Wednesday, September 18, 2013

RAIS KIKWETE AMTEUA BI JACQUELINE MALEKO MKURUGENZI MKUU TANTRADE

Bi.Jacqueline Maleko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi.Jacqueline Mneney Maleko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue,uteuzi huo ulianzia September 10,mwaka huu,2013.

Kabla ya uteuzi huu,Bi.Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Masoko, Wizara ya viwandana Biashara,kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa (TANTRADE).


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
DAR ES SALAAM.

18 SEPTEMBA, 2013

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...