Tuesday, April 16, 2013

SPIKA ATOA AGIZO KWA WABUNGE WANAOTUMIA LUGHA YA MATUSI NDANI YA BUNGE KUTOLEWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE NA ASKARI

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU MASUALA MBALI MBALI YANAYOJIRI BUNGENI.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Anne Makinda amesema kutokana na tabia ya baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi wakati wa vikao vya Bunge basi ataawaamuru askari wa Bunge kumtoa nje mbunge yeyote atakaetenda kosa hilo.
Mh Makinda amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo kufuatia jana baadhi ya wabunge kutumia lugha ambazo zimetafsiriwa kuwa ni za matusi na hazifai kutumika ndani ya Bunge hilo tukufu.
Jana Mbunge wa kondoa Mh Juma Nkamia alimwambia Mbunge wa mbeya mjini kuwa awe na adabu na kwamba hazungumzi na mbwa bali na mwenye mbwa hali iliyofanya baadhi ya wabunge kuomba muongozo wa kiti kwani walitafsiri kama wao ni mbwa,pia mbunge waIringa mjini Mh Peter Msigwa aliponukuu moja kati ya vipengele vya vitabu vitakatifu kuwa na kutumia neno la MPUMBAVU.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...