Monday, September 22, 2014

VAN GAAL AKUBALI KUPOTEZA MECHI

VAN GAAL

Louis van Gaal amesema timu yake ya  Manchester United imepoteza pointi tatu muhimu baada ya kuchapwa mabao 5-3 na Leicester City.

Manchester ilianza kwa kuwa mbele kwa mabao mawili lakini cha ajabu mabao hayo yalirudishwa na kuongezwa mengine katika kipindi cha pili na kuiacha Manchester United ikiendelea kupata uhaba wa ushindi.

“Van Gaal amesema huezi kuamini kuwa unaongoza kwa mabao 3-1 na upo mbele kwa goli mbili zaidi katika kipindi cha kwanza,tulitakiwa kumaliza mchezo kwa ushindi lakini tulishindwa kufanya hivyo,tulitengeneza nafasi nzuri na tukashinda magoli  mazuri lakini hayakudumu kwa dakika zote 90 tulizocheza uwanjani",amesema Van Gaal.

Mchezo ulianza kuwageukia Manchester United pale muamuzi wa mchezo Mark Clarrenburg alipowapa penati baada ya Reafael kumfanyia madhambi Jamie Vardy katika eneo la penati ambayo Van Gaal alikataa kusema chochote kuhusu maamuzi hayo ya mwamuzi.

"wakati matokeo yanasomeka 3-2 hakukuwa na tatizo,tulidhani tutaumaliza mchezo kwa ushindi,tutautawala mchezo wote ambao tuliutawala katika dakika zote kumi za mwanzo na kufunga mabao maridadi,lakini hatukuwa makini tukaupoteza mchezo" alisema Van Gaal.

Hadi mwamuzi Mark Clarrenburg anapuliza kipyenga cha mwisho,Manchester United ilikuwa imelala kwa mabao 5-3.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...