Wednesday, October 29, 2014

RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIARais wa Zambia Michael Sata amefariki dunia nchini uingereza alikokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa ambao mpaka kifo chake haijawekwa wazi kuwa alikuwa anaumwa nini.

Rais Sata ambae alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mfalme Edward VII amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 77.

Taarifa zinasema rais huyo wa Zambia aliaga dunia baada ya mapigo ya moyo kupanda ghafla.

Hakuna taarifa ya mara moja juu ya mtu atayemrithi Rais Sata,suala hilo litaamuliwa na baraza la mawaziri la nchi hiyo linalotarajia kukutana leo Jumatano asubuhi.

akitangaza kifo cha rais huyo,katibu wa baraza la mawaziri Roland Msiska kwenye televisheni ya taifa ya nchi hiyo,alisema kwa masikitiko na mshtuko mkubwa,natangaza kifo cha rais wetu mpendwa Michael Sata.

Aliongeza kwa kusema kuwa mke wake na mtoto wake wa kiume walikuwa pembeni yake wakati rais huyo anakata roho.

Akawataka wazambia wote kuwa watulivu,wamoja kwa kipindi hiki kigumu cha msiba uliolikumba taifa hilo.

kifo cha Rais Sata kimekuja siku chache baada ya Zambia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waingereza.

Rais Sata anakuwa Rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani mwingine alikuwa ni Levy Mwanawasa alifariki dunia mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...