Tuesday, October 21, 2014

OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA


Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kwa kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi wa pili mwaka jana.Pia amehukumiwa miaka mitatu kwa kosa la kutumia vibaya silaha aliyokuwa anaimiliki kisheria lakini hukumu hiyo imesimamisha na badala yake atatumikia miaka mitano yote kwa pamoja.
oscar 2 oct 21 
Hukumu hiyo imetolewa na jaji mwanamama Thokozile Masipa baada ya kusikiliza kwa makini na kupima hoja za kila upande dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mwanariadha huyo wa Afrika kusini.


Pia hukumu ya miaka mitatu imetolewa baada ya kuitumia bastola kinyume na sheria pale alivyoifyatua chini ya meza kwenye mgahawa wa Tasha uliopo Johannesburg mwezi January mwaka 2013,mwezi mmoja kabla hajamuua mpenzi wake siku ya wapendanao february 14,2013.

HUKUMU ILIVYOSOMWA

Katika hukumu yake,jaji Masipa alianza kusoma mwenendo mzima wa kesi jinsi ilivyokuwa inaendeshwa na hoja mbali mbali kutoka upande wa mashtaka na upande wa utetezi katika mahakama kuu mjini pretoria Afrika kusini.

Pistorius amepatikana na hatia ya kuua bila ya kukusudia mwezi uliopita baada ya kusababisha kifo cha Reeva Steenkamp pia kutumia sdilaha kinyume cha sheria tukio ambalo alilifanya kwa nyakati tofauti na lile la mauaji.

Jaji Masipa alisema wakati wa kuendesha mwenendo mzima wa kesi hiyo alikuwa na washauri wawili waliokuwa wanamsaidia katika kupima kila hoja zilizokuwa zinatolewa na pande mbili,lakini uamuzi wa hukumu ni wakwake yeye binafsi.

Alisema wakati mwingine kupata hukumu stahiki ni vigumu sana tatizo ambalo linazikabili mahakama nyingi zinazoendesha makosa ya jinai.


Masipa amesema kabla ya hukumu,upande wa utetezi ulipeleka mashahidi wanne wakatoi upande wa mashtaka uliita wawili tu katika kuthibitisha mashtaka waliyoyawasilisha mbele ya mahakama.

Akielezea ushuhuda wa daktari wa saikolojia Dr Löre Hartzenberg alisema kuwa alikuwa akimtibu Pistorius tangu alipofanya mauaji hayo mwezi february mwaka jana.
.

Hartzenberg alisema mahakama haina budi kuzingatia maisha ambayo amekuwa nayo mara baada ya tukio,kwani alipoteza marafiki,hakuweza kuendelea na kazi yake,na alikuwa ameathirika kisaikolojia.

Masipa alisema shahidi wa pili  Joel Maringa, ambae ni afisa ustawi wa jamii alipendekeza Pistorius angekuwa kwenye kifungo cha ndani lakini nyumbani kwake kwa miaka mitatu na kufanya kazi za kijamii kwa masaa yasiyopungua 16 kwa mwezi.

Meneja wa Pistorius Peet van Zyl, alikuwa ni shahidi wa tatu aligusua kuhusu matembezi ya hisani aliyopanga kuyafanya kuhusu kazi aliyokuwa anaifanya.

Ushahidi wa Van Zyl ulisema kwamba kabla hajamuua mpenzi wake kwa risasi,Pistorius alikuwa anaheshimika kama mwanamichezo mahiri ulimwenguni,amabae alitumia muda na pesa zake katika mambo mengi ya msingi.

Kwa mujibu wa  Van Zyl, amesema fursa ya pistorius kushiriki kwenye mambo yote hayo imesimamishwa tangu kifo Steenkamp

Shahidi wa nne ambae pia ni afisa ustawi wa jamii Annette Vergeer, ambae alitumia muda mwingi kuelezea hali mbaya na tete ya magereza ilivyo nchini humo.

Ameiambia mahakama kuwa jela za nchini humu hazikidhi mahitaji maalum ya Pistorius kulingana na hali yake.

Kwa upande wa mashahidi wa mashtaka dhidi ya Pistorius wa kwanza alikuwa ni binamu yake marehemu Steenkamp Kim Martin,ambae alielezea kwa undani kazi za mwanamitindo huyo marehemu pamoja na maisha yake binafsi yalivyokuwa.


Martin aliiambia mahakama jinsi Steenkamp alivyokuwa karibu saana na wazazi wake,Barry na June na aliwasaidia sana kifedha na walikuwa wakimtegemea kwa kila kitu.Jaji Masipa alibaini jinsi gani Martin alivyokutana na Pistorius kwa mara ya kwanza mwezi mmoja kabla ya kifo cha Steenkamp.Martin alikumbusha mahakama kuhusu taharuki iliyoikumba familia yao baada ya kupata taarifa ya kifo cha ndugu yao.

Alisema hali ya afya ya baba mzazi wa Steenkamp, Barry ilikuwa mbaya kwani alikuwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha mwanae.

Shahidi wa mwisho kwa upande wa mashtaka alikuwa ni kaimu mkurudenzi wa taifa idara huduma urekebishaji tabia Zac Modise alisema mfumo wa jela za nchi hiyo ni mzuri na unaweza kumhifadhi Pistorius.


Jaji Masipa aligusia namna upande wa utetezi ulivyotoa hoja kuwa Pistorius asiende jela kwa kuwa anahitaji msaada wa matibabau ya kisaikolojia na akakubaliana na hoja ya shahidi wa mashitaka bwana Modes kuwa huduma za aina hiyo zinapatikana na mwanariadha huyo anaruhusiwa kumpeleka daktari wake huko jela akamtibie.

alisema hata wanawake wajawazito ni kundi ambalo lina mazingira magumu sana kwenye jamii,na walikuwa wanakwenda jela na idara za amgereza ziliweza kuwahudumia vyema,hivyo haitakuwa vyema kwa sheria iwatazame kwa umuhimu wa kipekee watu wenye pesa na maarufu huku upande mwingine wa watu masikini waachwe.

Masipa anaamini kwamba upande wa utetezi umeegemea sana katika hoja zake kuhusu hali ya ulemavu aliyokuwa nayo Pistorius,lakini akasema ukiyaangalia maisha ya Pistorius hasa ya kazi yake alikuwa anashindana pia na watu wazima na alikuwa anashinda.

alisema hukumu yake imepangwa kuonyesha hali halisi ya Pistorius,kuwa aliweza kubadili mtazamo hasi wa watu dhidi ya ulemavu ana aliwavutia wengi hasa vijana,amesema jambo hili halitapuuzwa kamwe litaheshimiwa na kubaki kuwa hivyo japo meneja wake alisema akifungwa haya mambo yote aliyokuwa anafanya kwenye jamaii yatasimama.

Masipa anaamini  Pistorius anajutia kwa kile alichokifanya kutokana na ushahidi kwamba  alijaribu kuwatafuta wanafamilia wa Steenkamp kwa siri na kuwaomba radhi.


Baadae alimuamrisha Pistorius kusimama kisha akamhukumu miaka mitano jela kwa kuua bila kukusudia na miaka mitatu kwa kosa la pili ila ataitumikia yote kwa pamoja na miaka miwili inaanza sasa akiwa jela.

Pistorius baada ya hukumu aliweza kuwapa mikono baadhi ya wanafamilia wake kabla ya kupanda karandinga kwenda jela.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...