Saturday, September 14, 2013

RONALDO AMPOKEA BALE KWA KUMUUMIZA MAZOEZINI,JE NI MAKUSUDI KUTOKANA NA BALE KUMPIKU UTHAMANI AU BAHATI MBAYA TUU

1
Wachezaji wawili wenye historia ya kuweka rekodi ya kuwa wachezaji ghali kuliko wote hii leo wamekutana kwa mara ya kwanza kabla ya mazoezi ya timu yao .
Gareth Bale na Cristiano Ronaldo walikutana kwa mara ya kwanza tangu wakati Bale aliposajiliwa na Real Madrid toka klabu ya Tottenham Hotspurs .
Bale amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo baada ya usajili wake kwenda Real Madrid kuigharimu klabu hiyo ya Hispania paundi milioni 86 akiwa ameuzidi usajili wa Ronaldo kwa paundi mdilioni 6
.
2
Ronaldo na Bale dakika chache baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.
Bale na Ronaldo walikutana hii leo mapema dakika chache kabla ya kuanza kwa mazoezi ya Real Madrid wakiwa wamejiunga na klabu hiyo baada ya kuziacha kambi za timu zao za taifa .
Bale alicheza kwenye mechi mbili za Wales ikiwemo mechi dhidi ya Macedonia iliyochezwa jana huku Ronaldo akicheza na kuifungia Ureno kwenye mchezo dhidi ya Ireland Ya Kaskazini na aliukosa mchezo wa jana kati ya Ureno na Brazil.  


SIKU YA TATU MAZOEZINI MAMBO YAKAWA HIVI..
Katika siku ya tatu tu ya mazoezi yake kamili klabu hiyo mpya, Bale tangu ajiunge nayo kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 86, alijikuta akipitiwa kwanja na nyota huyo wa zamani wa Manchester United ambaye bila shaka alitaka kumuonyesha 'mchawi huyo wa Wales' kwamba si kazi rahisi kuwa mkali Real.
Pia Pepe alionekana kuchekelea wakati akiangalia Mreno mwenzake, Ronaldo akimtenda kitu Bale kwa kumrukia kwenye kifundo cha mguu.

That's just for starters: Cristiano Ronaldo looks up at Gareth Bale after making a sliding challenge
Cheki kitu hicho: Cristiano Ronaldo akimpitia miguuni Gareth Bale
Incoming: Ronaldo decides to launch into a slide tackle on Bale
Anamfuata: Ronaldo akimrukia Bale
Locked on: Ronaldo's boot is studs up but grounded as he homes in on Bale
Mguu umefika: Ronaldo akipeleka mguu wake kupitia mpira miguuni mwa Bale
Direct hit: Bale feels the full force as Ronaldo slides through his ankle
Maumivu: Bale akipewa kitu na Ronaldo 
Bale alionekana kuwa sawa tu baada ya kitendo hicho, lakini hakuonekana kuwa mwenye furaha baada ya hapo.
Ronaldo alikuwa anashikilia rekodi ya mchezaji ghali wa dunia wa awali kwa Pauni 80 alizonunuliwa kutoka Manchester United mwaka 2009 na kwa picha hizi inaweza kuchukuliwa kama ni wivu wake kwa mchezaji mwenzake mpya Bernabeu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...