Tuesday, September 17, 2013

SIMBA AUA MFANYAKAZI WA HIFADHI

SIMBA ANAEJULIKANA KWA JINA LA KENENISA BAADA YA KUMUUA ABERA MFANYAKAZI WA HIFADHI
Simba amemuua Abera Silsay (51),katika sehemu ya kutunzia wanyama pori ambao wanafugwa katika sehemu hiyo kwa ajili ya utalii huko Addis Ababa,Ethiopia.

Taarifa zinasema simba huyo alimvamia Abera baada ya kusahau kuufunga mlango wa sehemu simba huyo anapolala.

Abera aliuawa na simba huyo anaejulikana kwa jina la Kenenisa wakati akisafisha banda namba 10 analolala simba huyo kutokana na kusahau kuufunga mlango ndipo simba huyo alipotoka kumvamia na akamuangusha chini huku akimng'ata sehemu yake ya shingoni.

Mkurugenzi mkuu wa hifadhi hiyo bw Musie Kiflom amesema walinzi wa hifadhi hiyo walijaribu kupiga risasi hewani ili kumtisha simba huyo lakini jitihada zao ziligonga mwamba.

Taarifa zinasema hii ni mara ya pili kwa simba kuua muhudumu wa hifadhi kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 17 iliyopita katika hifadhi hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema wameamua kuchuklua hatua ya kuzidi kuwapa elimu wafanyakazi hao wa hifadhi namna ya kuwalinda wanyama,kuishi nao, kuwahudumia kwa kuwapa chakula na kuwasafisha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...