Thursday, August 6, 2015

BREAKING NEEEEEWS. HATIMAYE PROF LIPUMBA AACHIA NGAZI RASMI NAFASI YAKE YA UENYEKITI KATIKA CHAMA CHA WANACHI CUF

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Haruna Lipumba
Hatimae mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF professor Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti katika chama cha wanachi CUF. 

Prof Lipumba amesema ameamua kuachia nafasi hiyo na kuwa mwanachama wa kawaida kwa kuwa hakubaliani na wenyeviti wenza wa UKAWA kwa kuwakubali wanachama wa chama cha mapinduzi waingie UKAWA ikizingatiwa kuwa watu hao walishiriki katika kuipitisha katiba inayopendekezwa ambao yeye na wenzake waliipinga kwa nguvu zote.

Amesema dhamira yake imemsuta hivyo hawezi kuendelea kuwepo katika nafasi hiyo na hivyo ameamua kuwa mwanachama wa kawaida.

Prof Lipumba ametangaza azma yake hiyo katika ukumbi wa hoteli ya PEACOCK jijini Dar es Salaam na aliwasili hotelini hapo akiwa na watu wengine kabisa tofauti na ilivyokawaida kuwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na alikuwa kavalia mavazi ya kawaida tofauti na inavyokuwa siku zote ambapo huwa anavalia mavazi ya chama hicho.

Iliripotiwa jana kuwa prof Lipumba alitaka kutangaza adhma yake hiyo jana katika ofisi za chama hicho Buguruni Dar es Salaam lakini azma hiyo ilizimwa na wazee na baadhi ya wafuasi wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...