Tuesday, February 17, 2015

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 13 ASIMIKWA RASMI KUWA CHIFU WA WAHEHE

Mwanafunzi wa darasa la saba Adam Abdul Sapi Mkwawa(13) ametawazwa rasmi kuwa chifu wa kabila la wahehe kufuatia kifo cha baba yake mzazi Abdul Sapi Mkwawa(66).

Rais Jakaya Kikwete alikuwa ni mmoja kati ya watu waliohudhuria maziko ya Chifu Abdul Sapi Mkwawa katika kijiji cha Kalenga mkoani Iringa na baadae kushuhudia kusimikwa kwa chifu huyo mpya wa kabila la wahehe Adam.

 Kusimikwa kwa mtoto huyo anayesoma katika shule ya msingi Highland iliyopo mkoani Iringa kutasubiri hadi atakapotimiza miaka 20 ndiyo ataanza kutumikia wadhifa huo wa uchifu ambapo kwa sasa wadhifa huo utashikiliwa kwa muda na mdogo wa marehemu Salehe hadi hapo Adam atakapotimiza umri huo(20).
Chifu mpya wa kabila la wahehe Adam Abdul Sapi Mkwawa

Rais Jakaya Kikwete akimfariji Chief Adam Abdul Sapi Mkwawa
Wazee wz kimila wakimsimika Adam Abdul Sapi Mkwawa kuwa chifu mpya wa kabila la wahehe siku mbili baada ya kifo cha baba yake Abdul Adam Sapi Mkwawa aliyekuwa chifu wa kabila hilo


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...