukimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

TAZAMA PICHA ZA BABU SEYA NA MWANAE PAPII KOCHA WAKITUMBUIZA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA

NGUZA VICKING AKILICHARAZA GITAA HUKU PAPII AKIIMBA

PAPII KOCHA AKICHEZA KWA MADAHA
PAPII KOCHA AKIIMBA HUKU BABA YAKE NGUZA VICKING AKIPIGA GITAA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA YALIYOFANYIKA KATIKA BWALO LA MAGEREZA SIKU YA IJUMAA 20/06/2014 DAR ES SALAAM

PAPII AKITUMBUIZA NA WAFUNGWA WENZIE

PAPII AKIIMBA KWA HISIA WIMBO MAALUM WA SIKU YA MAGEREZA

PAPII AKIMUANGALIA BABA YAKE ANAVYOLICHARAZA GITAA

NGUZA VICKING NA MWANAE WAKITUMBUIZA

PAPII KOCHA MTOTO WA MFALME


Monday, March 10, 2014

WATAALAMU WA USALAMA WA ANGA WATOA SABABU ZINAZOHISIWA ZIMESABABISHA NDEGE YA SHIRILA LA NDEGE LA MALAYSIA KUANGUKANDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA BOING 777 ILIYOPOTEA NA MPAKA SASA HAIJULIKANI ILIPO IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200


WATAALAM WA VIETNAM WAKIWA KATIKA NDEGE KUFUATILIA ENEO AMBALO WANAHISI NDEGE HIYO ILIANGUKA

SEHEMU HII INAONYESHA MAFUTA YAKIWA YANAELEA WATAALAM WA VIETNAM WANAHISI IMEANGUKIA HAPA
SEHEMU INAPOHISIWA KUWA NDEGE YA MALAYSIA IMEANGUKA

WAPENZI HAWA WALIKUWEMO KATIKA NDEGE HIYO NA INAHOFIWA WAMEPOTEZA MAISHA

MOJA YA FAMILIA YA WATU WALIOSAFIRI NA NDEGE HIYO

NDUGU WA ABIRIA AKILIA KWA UCHUNGU MARA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA KUPOTEA KWA NDEGE HIYO

WAZAZI HAWA MAMA MWENYE SURUALI NYEUSI NA BABA MWENYE JAKETI JEUSI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIJANA WAO NA MPENZI WAKE KABLA YA KUONDOKA KUALA LUMPUR NA NDEGE ILIYOPOTEA

 Wataalam wa masuala ya anga wanasema wakati mgumu na tete kwa ndege yeyote ni wakati inataka kuruka au kutua,mara chache sana matukio yasiyokuwa ya kawaida huwa yanatokea pale ndege inapokuwa angani umbali wa takribani mile saba sawa na kilometa 11 kutoka usawa wa ardhi.
  

Kwa  hiyo kwa kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysi awakati ikiwa angani siku ya Jumamosi asubuhi ikiwa na abiria zaidi ya 200 katika bahari ya kaskazini mwa China,imefanya wataalamu wa masuala ya anga kubaini kwamba chochote ambacho kitakuwa kimetokea basi kitakuwa kimetokea ghafla na kwa haraka mno kiasi cha kumfanya hata rubani wa ndege hiyo kushindwa kupiga simu ya dharula. 


Inaweza ikachukua miezi au hata mwaka kwa wachunguzi wa ajali za ndege kubaini kile kilichotokea kwa ndege hiyo ya shirika la ndege la Malaysia boing 777 iliyoruka kutoka mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur kuelekea China.


Mmoja kati ya wachunguzi hao wa ajali za ndege bw Todd Curtis ambae ni mhandisi wa masuala ya ndege mstaafu,amesema katika hatua ya awali kabisa ya uchunguzi wao wanajitahidi kutafuta ukweli wa mambo ambayo mpaka sasa hawayajui.Todd ameshafanya kazi kwenye ndege hiyo boing 777 na sasa ni mkurugenzi wa taasisi moja ya usalama wa ndege huko Malaysia Airsafe.com foundation.


Radar ya jeshi imebashiri kwamba ndege hiyo iliyopotea Boing 777 inaweza kuwa iligeuza safari iliyokuwa imeianza kabla ya kupotea,Mkuu wa shirika la ndege la Malaysia amesema siku ya Jumapili kwamba mamlaka inachunguza abiria wanne ambao utambulisho wao unamashaka.Hii itaonyesha mazingira yalivyokuwa katika dakika za mwisho kabla ndege haijapata ajali.Mkuu wa shirika la ndege hakubainisha muelekeo wa ndege hiyo kabla ya ndege hiyo kupoteza uelekeo au ilikwenda umbali gani kabla ya kupotea ila baadhi ya taarifa zinatafutwa kwa kushirikiana na radar ya mtu binafsi.


Kama zikipatikana taarifa sahihi kuwa ndege hiyo iligeuza na kurudi ilikotoka kabla ya kupotea,basi kuna uwezekano mkubwa kuwa ndege hiyo ilikubwa na tatizo kubwa wakati ikiwa angani lakini maswali mengi yanaibuka kwa nini rubani hakutoa ishara yeyote katika chumba cha kuongozea ndege ili apate msaada.Kama kulikuwa na matatizo kidogo ya kiufundi au engine zote mbili za ndege zilizima,rubani lazima angekuwa na muda wa kupiga radio ya upepo,Kutokupiga kwake radio ya upepo kunatoa picha kwamba kuna kitu cha ghafla mno kilitokea hadi akashindwa kufanya chochote, alisema William Waldock ambae anafundisha masuala ya uchunguzi wa ajali za ndege katika chuo cha Embry-Riddle Aeronautical Arizona.


Inawezekana kuwa aidha lilitokea tatizo la ghafla au kitu cha haraka kilichosababisha ikaanguka.Baadhi ya wataalam wanadhani inawezekana pia likawa ni tukio la ugaidi au rubani akawa ameiangusha kwa makusudi.

Haijalishi tukio hili limetokea kwa namna gani,lakini ni mapema mno kusema kitu halisi kilichotokea,Kitu cha msingi ni kusubiri mabaki ya ndege hiyo yatakapopatikana na kupatikana kwa kisanduku kinachohifadhi sauti na uchunguzi wa tatizo.Wachunguzi wa kimarekani kutoka FBI,Bodi ya usafiri Salama ya taifa na shirikisho la uongozi wa anga, na wataalam wa ndege aina ya Boeing wote wameelekea Asia kusaidia uchunguzi huo.

Utafutaji wa hali ya juu umeshafanyika baharini lakini mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa kupatikana kwa ndege hiyo,ingawa Serikali huko Vietnam imesema kuwa Jumapili jioni ndege yao ilikuwa inapita chini chini katika bahari iliona kitu kama cha pembe tatu kilomita karibu 90 sawa na mile 56 kusini mwa kisiwa cha Tho Chu,sehemu hiyo hiyo ambayo mafuta yameonekana yakielea siku ya Jumapili,lakini gazeti la serikali limesema mkuu wa jeshi msaidizi wa Vietnam amekaririwa akisema kitu hicho kilichoonekana baharini ni mlango wa ndege.
Baadhi ya mambo yanayohisiwa kuwa yamesababisha ndege hiyo kupotea ni  muundo wa umbo la ndege ambao ni Alluminium,hali mbaya ya hewa,Rubani kutotambua tatizo mapema,kuzima au kushindwa kufanya kazi kwa ingini zote mbili za ndege,kupigwa bomu au kutekwa hizi ni baadhi ya sababu zinazohisiwa na wataalamu wa ajali za ndege na usalama wa anga kuwa zimesanbabisha ndege hiyo kupotea.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...