Tuesday, April 30, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI MBEYA KWA ZIARA YA SIKU MBILI PIA KUWA MGENI RASMI KESHO KATIKA MEI MOSI


Rais Jakaya Kikwete, leo anaanza ziara ya siku mbili mkoani Mbeya ambapo pia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi.
Maadhimisho hayo kitaifa mwaka huu yanafanyika  mkoani Mbeya.

 Rais Kikwete, amewasili  kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe saa 4:30 asubuhi.
Awali mkuu wamkoa wa mbeya bw Abbas Kandoro aliwataka wananchi hasa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake, kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Kikwete katika maeneo yote aliyotarajia kupita akitokea Uwanja wa Ndege wa Songwe na pia kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe za Mei Mosi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala, alisema maandalizi ya sherehe hizo yapo katika hatua nzuri na kuwa anaamini kuwa kutokana na uwapo wa Rais Kikwete kama mgeni rasmi, yatafana kuliko miaka ya nyuma.

Alisema sherehe hizo zinaandaliwa na Tucta na kwa mwaka huu maandalizi yake yanaratibiwa na Chama cha Wafanyakazi wa Meli na Bandari (Dowuta), huku kukiwa na kauli mbiu isemayo: ‘Katiba mpya izingatie usawa na haki kwa tabaka la wafanyakazi’.

Mwakapa alitoa wito kwa waajiri wote kuwaruhusu na kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu katika sherehe hiyo ili wafikishe madai na vilio vyao kwa waajiri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...