Wednesday, September 18, 2013

JELA MIAKA 2 KWA MAUAJI YA BILA KUKUSUDIA

 Steven Augustino wa Demashonews, Tunduru
 
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma kupitia Vikao vinavyo
endelea Wilayani Tunduru Imemuhukumu Kifungo cha Miaka Miwili Jela
Manywele Abdalah Ausi (35) baada ya kutia hatianai katika kosa dogo la
kuua bila kukusudia kinyume cha sheria kifungu namba 195 sura ya 16
cha kanuni ya adhabu kama ilivyo fanyiwa makebisho mwaka 2002.

Manyele aliye kuwa anakabiliwa na Shauri la mauaji  ya kukusudia Namba
Rm 16/2012 alidaiwa kuwa alimuua marehemu bakari Mohamed Komando
katika tukio la ugomvi wa kugombea deni la shilingi 2000 lilitokea
Januari 8 /2012 katika kijiji cha Chikomo mashambani  Wilayani humo.

Alisema baaya ya kusomewa Shitaka hilo ambao mtuhumiwa Manywele
akikanusha ,Wakili wa utetezi Dickson Pius Ndunguru aliiomba mahakama
mteja wake kuwa yuko tayari kukili kosa dogo la kuuwa bila kukusudia
ombi ambalo halikupigwa na upande wa mashtaka na ndipo mahakama baada
ya kusomiwa kosa hilo ilipo mtia hatihani kwa kosa dogo la kuuwa bila
kukusudia.

Akifafanua hukumo hiyo Jaji anayesikiliza Kesi hizo Njingafibili
Mwaikugile alisema kuwa adhabu hiyo Pamoja na mambo mengine mahakama
hiyo imezingatia hoja za wakili wa utetezi Dickson Ndunguru aliyeiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu ndogo kwa mteja wake kwavile ni mkosaji wa
mara ya kwanza hivyo alijikuta akipingana na sheria kwa bahati mbaya,
amekaa mahabusu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi tisa hali ambayo
inaonesha kuwa tayali amekwisha jutia na kujifunza kuwa vitendo vya
kufanya makosa havilipi.

Sababu nyingine iliyotolewa na Jaji Mwikugine katika utoaji wa adhabu
hiyo ni pamoja na kuzingatia hoja za utetezi kuwa kitendo cha
mtuhumiwa huyo kukubali kufanya kosa hilo la kuua bila kukusudia pia
kimeonesha uungwana wake hali ambayo inaonesha kuwa amejutia kosa
alilo lifanya na ameipunguzia mahakama muda na gharama za uendeshaji
wa kesi hiyo.

Jaji Mwaikugile aliendelea kuleza kuwa kutokana na hali hiyo pia
pamoja na kuzingatia adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia usalama ya
Mtuhumiwa na jamii Kijiji kwake Mahakama hiyo imechukua mamuzi hayo
Awali akitoa hoja Mahakamani hapo kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo
Mwanasheria wa a Serikali Hamimu Nkoleye pamoja na mtuhumiwa huyo
kukiri kufanya kosa hilo dogo la kuua bila kukusudia aliiomba Mahakama
hiyo kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa
wakichukua sheria mkononi na kusababisha matukio ya mauaji kuongezeka
Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na taifa kwa ujumla.

Upande wa mjibu hoja uliowakilishwa na Wakili wa kujitegemea Dickson
Ndunguru aliiomba Mahakama hiyo kumpatia mteja wake adhabu yenye
unafuu na ikiwezekana afungwe kifungo cha nje.

Awali akimsomea Shitaka hilo ambalo mtuhumiwa huyo alikiri kulifanya
kwa maelekezo kuwa hakuwa anajitambua, Mwanasheria wa Serikali Hamimu
Nkoleye alidai mbele ya Jaji huyo kuwa Manyele ambaye alikuwa
akishuhudiwa na Mkewe Asha Mohamed Selemani alipiga na kumkalia chini
marehemu hadi walipofika wasamalia wema kuamulia ugomvi huo zikiwa ni
juhudi za shuhuda huyo kupiga kelele za kuomba msaada huo.

Nkoleye aliendela kufafanua kuwa Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mkazi
wa Kijiji cha Chikomo Wilayani humo alifanya kosa hilo wakati marehemu
akiwa katika mashamba yaliyopo Kijijini hapo ambapo alienda
kumtembelea kwa nia ya kudai deni hilo ambalo tayari akuwa amekwisha
jibiwa kuwa hatalipwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...